Nchimbi na mchakato wa vazi la taifa ni kupoteza wakati na pesa za walipa kodi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nchimbi na mchakato wa vazi la taifa ni kupoteza wakati na pesa za walipa kodi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by jiwe1, Jan 18, 2012.

 1. j

  jiwe1 New Member

  #1
  Jan 18, 2012
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimekuwa karibu kufuatilian mchakato mzima wa kutafuta vazi la taifa ulianzishwa na muheshiwa Emmanuel Nchimbi waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.Kwa upande wangu sidhani kama huu mchakato una maana sana na faida juu ya taifa la tanzania hasa ukizingatia kipindi hiki ambacho nchi imekuwa hoi sana kiuchumi,kisiasa na hususani swala ambalo linaikabili wizara yake la ajira kwa vijana.Nimejiuliza maswali mengi sana tena sana baada ya vazi la taifa kupatikana ni kipi tutafaidika na hilo vazi la taifa?kwa kweli sijapata jibu hata moja.Kwa upande wangu nadhani viongozi wa serikali waangalie sana kufanya vitu vitakavyoleta faida kwenye nchi.viongozi wengi wa serikali wanakimbia changamoto ngumu na kufanya vitu ambavyo havina maana yeyote na mwishowe vinawashushia heshima na kudharauliwa na kuonekana wana uwezo mdogo sana wa kufikiri.
  Kwa upande wangu binafsi ningefurahi sana kama muheshimiwa nchimbi angetumia nguvu nyingi sana kupambana na watu wanawaibia wasanii katika kazi zao sanaa maita zake zingezaa mana labda vita vyake vingezaa matunda na kufanya hivyo vijana wengi wangepata ajiri kwa kuweka sawa sector ya sanaa.kivipi?kwa mfano kama angeweza kufanya sanaa ikawalipa vizuri wasanii kwa kupambana na mafisadi wa muziki hawa wasanii wangeajiri wenzao kibao mfano msanii kama jay z, ana walinzi sio mmoja sio wawili,ana ma dj, ana fashion designers,ana madereva hawa wote wanalipwa na masanii mmoja unaweza kukuta msanii mmoja ana wafanyakazi zaidi ya 200 hizi zote ni ajira na hasa kwa vijana.
  muheshimiwa badala ya kuwakumbatia hawa mafisadi wa sanaa na kukaa nao meza moja na kujidanyanya eti mnatafuta vazi la taifa ambalo hakuna mtanzania atayelivaa ni bora uwageukie waache kula pesa za wasanii ili kutengeneza ajira kwa vijana.Angalia serikali kama za nchi za ulaya au marekani wako very serious when it comes to piracy kwa sababu wanajua hizi ni ajira kwa watu wengi.
  ukweli ni kwamba mchakato wa kutafuta vazi la taifa kwangu naona ni kupoteza muda na pesa za walipa kodi kwa sababu mpaka vazi lipatikane ni vikao vingapi vitakuwa vimefanyika na pesa ngapi itakuwa imepotea?jibu unalo...viongozi wetu ni vema kujua ni jambo gani lina uzito kuliko jingine...mimi mwenyewe nimewahoji watu wengi kuhusu hili vazi la taifa hakuna hata mmoja aliyesema atakuwa radhi kulivaa hizo vazi la taifa na kwa taarifa tu vazi la laifa huja naturally and automatically sidhani kama wamasai walikaa kikao kutafuta vazi la lubega kama hatukuwa na vazi miaka ya 60 tutakuwa nalo leo?....na vile vile kumbuka hili vazi linatafutwa kipindi cha kizazi cha .com.
  mzee nchimbi unapoteza muda,jaribu kutatua matatizo magumu ambayo watanzania hawatakusahau kamwe,kwa mfano ukitatua hili la wasanii hawatakusahau kamwe kwenye maisha yao sawa sawa na kiongozi kwenye wizara ya nishati na madini akitatua la umeme watanzania hawatamsahau milele.ni hayo tu.
   
Loading...