Nchimbi: Viongozi wa CHADEMA watahojiwa juu ya kutishiwa kwao kuuwawa.

Akiongea leo na tbc1 waziri wa mambo ya ndani dr.Nchimbi amesema;
Shutuma walizo zitoa viongozi wa chadema kuhusu kutishiwa kuuwawa ni nzito sana. Amesema japo chadema hawajawapa tarifa serikalini, lakini yeye kwa niaba ya serikali hilo swala litafanyiwa kazi kwani ni wajibu wa serikali kulinda wananchi wake. Na tayari ameshaagiza wote walio toa shutuma hizo wahojiwe.
Usikose kuangalia kipindi cha mahojiano kati ya dr.Nchimbi na Tbc1 ifikapo saa tano kamili usiku huu.
Ni hayo tu.

Nchimbi ni mratibu mkuu wa mauaji na utekaji nyara unaofanywa na CCM, wajihadhari naye.
 
Hivi hawa viongozi wa ccm ukilaza imekuwa ni itikadi ya chama? Yaani nyie ndo watuhumiwa, halafu na wahojaji ndo ninyi hao hao?! Hivi hiyo taarifa ya mahojiano ataiamini nani?
 
Na ikithibitika ni hadithi za kutunga washtakiwe

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Yap kasema wanatafuta umaarufu kwa kuwa hawataki kutoa ripoti polisi wanakimbilia vyombo vya habari ili kuchafua hali ya hewa ya nchi.

Wanafanya hivyo kwa sababu jukumu la ulinzi ni la wananchi wote, hivyo sio mbaya kutangaza kwenye vyombo vya habari. Nyie mnataka iwe siri, mmechelewa wazee wa Mabwepande.
 
Mwanzoni aliongea vizuri aliposema ni jukumu la serikali kutoa ulinzi kwa raia wote wa Tanzania. Kumbe hii ilikuwa geresha tu, somewhere in the middle akaanza kuonesha bias yake - kwamba wanajitafutia umaarufu kwa kujenga hofu kwa wananchi. Yaani, ameshajua kuwa hawatishiwi kuuawa. Sasa huko kuhojiwa anakosema kunatokana na nini?

Mwenyewe nlimshangaa. Anakua Muongo wakati hana kumbukumbu. yaani ni sawa na kupiga salakasi wakati amevaa taulo.
 
Hivi ilo ni la kuhoji wakati walishaanza kwa kumsaka Dr.slaa na vinasa sauti kwenye vitanda gesti,,,mbona hawakutolea maelezo,,ilo dogo tu,waliingia mitini sembuse ili kubwa la kuangamiza!Nchimbi atoe us....ng...e wake watanzania wa leo sio wale miaka ya 1970
 
Nchimbi ana onekana kujua kinacho endelea maana kwa maneno aliyo sema utafikiri amesha fanya uchunguzi!

Yan hapo hakuna uchunguzi ni uzushi tu ndio watauleta, mtu kama nchimbi ni mnafiki hadi kwenye macho!

Wanaona soo deal limesanuka sasa hawana pakushika!
 
Hilo la Dr Uli tu mpaka sasa limewashinda pamoja na ushahidi dhahiri uliopo! Litakuwa hili?
 
[h=6]tamko toka ikulu

katibu mkuu kiongozi balozi ombeni sefue atamka kwamba hakuna mpango wowote unaoratibiwa na idara ya usalama wa taifa kwa ajili ya kuwaua viongozi wa chadema.
Huku akihoji sababu za serikali kutaka kuwaua viongozi wakati si tishio lolote kwa wananchi huku akisema idara ya usalama wa taifa haiko kwa ajili ya kuua raia au viongozi bali kulinda maslahi ya taifa sasa kwa nini wawaue wana nini hasa idara ya usalama wa taifa ifanye hivo, idara hii haifanyi kazi kisiasa inaangalia maslahi ya watz wote.[/h]
 
Chakufurahisha ni kwamba "mission" ya wauaji ime "backfire". sasa wanajiosha nyang'au wakubwa. Message send!

Tanzania nchi yangu nakuhurumia na ninajihurumia maaana HATUNA VIONGOZI KABISA. Huyu Nchimbi dokta fake hana lolote atakalofanya. Yaleyale ya Dr.Mwakyembe kuwa Tanzania ndiyo nchi pekee duniani ambayo mtu ukipeleka tuhuma Polisi unaambiwa ulete ushahidi. Kwamba viongozi wa CDM wametoa tuhuma na wanasema hawana imani na Jeshi la Polisi halafu yeye anaangiza haohao Polisi wakawahoji viongozi waliotoa tuhuma hizo! Ajabu kwelikweli.

Hawa viongozi wa CHADEMA siyo vichaa au wendawazimu kwamba wanaweza tu wakaamuka na kutoa tuhuma nzito kama hizo tena WAMETAJA NA MAJINA?JINA la vigogo/kigogo ambaye yuko nyuma ya mpango huu(MASTER PLAN).Hatujasikia Nchimbi akisema kuwa na hao vigogo waliotajwa kuhusishwa na tuhuma hizi wahojiwe!!!Kwanini?

Nchimbi aache kufanya kazi kwa mazoea. Maana ni wazi kabisa kuwa Polisi hawatakubaliana na tuhuma hizo badala yake mwisho wa siku watasema ni uzushi na uongo. Nchimbi mwenyewe tayari keshawaita viongozi wa CDM ati ni wazee wa tuhuma! Is he really serious? Watu wanatishiwa maisha wewe unakuja na porojo kweli?? This is NONsense!

Polisi hawahawa juzi wameng'ang'ania kufanya uchunguzi wa kuwatafuta watu(Polisi/TISS?) waliomteka Dr.Ulimboka pamoja na kushauriwa kuwa iundwe Tume Huru maana wao ni watuhumiwa namba 1! MPAKA LEO TUNAPOZUNGUMZA HAKUNA HATA MTU MMOJA ALIYETIWA MBARONI KUHUSIANA NA UTEKAJI WA DR.ULIMBOKA! Kwa hiyo Polisi hapa wanafanya mchezo wa kuigiza tu BUT THEY REALLY KNOW WHO ARE THE SUSPECTS AND RESPONSIBLE HOOLIGANS WHO ARE DOING THIS KIND OF A NASTY BUSINESS!

ONYO KWA VIONGOZI WA CHADEMA
: Iweni makini sana pale mtakapohojiwa na hawa Polisi au Mashushu maana huenda tayari watakuwa wamesha andaa sumu zao kuja kuwamaliza polepole. Mna haki ya kuwakataa hao Polisi/Mashushu na kuomba msaada wa Wanasheria/Mawakili wenu ili kujiridhisha na usalama wenu. Hii nchi sasa hakuna wa kumwamini hasa viongozi wa CCM na Serikali yake!
 
tamko toka ikulu

katibu mkuu kiongozi balozi ombeni sefue atamka kwamba hakuna mpango wowote unaoratibiwa na idara ya usalama wa taifa kwa ajili ya kuwaua viongozi wa chadema.
Huku akihoji sababu za serikali kutaka kuwaua viongozi wakati si tishio lolote kwa wananchi huku akisema idara ya usalama wa taifa haiko kwa ajili ya kuua raia au viongozi bali kulinda maslahi ya taifa sasa kwa nini wawaue wana nini hasa idara ya usalama wa taifa ifanye hivo, idara hii haifanyi kazi kisiasa inaangalia maslahi ya watz wote.

Kama UWT hawako kwa ajili ya kuua raia hawa waliomteka Dr.Ulimboka na walitoka Ikulu walikuwa wanafanya nini? Balozi Sifui atuambie KWANINI MPAKA SASA HAKUNA HATA MTUHUMIWA 1 ALIYEKAMATWA? HII NI ISHARA TOSHA KASBISA KUWA UWT WANAHUSIKA NA UTEKAJI,UTESAJI NA UUAJI WA RAIA WASIO NA HATIA HASA PALE WANAPO ONYESHA KUWA NI THREAT KWA CHAMA TAWALA!

BALOZI SIFUI ASITAKE KUDANGANYA WATU HAPA IKULU NA UWT WANAHUSIKA NA MIKAKATI YA UTEKAJI NA MAUAJI YA VIONGOZI NA WANACHAMA WA UPINZANI. Huu ni ukweli mchungu ambao CCM lazima waumeze.
 
Chadema kwa stori za kujiliwaza hawajambo.

Wewe nani kakwambia mimi CHADEMA?, sikujui hunijui hiyo kadi ya CHADEMA ulinipa wewe?

Usidhani kila anaepingana na upuuzi wa CCM basi ni CHADEMA. Mimi sina kadi ya chama chochote cha siasa. Huu ndiyo upuuzi tunaouongelea yaani kwa kuwa wewe ni CCM hata ukiona mpuuzi wa CCM anafanya uchafu utamsifia tu kwa kuwa ni CCM.

Hii nchi ina watu wengi sana ambao si wananchama wa chama chochote ambao hawaridhishwi na misuse of power inayofanywa na watu waliopewa dhamana.

Baba wa Taifa aliwaita watu kama hawa ni wahuni.
 
Akiongea leo na TBC1 waziri wa mambo ya ndani Dr. Nchimbi amesema;
Shutuma walizo zitoa viongozi wa chadema kuhusu kutishiwa kuuwawa ni nzito sana. Amesema japo chadema hawajawapa tarifa serikalini, lakini yeye kwa niaba ya serikali hilo swala litafanyiwa kazi kwani ni wajibu wa serikali kulinda wananchi wake. Na tayari ameshaagiza wote walio toa shutuma hizo wahojiwe.

