Ndalicha Chukua Chako Uende Zako | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndalicha Chukua Chako Uende Zako

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kigarama, Oct 9, 2008.

 1. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #1
  Oct 9, 2008
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Nimeandika Thread hii si kwa sababu Mitihani ya Taifa imevuja,bali kwa sababu katibu Mkuu wa baraza la Taifa la Mitihani anakanusha kwamba hakuna mitihani mingine iliyovuja zaidi ya ule wa Hisabati

  Muda mfupi uliopita nimetoka kuthibitisha mimi mwenyewe kwamba mtihani uliofanyika leo wa Geography (Jiografia) kwamba tangu juzi ulikuwa uko mitaani.

  Binafsi nilimtumia Mtahiniwa mmoja aniletee mtihani anaodhani umevuja kabla ya mtihani huo kufanyika,juzi aliniletea mtihani wa geography na leo baada ya mtihani huo kufanyika na mimi kupata nakala yake nimethibitisha kwamba mtihani wa leo unafanana kabisa na ule niliopewa juzi

  Naomba thread hii itumike kuweka ushahidi kwa wale wote wenye nao ili mwisho wa siku Ndalichako na wenzake wakubali kufuta mtihani mzima na kurudia siku utakaopangwa tena

  kupata wasomi wanaopatikana kwa kununua mitihani ni kuliangamiza taifa na si kulijenga. Mwalimu mmoja wa shule fulani ya Mbezi aliwagawiwa wanafunzi wake wote mtihani wa hisabati wa mwaka 1993 na mtihani kasora maswali mawili ndiyo uliotumiwa na NECTA kutunga mtihani wa mwaka huu

  Ndalichako NECTA si kampuni yako bianfsi bali ni mali ya watanzania wote kwa maslahi ya nchi yetu inaonekana pakushinda, chukua vitu vyako,uende zako
   
 2. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #2
  Oct 9, 2008
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,453
  Likes Received: 7,217
  Trophy Points: 280
  Hapa dawa ni ndogo kama kweli mitihani ambayo haijafanyika ipo mitihani ni kuianika!Maana hapa ni uzandiki huu!sasa maskini na mie wasio na uwezo wa kununua mitihani!ndo wanatolewa kafala!Watu wanatoka na A kumbe za kununua!nilifurahi sana 1998 ulivyofutwa!
   
 3. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #3
  Oct 9, 2008
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
   
 4. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #4
  Oct 9, 2008
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,435
  Likes Received: 2,310
  Trophy Points: 280
  Mkuu... huyu Ndalichako amekaririwa akisema tatizo lipo kwenye sheria... wanaokamatwa hawaadhibiwi. Yeye haoni tatizo ni wao NECTA kutowajibika ipasavyo... laa haula ....hawa ndio ma-doctor wa Tanzania...
   
 5. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #5
  Oct 9, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Wakubwa ni kwamba pepa zinavuja kuanzia shule ya msingi hadi vyuo vikuu, na hii kitu haijaanza leo. Kilichobadilika ni teknolojia ya habari tu, kwa hiyo hata wasio kwenye mtihani wanapata habari. Zamani hizi habari ziliishia huko mashuleni, na wale ambao hawajafanya mtihani walitunza siri ili hiyo "channel" ya pepa iendelee kudumu zamu yao ya kufanya mtihani ikifika nao waitumie. Mitihani ya kuvuja ilikuwa na majina mengi kama "nondo", "kirungu", kule chuo kikuu mlimani waliita "desa", Muhimbili waliita "mwezi" nk.

