Ndani ya Serikali ya Tanzania kuna wasaliti ambao hawana utii sio tu kwa mamlaka, bali hata kwa kiongozi mkuu wa nchi

badison

JF-Expert Member
May 29, 2015
1,451
2,692
Kwa sasa Serikali ya Tanzania hasa Bara kuna wasaliti flani ambao ni wahaini hawana utii sio tu kwa mamlaka bali hata kwa kiongozi mkuu wa nchi. Ni wazi kuwa ile dhana inayoogopwa ya government inside the government inajionyesha sura yake katika uongozi wa serikali wa awamu ya sita.

Dhana ya serikali ndani ya serikali kwa lugha nyingine ni deep state. Kuna makundi mawili ambayo yanaongozwa na Clowns wanaojifanya wao wana akili sana kuliko Mamlaka za Nchi na mkuu wa nchi. Serikali ya awamu ya Tano ilijitahidi sana kupambana na hawa deep state na kupelekea mkuu wa Nchi Hayati JPM kutukanwa sana yeye pamoja na mama yake na kuchafua dhamira na taswira ya serikali yake.

Kuwepo kwa deep state kuna punguza nguvu yako kama mkuu wa nchi na pia kunawekwa ucheleweshwaji wa makusudi wa jitihada za serikali. Kwa sasa Tanzania hakuna deep state yoyote nihawa Clowns wahaini wachache ambao ni wasaliti. Hawa wasaliti makundi mawili ndio wanajifanya wao ndio deep state.

Wahaini hao ambao ni vikundi viwili vinavyo shindana kwa falsafa za kugawa nchi havina hatari wala ushawishi wowote. Sio kwa katiba hii ya mwaka 1977 tulionayo. Katiba hii inakupa mamlaka wewe kumchagua umtakaye na nani umuondoe.

Usije ukaingia kwenye mtego wa kuchagua kikundi utagawa chama chako na utaigawa serikali yako na utajichimbia anguko lako. Nakushauri waondoe hawa watu wa makundi haya katika uso wa siasa za Tanzania kama JPM alivyo fanya.

Hakuna anaye kupenda katika makundi hayo bali ni watu wenye tamaa kali na maslahi ya kutaka kushika nchi na kujinufaisha wao kama kikundi.. Makundi hayo ya wahaini na wasaliti wa serikali kuu wameanzisha hizo Cartel kwa lengo la kutaka kushika dola na kusaliti watanzania wote. Wanataka vikundi au kikundi kimoja wapo kiwe na monopoly katika siasa za tanzania ili tufanane na nchi kama kenya. Hii sio sawa na haikubaliki.

Muda sio mrefu wataanza kampeni za kusema nani anafaa kuwa raisi 2025 na kama utachelewa kuwaondoa hawa watu mapema utawapa ushawishi mkubwa sana.

Watu tunakuangalia wewe tuone utafanyaje kwani changamoto uliyokuwa nayo ni ndogo sana ondoa hofu wewe ndio mkuu wa nchi. Mimi sikushauri kitu ila jua kuna watu ni watiifu sana na hawana majina wala umaarufu wa kisiasa lakini uongozi wanaujua na wana mapenzi na nchi yao.

Kwa mwaka 2022 vunja hilo baraza na uondoe masalia ya awamu ya tano na pia uondoe viashiria vya awamu ya nne vinavyoanza kujitokeza sura yake katika serikali yako na kufanya uonekane kama haupo huru katika utawala wako.

Mamlaka unayo usimwogope mtu. Jeshi lipo chini yako na Idara ya usalama wa Taifa ipo chini yako na kama wananchi tuna kuheshimu na hizo mamlaka zinakuheahimu pia.

Hawa wahaini wamepanga kukusumbua sana mwaka 2022. Waondoe haraka dalili zao sio nzuri vunja baraza la mawaziri chagua watu ambao hawana makundi yoyote chagua watu watakao ona Vision yako ni wapi unataka kutupeleka.

Namalizia kwa kukupa tofauti kati ya siasa za Tanzania na Afrika Kusini. Hapa Tanzania hatuja tenganisha kofia ya uraisi na mwenyekiti wa chama ndio mana nguvu unayo na hawa Clowns unaweza kudeal nao haraka sana na kuwafuta kabisa. Afrika kusini wao wametenganisha kofia za uraisi na mwenyekiti wa chama ndio mana mwenyekiti wa chama ANC anaweza kushindana na Raisi.

Zingatia usijiunganishe na kundi lolote kati ya haya. Makundi mawili wala usipatane na adui yako ambao ni haya makundi. Hayo makundi wote ni maadui zako na ni maadui wa Taifa kwani mipango yao ni Uhaini. Kama watu ni maadui zako usijipatanishe nao Wamalize kabla hawajakumaliza.

Katiba ya Tanzania ni moja kati ya katiba bora ndio mana huwezi kuskia wala kuona migongano kati ya mihimili nakukumbusha yanayo tokea kenya ndio hayo yataanza kujitokeza hapa Tanzania. Wataanza kukuchafua na kukuzushia. Jiandae sasa Unaingia Vitani.

Watanzania watiifu tuna kupenda sana na tuna kuheshimu sana. Kama amirijeshi mkuu waadhibu hawa Clowns wasaliti bila kujali una historia nao gani adui yako ni yule mtu wa nyumbani kwako. 2025 sio mbali hata kama huna dhamira ya kuendelea kuongoza hakikisha hawa maaduni wa makundi haya mawili hawana nguvu wala ushawishi wowote 2025 usipo fanya hivo utaingiza serikali na chama chako katika mpasuko mkubwa sana.

Hi hayo tu.
 
