Ndalichako: Marufuku wasio na sifa kujiunga na masomo ya shahada kwa kupitia kozi za'foundation'

BAKOI

JF-Expert Member
Jan 31, 2016
1,213
2,326
Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Pro.Joyce Ndalichako amepiga marufuku wanafunzi wasio na sifa kujiunga kujiunga na masomo ya Shahada (degree) kwa kupitia Foundation Course (kwa wasiofaulu kidato cha sita).

Prof. Ndalichako amesema mfumo wa elimu huria umechangia kuzalisha wasomi butu kwa kupokea wanafunzi dhaifu kitaaluma.

Kuhusu "foundation courses" kwa wanafunzi wa kidato cha sita walioshindwa kupata sifa za kusoma degree, Ndalichako amesema Foundation course haimuongezei mtu sifa.

"Kama mtu amemaliza kidato cha 6 akashindwa kufikisha "points" za kujiunga chuo kikuu, asidahiliwe kwa kusoma foundatiom course. Anapaswa kurudia mtihani wa kidato cha 6 kwa sababu baraza la mitihani linatoa fursa ya kurudia mara nyingi iwezekanavyo. Foundation course haimuongezei mtu sifa kama hana sifa zinazotakiwa kitaaluma" Amesisitiza Ndalichako.



DAR ES SALAAM: Kwa mara nyingine, Waziri wa Elimu nchini Tanzania Profesa Joyce Ndalichako, ametoa tamko linalozua mjadala mkali nchini humo.

Mara hii, ikiwa yaliyomo katika Hotuba yake yatatekelezwa, utakuwa mwisho wa moja ya mifumo iliyokuwepo ambapo mwanafunzi aliyemaliza kidato cha nne angeweza kuamua kusoma ngazi ya Diploma yaani Stashahada badala ya kupitia katika ngazi ya kidato cha sita.

Waziri huyo wa Elimu anaongeza kuwa wanafunzi wasiofaulu katika kidato cha nne wamekuwa wakienda kusoma ngazi ya cheti, kisha Stashahada na baadaye wakipenya na kuelekea katika Shahada yaani digrii lakini sasa watalazimika kupitia katika ngazi ya kidato cha sita.

Ambao hawatapitia katika safari ya kidato cha sita ni wale watakaofaulu katika kidato cha nne na kuchaguliwa kwenda kusoma katika vyuo vya ufundi daraja la kati.

Mfumo mwingine pia utakaaoathirika ni ule ambao mwanafunzi aliyehitimu kidato cha sita lakini akashindwa kukamilisha vigezo kadhaa vinavyotakiwa katika vyuo vikuu alikuwa anapata nafasi ya kufanya masomo ya muda yaani ‘Foundation Course’ katika Chuo kikuu huria cha Tanzania na kama angefaulu angeruhusiwa kuendelea na masomo ngazi ya degree.

Baadhi ya wale walioijadili hotuba hiyo hasa kupitia katika mitandao ya kijamii walionekana kumnukuu Rais mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa ambaye hivi karibuni amesema njia bora ya kuboresha elimu nchini Tanzania ni wadau wa elimu kukutana katika meza ya mazungumzo ili wajadili changamoto zinazowakabili.

Waziri Ndalichako mara tu baada ya kuchukua madaraka aliondoa mfumo wa wastani wa pointi yaani GPA na kurudisha mfumo wa upangaji wa madaraja yaani division na katika kuhamasisha watu wafike ngazi ya chuo kikuu, katika siku za hivi karibuni Waziri huyo aliwatangazia wale wanaohitimu ngazi za chini za elimu kutovaa majoho na kofia kama wavaavyo wanaohitimu katika vyuo vikuu.

========

KANUSHO;

Habari hii imekanushwa na kutolewa ufafanuzi. Habari zaidi soma=>Wizara ya Elimu imekanusha kuhusu kuzuia wenye Diploma kwenda chuo kikuu
 
that means hata kama ukitaka kusoma certificate au diploma lazima uwe umesoma A LEVEL kwanza.. sasa ole wao wasibadili vigezo kwenye guidebooks wanazotoa.. mana kuna vyuo vilikatazwa kudahili wanafunzi at the end of the day watu wamedahiliwa kama kawaida.. hizi hotuba hewa zitaanza kukosa mashiko sasa.
 
Haya ni maneno ya BAKOI na mama Ndalichako hajayasema popote.
Hata hivyo sina imani na maamuzi mbali mbali yanayofanywa na viongozi wa hawamu hii
 
Haaaah yatakuwa maajabu mengine ya dunia.....

Hawa watu wanaharibu kila kitu sijui watajenga kipi cha maana miaka hii 5...
 
Mbona sijaona sehemu akitoa hiyo kauli kwenye hii video uliyoweka mkuu, au hii video ni ndefu umefupisha?
 
Haya ni maneno ya BAKOI na mama Ndalichako hajayasema popote.
Hata hivyo sina imani na maamuzi mbali mbali yanayofanywa na viongozi wa hawamu hii
Hayo ni maneno yangu kivipi??? Inamaana hiyo video unaniona Mimi au waziri wako wa elimu??

Kama video inamuonesha huyo mama na bado huamin Mimi nakwambia. """ KUNYWA MAJI NDUGU YANGU""" Utulie na diploma yako mtaani
 
that means hata kama ukitaka kusoma certificate au diploma lazima uwe umesoma A LEVEL kwanza.. sasa ole wao wasibadili vigezo kwenye guidebooks wanazotoa.. mana kuna vyuo vilikatazwa kudahili wanafunzi at the end of the day watu wamedahiliwa kama kawaida.. hizi hotuba hewa zitaanza kukosa mashiko sasa.
tuache kupotosha, prof kasema jambo la msingi haiwezekani mtu anaziro anaenda kusoma foundation course wiki tatu anadahiliwa chuo kikuu hapana, tusigeuze elimu kuwa biashara ya bodaboda.
 
Wanyime watu elimu uwatawale
Katika hili la diploma ajipange!!!!
Fight yake itahusisha silaha zote ukianzia na silaha za maombi mpaka zile za "tandauma mlango wa chuma.........

Bila kusahau za mila.
Msije kutulazimisha kusema RIP.
 

Hamjamuelewa Ndalichako hasa mleta mada, Hiyo form six ameitaja kama mfano tu hajasema kwenda chuo kikuu lazima upite form six,
Ametoa mfano kama mtu umefeli form six kwann usirudie mtihani badala ya kufanya foundation course?
Ina maana hata mwenye diploma akidhi vigezo ndio aende degree that's why wameweka kigezo cha GPA 3.0 kwahyo mwenye 2.7 hana vigezo na haruhusiwi kufanya foundation course.
 
Certificate na Diploma sio foundation course. Kwasababu na zenyewe zina sifa za kuingilia.
Foundation course inayotajwa hapo ni kwa vile vyuo vinavyopokea wanafunzi wasio na sifa za kudahiliwa level ya degree kwa mujibu wa TCU, halafu wanawapa hiyo foundation course then wanawadahili.
Ulikuwa ni uhuni tuuu. Kama vp waliopewa hizo degree wafutiwe tu, hakuna namna.
 
Back
Top Bottom