  Wavujishaji wakuu wa mitihani wako katika makundi kadhaa:
  1. Wafanyakazi wasio waaminifu wanaotaka kujipatia fedha kwa kuuza mitihani. Hawa wako katika sections mbalimbali katika process ile ya kuandaa mitihani kuanzia uchapaji, kurudufu, kufungasha, kusafirisha nk. Na hawa ni ngazi zote, shule ya msingi hadi university. Uzuri ni kwamba hawa ni rahisi kuwadhibiti kwa kuziba mianya yote na kuweka kanuni za usalama zinazozingatiwa na zinazoji-monitor zenyewe.
  2. Kundi la pili ni la wamiliki wa mashule na wakuu wa mashule wanaotaka kujenga sifa kuwa shule zao ni bora. Hawa hununua mitihani kwa gharama yoyote na kuifundisha mashuleni, na wala huwa hawaoni aibu kuwaambia wazazi waongeze michango ya "special tuition" kwa ajili ya watoto wenye mitihani (form 2, 4, 6). Kinachowawezesha hawa kufanikisha hii ni kupenyeza vigogo wa baraza la mitihani kwenye payroll za shule zao, kwa hiyo hizi paper zinatoka kwa wakuu wa Baraza la Mitihani, wale wenye dhamana ya mwisho kabisa ya kuaminiwa (actually wale wanaodhibiti wizi wa mitihani ndio wanaopelekea hawa jamaa hizo pepa). Mitihani ya namna hii inapovuja si rahisi kuonekana mizimamizima maana wahusika huwa wanakabidhi maswali kwa waalimu wa masomo, ambao wanayafundisha darasani kama "revision" za kawaida, kwa hiyo si rahisi kuwastukia. Tatizo linatokea wanapomkabidhi mwalimu paper nzima na yeye ana tamaa ya pesa, anauuza kwa dalali (au madalali) ambao wanaanza kuutembeza kama njugu, hapo ndio "soo" linabumburuka!
  3. Kundi la tatu ni wazazi wenye influence huko baraza la mitihani ambao wanaiba mitihani hiyo kwa ajili ya watoto wao. Hawa pia ni vigogo, na huipata kutoka kwa vigogo wa baraza. Anapofikisha mtihani nyumbani anamkabidhi mwanae anamwambia "ushindwe mwenyewe sasa!" Ikitokea mtoto hajiamini, anatafuta rafiki (au marafiki) anaoamini ni "kipanga" katika kila somo ili wamfundishe (siri imeanza kutoka hapo). Wakimaliza kufundishana, wanakumbuka "unajua tunaweza kutengeneza hela hapa?" Wanaanza biashara kuuzia wenzao.

  Udhibiti wa mitihani unatakiwa uanze kwanza na vigogo wa baraza la mitihani, maana hawa wengine wa chini wanaumiza vichwa kulinda mitihani ambayo ilishavuja kabla hawajakabidhiwa!

  (BTW hii ndio ilikuwa proposal yangu ya awali kwa ajili ya tasnifu yangu ya masomo ya uzamivu, lakini kutokana na "siasa" zilizomo ndani yake niliiacha maana uwezekano wa kuifanikisha ulikuwa mdogo sana. Changamoto kwa anayeipenda aichukue, awe jasiri!)
   
 6. Sam GM

  Sam GM JF-Expert Member

  #6
  Oct 9, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 536
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  I tend to believe that exams leakage has come to Tanzania as a problem due to the system breakdown. The ministry of education has no direction, first they remove six crucial subjects (Geography, Book keeping, History, Agriculture etc) from both primary and secondary schools witha lame justification that students have too many subjects that they need to study. Three years later they swallow their own puke by reversing the move. How did they justify both moves beats my understanding. My argument today is how do we rectify our education system when we seem to fix our problems with temporary solutions? where is the road map for the ministry to prepare competent qualified teachers for our schools? It really beats my understanding that an individual in the ministry can make all major decisions that affect education system of our country without feasibility studies or consultations!!!

  Kama system ndio mbaya haiwashughulikii wanaokamatwa kwa nini huyu bwana anayesema kuwa system ndio mbovu na ni mtu ana madaraka tena makubwa asifix tatizo hili?
   
 7. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #7
  Oct 9, 2008
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,435
  Likes Received: 2,310
  Trophy Points: 280
  ...........na channel nyingine ipo kwa wakuu wa shule kupanga na ma-
  invigilator.. mitihani inafunguliwa kabla (pale ilipohifadhiwa baada ya kusambazwa), inatolewa copy halafu inafungwa tena ki-ustadi.
   
 8. deny_all

  deny_all JF-Expert Member

  #8
  Oct 27, 2008
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 428
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kashfa ya mwaka Baraza la Mitihani

  2008-10-27 13:57:26
  Na Waandishi Wetu

  Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), limesambaza vyeti bandia vya matokeo ya kidato cha nne mwaka jana, (result slip) katika shule mbalimbali za sekondari nchini.

  Wanafunzi walioathirika na hatua hiyo, ni wale waliohitimu kidato cha nne mwaka jana, na baadhi yao wameanza kupata misukosuko, ikiwemo kufikishwa mahakamani kwa madai ya kughushi.

  Akizungumza na Nipashe nyumbani kwake Magomeni, mmoja wa wazazi wa wanafunzi hao, Rehema Mlata, alisema mtoto wake, Alexander Gundula (22), hivi sasa yupo mahabusu mjini Mbeya, kwa kosa lililofanywa na NECTA, kusambaza vyeti hivyo.

  Alexander alikuwa miongoni mwa askari wanafunzi katika Chuo cha Magereza Kiwira, mkoani Mbeya.

  Mlata, alisema Alexander alisoma na kuhitimu katika Shule ya Sekondari Azania, mkoani Dar es Salaam kati ya mwaka 2004 hadi 2007.

  Uongozi wa Azania, kupitia waraka wake wa Oktoba 3, mwaka huu kwa Mkuu wa Mafunzo, Chuo cha Magereza Kiwira, umethibitisha mwanafunzi huyo kusoma katika shule hiyo.

