Ndani ya jiji la Dodoma baada ya miaka 26, asante Hayati Dkt. Magufuli

Elitwege

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
5,154
10,809
Hii mada inaonesha kumbe watu wengi bado wana mtazamo hasi dhidi ya mji wa Dodoma.

Binafsi mara ya kwanza nimefika Dodoma miaka 26 iliyopita. Kweli wakati huo maisha yalikuwa magumu sana kuishi Dodoma kwa sababu zifuatazo;

Mosi, mji ulikuwa ni mfinyu mno, ulikuwa unaweza kutumia dk zisizozidi 40 ukatembea mji mzima. Kipindi hicho hata daladala hazikuwepo.

Pili, maji yalikuwa ya shida sana kiasi kwamba tulilazimika kufukua makorongoni kutafuta maji. Hali hiyo ilichangia sana kuwepo kwa magonjwa mbalimbali ikiwemo ugonjwa wa macho, kipindupindu, homa ya matumbo n.k.

Tatu, sehemu kubwa ya mji ulikuwa ni jangwa hali iliyopelekea kuwa na hali mbaya ya hewa hasa kipindi cha kuanzia mwezi Mei hadi Julai.

Nne, mzunguko wa fedha ulikuwa mdogo kutokana na kukosekana kwa shughuli za uzalishaji mali.

Kuanzia mwaka 2018 hali imekuwa tofauti. Changamoto nilizozibainisha hapo juu sasa zimefanyiwa kazi. Mji umekuwa sana na miundombinu ya kisasa imewekwa.

Dodoma kwa sasa hakuna nyumba iliyokamilika yenye kuhitaji wapangapi ikakosa wapangaji tena kwa bei nzuri ukilinganisha na bei katika miji mingine ya nchi yetu.

Hata suala la usafiri sasa hivi limeboreshwa sana. Kwa upande wa usafiri wa anga, zamani ili kupanda ndege mfano kwenda Dar au kokote ilikubidi ukodi ndege nzima ambapo nakumbuka mwaka 2011 tulikuwa na na shida ya haraka kwenda Arusha ili ilibidi tukodi ndege nzima kwa Tshs 6,000,000/ kutoka shirika la ndege la MAF. Sasa hivi Dodoma kupitia mashirika ya ATCL na PRECISION karibu kila siku kuna safari za kwenda miji yote muhimu kutokea Dodoma tena kwa bei nafuu.

Dada hivi kupitia mpango kabambe wa kuendeleza mji wa Dodoma inatarajiwa kuanzishwa usafiri wa treni za mjini (commuter) utakaounganisha maeneo yote muhimu kuanzia Ikulu, mji wa kiserikali, uwanja wa ndege Msalata, stendi ya mkoa na mjini kati.

Pia sasa hivi serikali inaendelea na ujenzi wa majengo 24 ya ghorofa 6 ya wizara mbalimbali katika mji wa kiserikali Mtumba sambamba na ujenzi wa barabara za lami katika mji huo na maeneo mengine.

Jambo pekee linalohitaji kufanyiwa kazi na mamlaka za jiji na wakazi ni kuhakikisha tunaongeza kasi ya upandaji miti na kuitunza iliyopo kwani kupitia miti hiyo sasa hivi hali ya hewa na mandhari ya mji ni ya kuvutia tofauti na zamani. Pia mradi wa kuchukua maji ziwa Victoria na kuyaleta Dodoma ukitekelezwa kama serikali ilivyoahidi mji utakuwa wenye kuvutia zaidi kwani maji ya ziwa Victoria ni baridi kupita haya tunayoyatumia sasa.

Fursa za uwekezaji katika mji huu ni nyingi kuanzia nyumba za makazi, shule za binafsi, viwanda vya kukamua/ kusindika/ kukoboa mazao kama zabibu, alizeti, mahindi, mchele, ubuyu n.k. Pia kutokana na uwepo wa vyuo vingi kuku na mayai vinahitajika sana.

Dodoma sio pa kusimuliwa, fika mwenyewe ujionee na uwekeze kabla hujachelewa kwani miaka mitano ijayo hata Gaborone Botswana itakuwa imepitwa.
 
Tutamkumbuka kwa mengi mazuri hayati JPM. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Amina!
 
Mji wa serikali Dodoma, kweli kuna mambo makubwa na mazuri yanaendelea kufanyika, lakini hakuna jambo unaloweza fanya kwenye hii dunia likafunika uovu na ukatili dhidi ya binadamu wenzako kisa tu mna tofauti za mawazo, n.k.

Kweli mkuu, hata Marehemu Chacha Wangwe alipopishana mawazo na Mbowe ndipo kifo tata kikamkumba
 
Mji wa serikali Dodoma, kweli kuna mambo makubwa na mazuri yanaendelea kufanyika, lakini hakuna jambo unaloweza fanya kwenye hii dunia likafunika uovu na ukatili dhidi ya binadamu wenzako kisa tu mna tofauti za mawazo, n.k.
Angalau kwa leo umeenda sambamba na nafsi yako kwamba unamkubali Magufuli kimyakimya
 
Uliyesema ni kweli tupu Dodoma imebadilika sana na kuwa bora kuliko kipindi cha nyuma. Sasa hivi imeunganishwa na mikoa yote muhimu kwa njia za ardhini (barabara) na anga. Mji umependeza kweli kweli.
Wagogo tutembee vifua mbere serekali iko hapa.
#Tatizo la macho liko palepale kutokana na mionzi mikali ya madini fulani hususani kule Bahi chukua hatua
 
Mji wa serikali Dodoma, kweli kuna mambo makubwa na mazuri yanaendelea kufanyika, lakini hakuna jambo unaloweza fanya kwenye hii dunia likafunika uovu na ukatili dhidi ya binadamu wenzako kisa tu mna tofauti za mawazo, n.k.
Kama alivyokua anataka kufanya mwamba?
 
Dodoma bado sana ukipanda dala2 vi vibasi vidogo watu wmesongamana, wamechoka kusubiri abiria hadi saa nzima! Bado sana ddma na sijui kulikuwa na uharaka gani kuhamia hapa jangwani. Hakuna utalii, hakuna viwanda, hakuna misitu, ni vumbi kila mahali!

Ndo maana ofisi za mabalozi zimegoma kuhamia Ddoma! hata Samia karibu kila siku yuko Dar! mawawaziri na watendaji wengi ya serikali familia zao ziko Dar! Yaani mioyo yao iko Dar!

Huo ndi ukweli mchungu!
 
Back
Top Bottom