Ndalichako: Tumefuta rasmi wiki ya elimu, ilikuwa inatupotezea fedha nyingi

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,968


Waziri wa elimu Joyce Ndalichako amesema kuwa wamefuta wiki ya elimu kwa kuwa ilikuwa inapoteza fedha, na fedha hizo kiasi cha bilioni 1.2 zitatumika kuboresha miundombinu ya shule, aliyasema hayo alipokua mkoani Morogoro alipokuwa anatoa zawadi kwa wanafunzi, shule halmashauri na mikoa iliyofanya vizuri kwenye mitihani

Kwa maoni yangu: Naona hii wiki ilikuwa inapoteza hela kweli na isiishie kufuta hii tu hata nyingine kama wiki ya maji etc ambazo hutumia hela nyingi
 
Tunasubiri mitaala ya elimu isiyobagua watanzania kati ya wenye nacho na wasiokuwa nacho. Ondoa misululu ya vitabu tofauti kila shule, weka vitabu vinavyofanana kwa shule zote kitaifa.
 
Hawa kazi yao kuzifuta sherehe tu. Hivi mwenge wa uhuru wameshindwa kabisa kuutupa pale makumbusho? Huu ndo unateketeza pesa za wananchi kwa kiasi kikubwa kuliko hata hizo sherehe.
 
Kweli NCHI ni Rais utawala wa ... hizo pesa watu wangezipiga asubuhi wakilipana posho na per diem . Mwaka huu tutaheshimiana mjini hapa, ndio maana baa zinaendelea kufungwa mtaa kwa mtaa
 
Kuna vitu vingi vya kufuta nchi hii.

Kwenye maonesho ya Sabasaba huwa najiuliza idara za serikali, mashirika ya umma na vyuo vikuu wanaonesha biashara gani.

Kuna machache inawezekana lakini wengi wao hawana cha kuonesha kwa maana ya madhumuni ya maonesho ya biashara ya kimataifa.
 
Wafute na saba saba maana naonaga maadhimisho ni DSM tuu uku mikoani inakuwa hainaga maana
 
Washughulikie kuhusu text books, kuna mradi unaendelea unakuta vitabu say vya o-level history. Unakuta form 1 kitabu chake, form 2 kitabu chake... mpaka form4 chake. Kwa nini wasi tengeneze kitabu kimoja ambacho kikodetailed.

Na vitabu hivi viko very shallow knowledge wise, vinaongeza gharama kwa kutawanya kila mwaka chake na pengine inahitajika ununue kitabu zaidi ya kimoja kwa somo hilohilo. Huu ni mradi mwingine wa kinyonyaji utupiwe jicho na serikali.
 
Hawa kazi yao kuzifuta sherehe tu. Hivi mwenge wa uhuru wameshindwa kabisa kuutupa pale makumbusho? Huu ndo unateketeza pesa za wananchi kwa kiasi kikubwa kuliko hata hizo sherehe.
Mwenge wa Uhuru ni michango ya Wazalendo haihusiki kwny Bajeti za serikali. Kama wewe huipendi usichangie sie tunaoutaka acha tuendelee kuchangia
 
Back
Top Bottom