  Mlata alisema Alexander alichukua result slip shuleni hapo Februari mwaka huu, kwa ajili ya kujiunga na Magereza, na kwamba alifanikiwa kuanza mafunzo chuoni hapo.

  Alisema Septemba mwaka huu, Alexander alikamatwa mjini Mbeya na kufikishwa mahakamani, akidaiwa kughushi result slip yenye namba S0101/0032, aliyopewa na uongozi wa Azania.

  Ilidaiwa kuwa hatua hiyo ilifikiwa baada ya Magereza kuthibitishiwa na NECTA, kuwa cheti hicho kilikuwa na kasoro zilizokifanya kisifanane na vingine vilivyotolewa mwaka jana, hivyo kuamua kwamba kilikuwa cha kughushi.

  Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Magereza, ilimwandikia barua Alexander, yenye namba HQC.58/X1/287, ikielezea kuachishwa mafunzo kutokana na kosa la kughushi cheti hicho, na hivyo kukosa sifa ya kuajiriwa.

  Kufuatia uhakiki wa ajira uliofanywa na kamati ya uhakiki kutoka Makao Makuu ya Magereza kuanzia tarehe 31 Agosti mwaka 2008 hadi Septemba mwaka huu, imedhihirika kuwa cheti cha kufuzu masomo ni cha kughushi hivyo moja kwa moja unapoteza sifa za kuajiriwa kama askari Magereza, ilieleza sehemu ya barua hiyo iliyosainiwa na Kaimu Kamishna Mkuu wa Magereza, E.M. Nkuku.

  Mlata alisema alikwenda kuonana na uongozi wa Magereza jijini Dar es Salaam, na kujibiwa kwamba uthibitisho kwamba cheti hicho kilikuwa cha kughushi, ulitolewa na NECTA.

  Mzazi huyo alifanikiwa kupata nyaraka kadhaa zinazothibitisha kuwa result slip hiyo, ilitolewa katika Shule ya Sekondari Azania.

  Kwa upande wake, uongozi wa Azania uliandika barua tofauti, ikiwemo namba AZ/BMT/19, kwenda NECTA, ikieleza kuwa Alexander ni mwanafunzi halali wa shule hiyo na result slip husika ilikuwa halali na ilitolewa shuleni hapo.

  Lakini Magereza waliendelea na msimamo wao kwamba wamethibitishiwa na Baraza la Mitihani kuwa result slip hiyo ni feki, alisema.

  Mlata alionyesha barua ya Baraza kwenda Magereza inayotaka Alexander achukuliwe hatua za kisheria, ili iwe fundisho kwa wengine wenye kawaida ya kughushi.

  Hata hivyo, Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Azania, Benard Ngoze, alilithibitishia gazeti hili kuwa Alexander alikuwa mwanafunzi halali wa shule hiyo, na kwamba result slip iliyotolewa shuleni hapo ilitoka NECTA na si ya kughushi.

  Alisema vyeti hivyo vilipelekwa shuleni hapo na NECTA mwaka jana, na kwamba vijana wengi wanaokutwa navyo hivi sasa wanakamatwa na kufikishwa mahakamani.

  ``Zile result slip walileta wenywe Baraza kwa dispatch na tukazipokea, wanafunzi walikuwa wakija kila mtu kwa wakati wake, wanalipia Sh. 5,000 na kuchukua, sasa wanaziruka wakati zimetoka kwao?`` alihoji.

  Alisema alishaandika barua mara kadhaa kwa uongozi wa Baraza la Mitihani na Magereza kuthibitisha kuwa result slip ya Alexander ilipatikana kihalali shuleni hapo, lakini inashangaza kuona bado wahusika wanaendelea kumtia msukosuko kijana huyo.

  Baada ya kugundua kuwa ni kweli hizo result slip zimetoka kwao, Baraza walichukua nyingine 17 zilizobaki hapa shuleni na walisema wanaenda kuwashughulikia watu wa idara ya uchapaji, kwamba walihusika na udanganyifu huo, alisema.

  Alisema inawezekana watu wa idara hiyo katika Baraza, waliuza result slips halisi na kisha kuchapisha za kughushi na kusambaza katika shule mbalimbali nchini.

  Walipokuja hapa tuliwaambia watu wa Baraza kuwa wanastahili kushtakiwa kwa kutengeneza vyeti bandia hata sisi tumeanza kuogopa, kama taasisi nyeti kama hii inafanya vitu vya ajabu kama hivi nani tutakayewaamini, alihoji Mwalimu Ngoze.

  Baraza hilo limekiri kutokea kosa hilo katika barua yake ya Oktoba 13, mwaka huu, ikiwa na kumbukumbu namba MTS.2/14/Vol.L.IV/65, ya kumwomba radhi Alexander kwa kosa lililofanyika.

