Nchi zinazoendelea, chama tawala na uhusiano wa sheria za nchi

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Jul 17, 2019
322
645
NCHI ZINAZOENDELEA, CHAMA TAWALA NA UHUSIANO WA SHERIA ZA NCHI.

Na Elius Ndabila
0768239284

Kuna uhusiano wa karibu sana kati ya Chama kinachotawala na sheria zinazoongoza Taifa. Katika nchi zinazoendelea kuna uhusiano mkubwa wa Sheria za nchi na msimamo wa chama Tawala.

Ninatoa tafsiri hii baada ya wiki jana Mhe Polepole kuwanyoshea kidole TCRA na Juzi mzee Balozi Khamis Kagasheki kutoa mtazamo wake wa natural justice(Right to be heard).

Kosa kubwa ambalo nchi zinazoendelea, hususani viongozi wake hujisahau ni kuwa Sheria wanazotunga au kuzisimamia haziwahusu wao. Wanasahau kuna wakati watakuwa Raia wa kawaida Sheria hizi hizi zitawashughulikia au ndugu zao watashughulikiwa na Sheria hizo.

Kwa nini nimesema Vyama tawala kwenye nchi zinazoendelea zinauhusiano Mkubwa na Sheria za nchi? Sababu ni kuwa kinapoitwa Chama tawala maana yake ndicho chenye serikali na ndicho Kwa kiasi kikubwa kinakuwa na Wabunge wengi wanaotunga Sheria. Hata zile subsidiary law zinatokana utawala huo huo. Hakuna Sheria inaweza kupitishwa na bunge au mamlaka zingine zenye wajibu wa kutunga Sheria kama Chama kinachitawala kinaona hiyo sheria haina masilahi Kwa nchi. Haiwezekani!

Kinyume na hapo Chama tawala kupitia Party Kokasi au namna nyingine watazuia hiyo Sheria isitungwe.

Ukweli ni kuwa Sheria ambazo Leo Mhe Polepole anasema ni mbaya na anasema tunasafari ndefu ya kuusema ukweli, Yeye mwenyewe Kwa karibu miaka mitano alishiriki kuithibitisha. Akiwa Katibu Halmashauri Kuu Itikadi na Uenezi alikuwa na fursa ya kuona Sheria zote zinazotungwa na kushauri.

Sheria zinazotumika sasa na ambazo hata TCRA wanazisimamia nyingi zimepitishwa mwaka 2019 Mhe Polepole akiwa mwenezi. Bahati mbaya huenda kipindi hicho alijua hizo Sheria ni zetu yeye hazimhusu.

Hata zile Sheria za CHAMA ambazo leo anatangaza kuwa niliitwa, akiwa mwenezi na viongozi wengine walizihuisha Kwa kiasi kikubwa kanuni, sera na Sheria za CCM. Kama umebahatika kusoma sheria za maadili za CCM ambazo Mhe Polepole alishiriki kuziandika, ijapo huenda Kwa kipindi hicho alidhani zinatuhusu watia nia TU ni kali sana.

Hivyo ni mhimu tunapokuwa na nafasi tukumbuke kufanya mambo ambayo kesho hayatatuumiza au kuumiza ndugu zetu.

Ninaamini Mhe Polepole angejua kuna siku Sheria ya TCRA itamkwangua, basi mwaka 2019 wakati inajadiliwa angewashauri Wabunge wa CCM Kwa uwingi wao waachane nayo Kwa kuwa uhusiano wa Sheria na chama tawala ni sawa na Pande mbili za shilingi. Upande mmoja unapokosekana basi hiyo ni pesa feki.
 
Pole yake alimtumainia mungumtu badala Mungu alie hai....we mbinguni
 
Back
Top Bottom