Usikose kuangalia kipindi cha mahojiano kati ya dr.Nchimbi na Tbc1 ifikapo saa tano kamili usiku huu.
Ni hayo tu.

Hivi Mhe. Sam six kuhusu Mwakyembe wamekwisha mhoji?
 
Mkuu hii inanikumbusha teja mmoja alikuwa na tabia ya kupitia viatu nje ya mlango wangu, sasa kuna siku ile natoka nje nakutana nae uso kwa uso ananyemelea viatu na kwa kuwa hakuna njia ya kupita akajifanya amepotea nyumba na kumuulizia mtu ambaye wala simfahamu. Nilipombana sana akakiri kuwa ni yeye ambaye huwa anachukua viatu mlangoni ila ni kwa ajili ya njaa na kuniahidi kuwa atahakikisha hakuna kibaka mwingine anachukua viatu pale...
Sasa najua kwa nini raia kama wana 'tip' fulani ya uhalifu wanaogopa kutoa taarifa polisi maana kibao kinaweza kuwageukia.

Baada ya polisi kufanya kazi yao ya kupeleleza, wanaanza kukuandama wewe uliyetoa taarifa. Hivi Tanzania tumelogwa na nani? Kwa style hii hakuna atakayekuwa tayari kutoa ushirikiano kwa polisi!

Ndiyo maana hata 'approach' ya ulinzi shiriki kwa vile ni 'top-down approach' ni "mbio za sakafuni huishia ukingoni".
 
Hata wakipewa viti wasikae, waende na viti vyao, wasije wakakalia sindano za sumu, wawe na maji yao, wawekewe tape recorder kwa mbali kiasi, wasitumie vipaza sauti vya huko, kama vipi, now waanze kutembea na vipaza sauti vyao kila mahali, hadi Bungeni, wasitumie vile vya Bungeni, wawe na vya kwao binafsi wanavyoviweka just kwenye mabegi yao, kama wakiamua tu kwenda polisi, though hawana msaada wowote kiukweli kwa watu wasio wa chama tawala, chumba watakachokuwemo wahakikishe kiwe na madirisha makubwa ya kutosha, wasije wakajitoa mhanga kufa nao kwa kutumia gesi ya sumu, wawe na bodyguards wa kutosha kwenye misongamano kiasi na mikubwa ya watu, hata wanapokuwa njiani, bodyguards wanaowaamini kwa kiasi kikubwa, wasije wakachomwa sindano za sumu, kwenye misongamano ya watu wengi, hao washenzi, wanaweza kufanya uhalifu wao maeneo kama hayo, hata kama wataenda kwa hao polisi, pia wawe makini sana, bodyguards wa kutosha kupambana na lolote wakati nje Wananchi watazunguka hiyo ofisi ya polisi kinoma, ukitokea ujinga polisi watajuuuta!

Unajua wewe unaongelea zaidi sinema na tasnia ya maigizo.....mawazo yako na ushauri wako ni full nadharia tu ambazo hazipo kwenye real world.
 
Nchimbi hana moral right ya kuchunguza,kuhoji wala kusemea maswala ya haya.. otherwise anapaswa kuelezea vifo vilivyotokea kama cha
  1. Salome Mbatia
  2. Ipyana Malecela
  3. Amina Chifupa
  4. Ulimboka etc
ndipo aje awahoji viongozi wa Chadema. Afteral hiyo ni trick ya kujua sources za information za Chama and i hope wamemshtukia tayari

Naona umetangaza kifo cha Ulimboka kwenye list yako kama namba 3,hii ni breaking news hatukujua kama amekufa kama ulivyoandika
 
Kwa hili la nchimbi na serikali nasema hivi, " Ni rahisi jua kuchomoza upande wa magharibi na kuzama upande wa mashariki kuliko Serikali ya magamba kulitendea kazi suala hili kwa ukweli na uwazi". Hiyo ni danganya toto ya serikali. Watakuja na matokeo yanayosema: "Tumebaini kwamba ni uzushi tu na hakuna ukweli wowote". Hili ndilo litakalokuwa jibu la uchunguzi wao. Hivi inawezekana hata siku moja shetani akafanya jitihada za kutafuta tiba ya dhambi ili kuhakikisha inatokomezwa ulimwenguni? Kama kweli shetani anaweza kufanya hivyo basi hata CCM wanaweza kushughulikia matatizo na shida za wapinzani kwa moyo.

lakini hivi serikali isingesema kituwatu wangesema hawajali raia wake, imetoa tamko la kufanya uchunguzi watu bado wanasema hakuna lolote, tumekuwa washabiki sana hata ktka mambo ya kiusalama tuache ushabiki wana JF.
 
Back
Top Bottom