  Uchunguzi katika kumbukumbu za Baraza la Mitihani Tanzania umeonyesha kuwa result slip ya Alexander Gundula ni sahihi.

  Tayari tumemwandikia Kamishna Mkuu wa Magereza kumjulisha kuhusu uhalali wa result slip hiyo ambayo pia imerudishwa kwake tunaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza, ilisema barua hiyo iliyosainiwa na Kaputa kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dk Joyce Ndalichako.

  Ingawa Baraza hilo halikukiri moja kwa moja katika barua yake kuwa result slip hizo zilitolewa na Baraza hilo, maofisa wake waliokwenda shule ya Azania, walikiri kuwa zilitolewa na taasisi hiyo yenye jukumu la kuandaa mitihani nchini.

  Msemaji wa Magereza, Omari Mtiga, alisema uhakiki wa vyeti vya askari wanafunzi, ni mchakato wa kawaida unaofanywa na jeshi hilo.

  Mtiga aliyeahidi kulifutilia suala hilo kwa undani, alisema utaalamu wa kubaini ikiwa vyeti vilivyowasilishwa na wanafunzi ni sahihi ama vimeghushiwa, unafanywa na NECTA.

  Wakituambia kwamba cheti fulani kimeghushiwa, sisi tunaamini hivyo na hatua inayofuata ni kumfikisha mhusika katika vyombo vya sheria, alisema.

  Hata hivyo, Mtiga alionyesha kushangazwa na tukio hilo alilolifananisha na mchezo wa kuigiza, na kusema taarifa zaidi itatolewa leo.

  ``Njoo Jumatatu, mimi nitakuwa nimesafiri, lakini taarifa zaidi utazipata kwa huyu Kaziulaya, ni mmoja wa wasaidizi wangu,`` alisema.

  Kwa upande wake, Dk. Ndalichako hakuwa tayari kulizungumzia suala hilo, kwa madai kuwa halijui.

  ``Kuna maamuzi yanayofikiwa na wasaidizi wangu, naomba tuwasiliane kesho, nitakuwa nimelifuatilia na kukupa jibu, nipigie simu kabla hujaja ofisini kwangu,`` alisema.

  Hata hivyo, Nipashe ilipowasiliana naye kwa mujibu wa ahadi yake, Dk. Ndalichako alidai yupo kwenye mkutano, na baadaye alipopigiwa mara kadhaa, simu yake ya mkononi ilikuwa inaita bila kupokewa.
  Taarifa nyingine zilizopatikana hivi punde, zilidai kuwa, Magereza imeagiza Alexander kuripoti chuoni hapo na kuendelea na mafunzo, baada ya barua ya NECTA kuthibitisha kuwa result slip aliyonayo imetolewa na Baraza hilo.

  Imeandaliwa na Mashaka Mgeta na Joseph Mwendapole

  Source: Nipashe

  Hii nayo kali ya mwaka, Kijana Alexander tafuta wakili hao NECTA wamenunua kesi kwenye hili.
   
 9. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #9
  Oct 27, 2008
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Eeeheee, this is more than serious. Hii level ya incompetence na ufisadi katika nchi yetu mwisho wake ni wapi? Au tukubali tu kuwa ndivyo tulivyo??!
   
 10. Ladslaus Modest

  Ladslaus Modest JF-Expert Member

  #10
  Oct 27, 2008
  Joined: Jun 27, 2008
  Messages: 638
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mungu ibariki Tanzania,
  Mungu wabariki WaTanzania

  Mungu wageuze WaTanzania wawe na mioyo wa kuipenda nchi yao.
  Mungu wageuze WaTanzania wenye kupenda kupata bila kutoa jasho wawe na mioyo ya kuwa na 'kitu' chao na sio 'kitu' walichoandaliwa
  Mungu wageuze WaTanzania wasiopenda kufanya kazi wafanye kazi.
  Mungu wageuze WaTanzania wasiopenda kusoma na kutegemea kuiba mitihani wawe na moyo wa kupenda kufanya mitihani kwa kutoa majibu vichwani mwao, na wafanye mtihani ambao hawajauona kabla.

  Mungu Ibariki Tanzania,
  Mungu wabariki WaTanzania

  Mungu wawezeshe WaTanzania Mafisadi kuacha Ufisadi
  Mungu wawezeshe WaTanzania Wezi kuacha kuiba.

  Mungu Ibariki Tanzania
  Mungu Wabariki WaTanzania.
   
 11. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #11
  Oct 27, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Huu ulikuwa mchezo wa kuigiza ukimhusisha character anaitwa Alexander au ni habari ya kweli?
  Wanasheria mnasemaje? Je hapa huyu Alexander basi aishie hapa tu kwa kurudi chuo cha magereza? au ajipatie fidia kwa usumbufu na kuswekwa rumande bila kosa?
  Ebu tuhabarisheni!
   
Loading...