Ndani ya wiki moja nimeota ndoto ambayo watu wengine wameiota juu yangu

Kajeba

JF-Expert Member
Oct 15, 2020
804
1,945
Habari Jf
Hapa kuna wataalamu wa maswala ya ndoto, hizi tunazoota wakati tumelala usiku na pengine mchana

Ndoto hiyo sio mbaya inaonesha nimefanikiwa katika kutimiza lengo kubwa nililokuwa nimelipanga tena kiuhalisia naliona halitafanikiwa kwa sababu za kiuchumi

Nilianza kuota mimi, nikakaa kimya sikumsimulia mtu sababu siziamini ndoto

Baada kama siku mbili hivi akanipigia simu jamaa yangu tumepotezana zaidi ya miaka 6 sasa akaniambia ameota nimekamilisha jambo fulani ambalo hata yeye sijawahi mwambia na pia siongeagi nae mara nyingi

Mtu wa tatu ni kutoka familia yangu japo yeye niliwahi share nae wishes zangu, aliota ndoto nimefanikiwa!

Ndoto yenyewe ni kuanzisha biashara ambayo nilipiga hesabu kwa muda wa hivi karibuni haitawezekana
Yaani nimeota biashara inatoa pesa kila uchwao

Wataalamu nipeni mchanganuo wa ndoto hii
 
Back
Top Bottom