Nchi zinazoendelea zinafurahi kuona China na Marekani zinaimarisha ushirikiano wao

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,008
1,028
Na Fadhili Mpunji

1637193365988.png


Katika muda mrefu miaka karibu mitano sasa, mawasiliano kati ya China na Marekani yamekuwa katika hali ambayo wachambuzi wengi wameiita si ya kawaida. Tangu Rais Donald Trump alipozusha mvutano usio na maana na China, mawasiliano ya kidiplomasia na hata uhusiano wa kiuchumi kati ya pande hizo mbili ulitetereka. Mawasiliano kwa njia ya video kati ya Rais Xi Jinping na Rais Joe Biden yanaleta matumaini kuwa busara imeanza kurudi kwenye mahusiano ya kidiplomasia kati ya China na Marekani.

Ukweli ni kuwa China na Marekani kwa sasa ni mihimili muhimu ya uchumi wa dunia. Nchi hizi mbili zinaposhirikiana vizuri, kuna manufaa makubwa kwa maendeleo ya dunia, na kama hazina ushirikiano kuna kuwa na changamoto mbalimbali, sio tu kati ya pande hizo mbili, bali pia kwa pande nyingine.

Hivi karibuni kwenye mkutano wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika mjini Glasgow, kulikuwa na faraja kubwa baada ya China na Marekani kuwa na sauti moja kuhusu jambo hilo na kuahidi kushirikiana. Ni kweli tofauti ndogo ndogo bado zipo, lakini dunia nzima imefurahi kuona nchi hizi mbili kubwa zimekuwa kuangalia maslahi mapana ya dunia nzima.

Saa chache kabla marais Xi Jinping na Joe Biden kuongea kufanya mazungumzo kwa njia ya video, baadhi ya vyombo vya habari vilitabiri kuwa yatakuwa ni mazungumzo mafupi, makali na yaliyojaa mivutano. Hasa ikikumbukukwa kuwa mkutano kati ya China na Marekani uliofanyika mwezi Machi huko Alaska uliisha katika mazingira ya kutoelewana, wengi walidhani mkutano kwa njia ya video kati ya Rais Xi na Rais Biden utakuwa hivyo. Lakini kilichotokea ni kuwa mazungumzo hayo yaliyokuwa yamepangwa kufanyika kwa muda wa saa mbili yalifanyika kwa karibu saa nne, katika mazingira ya kirafiki, usawa, uwazi na kuheshimiana.

Hatuwezi kuepuka ukweli kuwa China na Marekani ni washindani na kuna wakati zinakuwa na migongano ya hapa na pale, lakini Rais Joe Biden alisema wazi kubwa hapendi kuona ushindani na migongano kati ya Marekani na China inabadilika kuwa mapambano, iwe ni kwa kukusudia au kwa bahati mbaya. Ni kweli kuwa Marekani haifurahi kuona China inakaribia kuchukua nafasi yake kiuchumi na kutaka ya kwanza duniani. Hili ni jambo linaloeleweka, mara nyingi ni kuwa mtu aliyezoea kuwa juu, siku zote anakuwa na hofu anapoona kuna wengine wanataka kumpita.

Rais Xi Jinping pia alikuwa muwazi kwa Rais Joe Biden na kusema China haifurahii kitendo cha Marekani kuingilia mambo yake ya ndani kwa visingizio mbalimbali kama vile suala la haki za binadamu na demokrasia, au uingiliaji kwenye suala la Taiwan, ambalo China imesema wazi kuwa kujaribu kuwaunga mkono watu wanaotaka kuitenga Taiwan kutoka China ni sawa na kucheza na moto. Bila shaka migongano kama hii haiwezi kuondolewa kwa urahisi au kwa siku moja. Lakini ukweli kwamba kitendo cha pande mbili kufanya mazungumzo kwa zaidi ya saa nne, ni mafanikio makubwa ya kidiplomasia na ni mwelekeo mzuri. Karibu mambo yote makubwa yanayotatiza uhusiano kati ya nchi hizo mbili yalijadiliwa, lakini pia mambo makubwa yanayohusu dunia kama vile mabadiliko ya tabia nchi, mapambano dhidi ya janga la COVID-19,

Rais Xi Jinping alitaja kuwa China na Marekani ni sawa na meli mbili kubwa zinazosafiri baharini. Bahari kubwa inatoa fursa kwa meli kubwa kusafiri bila kugongana, kama meli hizo zitagongana basi hiyo itakuwa ni sababu ya kukosa mawasiliano kati ya manahodha.
 
Back
Top Bottom