Mama mzito sana kuchukua hatua, hapo tu ndo anaponichosha. Wananchi tuna imani naye sana lkn kuna maamuzi magumu anatakiwa kufanya, kwanza aondoe masalia yote ya Mwenda na pili asuke team yake mpya ya vijana/wazee wasio na makundi ndani ya serikali na chama. John alifanikiwa sana hapo kwenye kusuka team yake na mpaka kesho itabaki kuwa tiifu kwake hata kama hayupo. Wakati ni sasa, Mama akijivutavuta atachelewa.
 
Tatizo mnatumia hila nyingi kujipa hayo mamlaka ya urais, kama mtu umechaguliwa kihalali kwa kura za wanachama na kwa kura za wananchi hakuna mtu ndani ya serikali atakuyumbisha, mara utasikia hooo mimi nimeupata urais kwa ngekewa, mara hooo huu ni muhula wangu wa pili kwa hiyo napita bila kupingwa ndani ya chama. Kwa nchi za wenzetu zilizoendelea kiongozi anaweza kuitisha uchaguzi wa mapema kupima kama bado anakubalika........
 
Kwa kuwa ndugai anamawazo mbadala, anafaa kuchukuwa fomu ndani ya chama! Makinda unasemaje? Polepole unasemaje? Bashiru vipi? Naomba mawazo yenu!
 
Baba wa Taifa alisema kwamba vijana tusiwe waoga kusema mambo yanayohusu Taifa hili.

Katiba inayompa mamlaka Rais pia imewapa Raia haki ya kutoa maoni na kushiriki katika shughuli za kisiasa.

Hivyo kutoa maoni na kushiriki kwenye siasa sio kosa ni haki ya kikatiba.

Tatizo ni kuwa watawala wanaogopa sana kukosolewa na wapambe wao wanawaita wanaotumia haki zao za kikatiba kama wahaini kwakua eti maoni yanayotolewa hayampendezi bosi wao.

Nchi yetu wote hii.
 
Hahahaha ahahaha awaondoe wote masalia ya awamu ya tano!! Yeye siyo masalia?🤣🤣🤣🤣🤣
 
Mama mzito sana kuchukua hatua, hapo tu ndo anaponichosha. Wananchi tuna imani naye sana lkn kuna maamuzi magumu anatakiwa kufanya, kwanza aondoe masalia yote ya Mwenda na pili asuke team yake mpya ya vijana/wazee wasio na makundi ndani ya serikali na chama. John alifanikiwa sana hapo kwenye kusuka team yake na mpaka kesho itabaki kuwa tiifu kwake hata kama hayupo. Wakati ni sasa, Mama akijivutavuta atachelewa.
Hebu taja hayo masalia kisha na useme yeye Samia ni salia la nani
 
Baba wa Taifa alisema kwamba vijana tusiwe waoga kusema mambo yanayohusu Taifa hili.

Katiba inayompa mamlaka Rais pia imewapa Raia haki ya kutoa maoni na kushiriki katika shughuli za kisiasa.

Hivyo kutoa maoni na kushiriki kwenye siasa sio kosa ni haki ya kikatiba.

Tatizo ni kuwa watawala wanaogopa sana kukosolewa na wapambe wao wanawaita wanaotumia haki zao za kikatiba kama wahaini kwakua eti maoni yanayotolewa hayampendezi bosi wao.

Nchi yetu wote hii.
Mkuu kwema??hii comment umeandika wew?
 
Acha kumdanganya kama ingekuwa ni rahisi kihivyo angeshafanya hayo yote zamani sana, kumbuka kuna maisha baada ya Uraisi pia na kwamba hawezi kuwa raisi forever, hivyo akijenga maadui they will get back at her at some point in life, na akishaamua kufwata ushauri wako huwezi jua chaos atakayoitengeneza itaishia na yapi inaweza ikamgeuka pia kila kitu kinawezekana Dunia hii, tunaona kila siku waliokuwa na Magufuli wanavyomkana na kumgeuka nini kinakuthibitishia hawa wanaomsifu won’t turn against her ?

Kama una ushauri wa kumpa ni afwate na kuheshimu Katiba iliyompa Uraisi ambayo inatambua Mihimili iliyopo ambayo ni Serikali, Bunge na Mahakama, na Spika kama Mbunge hakuna kosa amefanya, amehoji maamuzi ya Serikali hajatukana wala kuvunjia heshima mtu.

Besides unamtaka awe Dikteta huku mkililia Katiba mpya?
 
Baba wa Taifa alisema kwamba vijana tusiwe waoga kusema mambo yanayohusu Taifa hili.

Katiba inayompa mamlaka Rais pia imewapa Raia haki ya kutoa maoni na kushiriki katika shughuli za kisiasa.

Hivyo kutoa maoni na kushiriki kwenye siasa sio kosa ni haki ya kikatiba.

Tatizo ni kuwa watawala wanaogopa sana kukosolewa na wapambe wao wanawaita wanaotumia haki zao za kikatiba kama wahaini kwakua eti maoni yanayotolewa hayampendezi bosi wao.

Nchi yetu wote hii.
Siku zinakwenda mbio sana kwa kweli. Mpaka wewe umejua hii nchi ni yetu sote na hakuna mwenye haki zaidi ya mwingine? Mpaka wewe umejua viongozi wa nchi kukosolewa na dhambi na anayekosoa anaitwa Mhaini? Mungu mkubwa aliyekuonesha maono hayo.
Umeeleza vizuri sana dhana ya Uhuru wa kujieleza na jinsi inavyosiginwa nchini, hali hii imeondoa waoga kwenye reli na kubaki kusifia hata yasiyostahili.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom