Nchimbi: Tupo tayari serikali kukaa pamoja na vikundi/taasisi za kidini

Unajitahidi kuandika ila inaonekana sio mfatiliaji? ponda na wenzake tunaomuunga mkono tumeomba taasisi yetu isajiliwe lakini serikali inakataa jaribu kufatilia hilo utaugundua ukweli.

Na kama umenisoma vizuri nimeuliza nimeuliza under Islam kuna makundi (naombe niite denominations) mangapi? Ni Sunni na Shia tu au kuna zaidi? Na Ponda anawakilisha kundi gani?

Kwa mfano huwezi kukuta Catholic church ina mabaraza zaidi ya moja. Je Ponda anataka kuvunja BAKWATA au anataka kusajili Baraza jingine in addition to BAKWATA? Na kwanini alikataliwa? Waliomkatalia waliamuambia nini specifically?
 
Shari unaijua na kuiweza wewe?? Unaclick simu yako tu unadhan maisha rahis hivyo!! Na isitoshe hata nchini haupo hapa kazi kuchochea tu ili mpewe ukimbizi huko! Nimegundua wengi wa watoa porojo humu hawapo nchini na wanaombea kinuke wapate hifadhi ya kudumu huko,njoo ulingoni hapa
ww ndiye uko nje ya nchi!!!!! mimi na ndugu zangu niko/wapo hapahapa TANZANIA, na siondoki kesho wala kesho kutwa.

Na hakuna kauli ya kichochezi niliyotoa hapo, vinginevyo una matatizo ya kuelewa hoja, haiwezekani mtu azuie sensa, tuseme asante, avamia mali za watu, tuseme asante, atishie kuua tuseme asante, wengine wachome makanisa kwa 7bu za kitoto tuseme asante. LABDA KAMA SERIKALI YETU IMEAMUA KULEA MAKUNDI YA WAHALIFU ITAFANYA NAO MAZUNGUMZO, lkn ikiwa sio, ajenda hiyo ife natural death na aliyeshauri hili kampotosha waziri.

rafiki yangu kwa taarifa yako ni marafiki kibao ambao ni Muslims na kilichoniunganisha nao sio uislam wao bali UTANZANIA na hawaungi mkono ujinga huu. ww unaonekana ni miongoni mwa waathirika wa huu ujinga unaonekana uko hapa kuseek sympathy ili ndugu zako waliofanya uhalifu waachiwe bila masharti, hilo sahau, imekula kwao, serikali makini haiwezi kuwaachia wahalifu hawa ng'o.

Hivi ww kwa akili yako uliyo nayo ni busara kufanya mazungumzo na mtu aliyekuibia badala ya kumpeleka mahakamani, anyway it can happen in TANZANIA but only in TZ,
 
Hii ndio shida ya kubebwa (Uwaziri, Mzumbe PhD na Ubunge) in really world, Nchimbi mweupe tena fedheha
 
Mkuu chama ni vikundi gani vya kidini zaidi ya Uamusho na Shekhe ponda&co vilivyoleta vurugu Tanzania.?

Amani haipatikani kwa kuongea na waleta vurugu tu hata wale wanaofanyiwa vurugu wana nafasi kubwa sana kudumisha amani.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Amani haipatikani kwa kuongea na waleta vurugu tu hata wale wanaofanyiwa vurugu wana nafasi kubwa sana kudumisha amani.

Chama
Gongo la mboto DSM

mkuu kama ni hivyo tupe madai ya wafanya vurugu na wafanyiwa vurugu tupate kuchanganua. Kwa ninavyojua wafanya vurugu ndio waliofanya vurugu kariakoo na wachache wao walivamia ikulu hadi wakakamatwa,ambao ndio Ponda &co. Kwani ni lini waliwai kuomba kukutana serikali wakakataliwa hadi wafanye vurugu ndipo wasikilizwe.!!
 
Tatizo la Waislamu ni BAKWATA + CCM. Serikali ya CCM inawalazimisha Waislamu wote kua chini ya BAKWATA wakati upande wa pili wa Wakristo kuna Mabaraza mengi tu ya kuwasimamia.

Upo ushahidi kua kuna taasisi nyingi tu zinashindwa kutoa misaada mbalimbali kwa Waislamu kwa kulazimika kupitia Bakwata wakati hawaiamini.

Bakwata ndio iliyouza kwa Manji kiwanja cha waislamu cha Chang'ombe kwa bei ya kutupa. Lakini kama kungekua na mabaraza mengine Huru, hili lisingetokea kwa urahisi.

Serikali ya CCM kama inania ya dhati ya kumaliza haya matatizo basi iondoe monopolistic kwa hili baraza juu ya affairs za Waislam.

Tukianza hapo kwanza, mengine pia yatafuata maana naamini waislam wana hoja nyingi tu za kusikilizwa.
Umasikini ni kitu kibaya sana, umaskini unapofanikiwa kuua moyo na akili ya kujitegemea na kuanza kutegemea misaada kiasi cha kujidharirisha hapo inakuwa mbaya zaidi. Kumbe makelele na fujo zote hizo ni kwa kutaka kutembeza bakuli " what a shame!"
 
Huu utayari umekuja lini na kwa nini? halafu watakaa chini wakishainuka kiwe nini? Itabidi tuwasaidie kweli kuwapa mawazo ya kulitoa taifa kwenye udini ambao wameliingiza.
 
QUOTE=mnyanyaswaji;4867959]Amesema kama serikali hatupo tayari kusubiri watu wauwane ndipo tuseme tukae chini,inatosha na wapo tayari kukaa kimazungumzo na taasisi za kidini.
My take: kauli kama hii ilitakiwa mapema mnoo na sio mpaka watu walaluwane, na isiwe kwenye dini hata siasa na mambo mengine.
Source Channel Ten Habari saa moja.

Nawakilisha[/QUOTE]

Mmmh Yasije yakawa ya Ulimboka. Bakwata ni ulaji wa wachache, kwa serikali hii sidhani kuna kitakachobadilika. Isije ikawa ndio opportunity yakuwindana; baada ya mazungumzo tunasikia watu wameokotwa mahali. Sijawahi kuona serikali hii imekaa na kundi lolote kitu kikawa productive au kukafikiwa makubaliano fulani. Well we will see.
 
Ngoja Taasisi za Dini za Kienyeji nazo ziamke ndio atajua vizuri na sisi Judaism asinisahahu Sikukuu zetu haziheshimiwi kabisa Majuzi tulisheherekea Mwaka mpya hapa Tanzania watu wakawa hawajali kabisa...
 
Huu utayari umekuja lini na kwa nini? halafu watakaa chini wakishainuka kiwe nini? Itabidi tuwasaidie kweli kuwapa mawazo ya kulitoa taifa kwenye udini ambao wameliingiza.
Umshauri nini wakati hata mkutano bado? We kama mjuzi sana/mshauri mzuri ingia kwenye kikao uliza dukuduku zako kama mwanajopo utapewa majibu na ushahidi wa wazi. Sawa MMK?
 
ww ndiye uko nje ya nchi!!!!! mimi na ndugu zangu niko/wapo hapahapa TANZANIA, na siondoki kesho wala kesho kutwa.

Na hakuna kauli ya kichochezi niliyotoa hapo, vinginevyo una matatizo ya kuelewa hoja, haiwezekani mtu azuie sensa, tuseme asante, avamia mali za watu, tuseme asante, atishie kuua tuseme asante, wengine wachome makanisa kwa 7bu za kitoto tuseme asante. LABDA KAMA SERIKALI YETU IMEAMUA KULEA MAKUNDI YA WAHALIFU ITAFANYA NAO MAZUNGUMZO, lkn ikiwa sio, ajenda hiyo ife natural death na aliyeshauri hili kampotosha waziri.

rafiki yangu kwa taarifa yako ni marafiki kibao ambao ni Muslims na kilichoniunganisha nao sio uislam wao bali UTANZANIA na hawaungi mkono ujinga huu. ww unaonekana ni miongoni mwa waathirika wa huu ujinga unaonekana uko hapa kuseek sympathy ili ndugu zako waliofanya uhalifu waachiwe bila masharti, hilo sahau, imekula kwao, serikali makini haiwezi kuwaachia wahalifu hawa ng'o.

Hivi ww kwa akili yako uliyo nayo ni busara kufanya mazungumzo na mtu aliyekuibia badala ya kumpeleka mahakamani, anyway it can happen in TANZANIA but only in TZ,
Naona unajieleza mpaka povu linamwagika, ni hivi kwenye maisha usiangalie Results angalia source yake ni nini. Sasa uliyoorodhesha wewe yooote ni matokeo je chanzo unajua? Hapo ndo wenye akili kama akina Nchimbi wakaona bora wakae nao kitako, endelea na unazi wako wa...
 
waongee nini na vikundi vya kidini.? Haoni kama ni kuhalalisha udini.?....akianza kusikiliza vikundi vya kidini vya kiislamu sawa na kuhalalisha makundi ya kidini tanzania na ndio mwisho wa tanzania moja.!

Hebu tufafanulie kuhusu kuhalalisha udini ktk suluhisho hili.Na je wewe kama wewe unatakaje,violence iendelee na mwishowe ni nini?Au unataka nchi ikatike vipande viwili yaani pwani na bara kila mtu kivyake?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom