Nchi zilizotawaliwa na mfaransa zipinduliwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nchi zilizotawaliwa na mfaransa zipinduliwe

Discussion in 'International Forum' started by Netanyahu, Sep 6, 2009.

 1. Netanyahu

  Netanyahu Senior Member

  #1
  Sep 6, 2009
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 148
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  NCHI ZILIZOTAWALIWA NA MFARANSA ZIPINDULIWE

  Hivi mkoloni wa kifaransa alikuwa na matatizo gani.Nchi alizotawala mfaransa zinazoongea kifaransa zimejaa mapinduzi na migogoro ya kivita isiyoisha.Anzia Afrika mashariki viinchi kama Rwanda na Burundi fujo tupu ukienda Afrika ya kati nchi zote ziongeazo kifaransa vita tupu,nenda Afrika magharibi ubabe tu wa kivita na mapinduzi ya kivita,Ukienda Afrika kaskazini nchi zinazoongea kifaranza zimejaa historia ya kupinduana tu.Ukienda baharini kwenye visiwa vinavyorumia kifaransa si komoro,shelisheli wala Madagascar n.k ni balaa tupu hadi ma DJ wa miziki akina Ravolomanana wanasumbua.Je wafaransa hawana au hawakuwa na uwezo wa ku-groom viongozi bora wa kutawala nchi walizotawala au ni nini?
  Kiasilimia ni kuwa asilimia tisini ya vita na mapinduzi ya nchi Africa iko katika nchi ziongeazo kifaransa,

  Wataalamu wa fani za kivita na historia na wengine tusaidiene hivi nini kifanyike kuleta utulivu katika nchi hizi zilizotawaliwa na mfaransa ambazo ndizo zinalitia aibu bara la Africa lionekana la wahuni kwa asilimia kubwa.Niko katika utafiti wa kijeshi kama mpiganaji wa porini nisiye na kombati wala cheo kujua nini kifanyike kwa sisi wapigaji wa misituni ili utulivu urejee Africa kwenye hizo nchi.

  Rwanda iliamua kupindua na kuifanya Rwanda iwe English speaking Country kujitoa kwenye matatizo ya kifaransa. Labda iko haja ya vijana na wazee watokao nchi hizo waliokulia katika nchi zizungumzazo kiingereza au Kiswahili waige mfano wa Kagame wakapindue hizo nchi na wageuze ziwe English speaking country au Swahili speaking countries.Maana inaelekea Swahili na English speakers groomed leaders wanaweza kuziwezesha kuwa na utulivu na amani za muda mrefu.

  Mimi kama mpiganaji nilikuwa nafikiri dawa na kuzipindua tawala za wazungumza kifaransa waliokulia kifaransa faransa wawekwe wengine toka nchi hizo waliokulia na kulelewa kingereza ngereza au kiswahi Swahili washike watawale .Waheshimiwa wadau mnasemaje maana hatuwezi kuendelea na aibu hii milele lazima ufumbuzi upatikane.

  Mfaransa inaelekea ni mtanashati tu tu lakini kashindwa kutoa watawala wazuri kupitia education system na political system yake iko haja apinduliwe afungashwe virago Africa tuwe na Afrika iliyojaa amani.
   
 2. M

  Mkandara Verified User

  #2
  Sep 6, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu hujaelewa hadi leo kuwa kuna kitu kinaitwa Ukoloni Mamboleo ktk kufanya kazi!
  Nchi zote za kifaransa na nchi nyinginezo zimeundiwa maadui wao kisiasa yaani rebels na serikali zinazongumza kiingereza ndio wako nyuma ya kila matukio. Sudan vita yao imeundwa (sababu ni Mafuta) Rais wa Sudan alipotangaza kuwapa contract ya Mafuta China..
  Marekani akaunda uadui kwa kuunda jeshi Darfur against serikali... leo hii Sudan imerudisha mkataba Marekani unasikia kuwa wale ma rebel waliokuwa wakipewa support ndio wao wanateka magari ya wafanyakazi wa UN na kuua watu..Jamaa waliingizwa Mkenge na mzee Bush kama walivyofanyiwa Wairaq wa Basra (Shia) na Marekani mwaka 1992.
  Kila jeshi la Upinzani Afrika ni mbegu ya mzungu yaani wanapewa support na nchi za magharibi.. Watazungumzia Demokrasia lakini nchi kama Egypt na Gabon hazitaguswa hata kama utawala wake ni mbovu kiasi gani..Mkuu Afrika now is for grab mwenye wanasema Sadakallahu sadakallahu - Mwenye kupata na apate! mwenye kukosa na akose kisha kifurushi kinarushwa juu hewani!
   
 3. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #3
  Sep 6, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Tena orodha yake ni ndefu ukiongeza na zilizotawaliwa na Belgium. Belgium ni wafaransa vile vile hata lugha wanatumia kifaransa. Ni kweli kwamba nchi hizo zipo ktk hali mbaya sana kama DRC, Mali, Mauritania, Gabon, Senegal, Benin, Guinea etc
   
 4. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #4
  Sep 6, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mkuu Nemesis,
  Usiwe mtu wa kusikiliza tu habari na KUMEZA bila kutafuna. Ona sasa unavyojionyesha kuwa wewe ni MWEUPE. Hizo nchi nimeziwekea BOLD ni kwamba ZINATUPITA KIUCHUMI. Mali wametupita kidogo ila Mauritania na Senegal wametuzidi mara mbili katika GDP (Nominal).

  Sisi tupo kapu moja na akina Rwanda na Burundi ingawa wenzetu vita iliwarudisha nyuma sana na sisi tumekalia kuwachagua MAFISADI ili waendeshe vita na pesa zetu. Wanaziuwa kama wale waarabu wakija Loliondo.
  Tanzania tunafikiri sisi ni BAAB Kubwa tukiwa Dar ila ukweli sisi ni WEUPEE.
   
 5. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #5
  Sep 6, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Acha chuki binafsi dhidi yangu, wewe ndo mweupe. Mtoa hoja hajaeleza masuala ya GDP, ameeleza juu ya political unrest. Hizo nchi ulizobold hazijatulia kiusalama na masuala ya kisiasa. Uwe unasoma na kuzingatia hoja kabla ya kuandika.
   
 6. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #6
  Sep 6, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Hii analysis inapwaya.

  1. Muandishi hajaweza kutambua tofauti ya Ubelgiji na Ufaransa.Hata hao waliokuja kumuunga mkono kwamba wabelgiji ni wafaransa kwa sababu wanaongea kifaransa wamekosea kwa sababu moja si kila anayeongea kifaransa ni mfaransa, kama vile si kila anayeongea kiingereza ni muingereza, lakini zaidi ya hapo ukiifuatia historia ya Ubelgiji utagundua Ubelgiji imekuwa Ubelgiji kwa sababu ya Napoleon kushindwa katika battle of Waterloo, Sunday 18 June 1815.Ubelgiji mpaka leo kuna upande wanaongea Kifaransa na upande mwingine wanaongea Flemish, kwa hiyo si kweli hata kusema kwamba Ubelgiji wanaongea Kifaransa.

  2.Kusema nchi zilizotawaliwa na Mfaransa zina matatizo ya mapinduzi si sahihi, kwanza tushaona kwamba nchi zilizokuwa cited Rwanda na Burundi hazikuwa chini ya Mfaransa bali Mbelgiji kama sehemu ya mkataba wa makoloni uliokuja baada ya Ujerumani kushindwa vita vya kwanza vya dunia na kunyang'anywa makoloni yake.

  Kuna nchi zilizotawaliwa na mfaransa zimekuwa stable kutoka uhuru mpaka leo.Mfano ni Senegal, hakujakuwa na mapinduzi kutoka Leopold Senghor, Abdou Diouf mpaka leo Abdoulaye Wade.

  At the same time kuna nchi za Anglophone Africa kama Uganda, Nigeria na Ghana ambazo zina historia ya unstable governments na coup d'etats.

  Granted objectives za Wafaransa katika ukoloni zilikuwa tofauti sana na za Waingereza, l wafaransa walikuwa wanataka kuweka mizizi hasa Afrika na hata kuwachukulia wakazi wa makoloni yao Afrika kama raia wa Ufaransa walio Afrika -Senghor was a legislator in Paris before the Senegalese independence-labda huku ndiko unakoelekea.Bottom line wakoloni wote wali destabilize Africa, na hii habari ya kusema waliotawaliwa na Wafaransa walikuwa hivi na sisi Anglophone ni hivi, at least in the contest provided here, ni illusion tu.
   
 7. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #7
  Sep 6, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kaka pia kuna hii nchi ndogo tu kule pembe ya Afrika, inaitwa Djibouti (wenyewe wasonjo wanatamka Jabuuti), hii nchi ilitawaliwa na Wafaransa na mpaka leo wanazungumza Kifaransa na kiarabu, hizi ndio lugha kuu za mawasiliano. Hii nchi ilipata uhuru mwaka 77 tarehe 27 June...!
   
 8. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #8
  Sep 7, 2009
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,758
  Trophy Points: 280

  Bob,

  sasa na wewe umeanza propaganda za wanasiasa wetu wa Africa. Hivi kweli matatizo ya Sudan yameanza na Darfur? Iam sure you know better ila unajaribu kuspin..kusudi wazungu walaumiwe kwa kila kitu.

  Sudan imekuwa kwenye mgogoro since independence mwaka 1956. Unaujua ule mgogoro wa kusini? ule mgogoro umeua watu wengi sana. Darfur unaijua kwa sababu imewekwa kwenye CNN...na akina Bono..wanafanya fundrising za Darfur.....It is estimated watu zaidi ya million tano walikufa kule kusini na mpaka leo wanazidi kufa...what has mzungu got to do with that???... Au kwa vile mgogoro haukuchukua headlines za CNN na BBC? ndo watu hatuuelewi? Tatizo la Sudan has nothing to do na wazungu ni ujinga wa BASHIR na waliomtangulia akina Mahdi, Nimeir nk. Hivi kweli mzungu yuko responsible kuwasilimisha watu wa kusini wote wawe waislamu? How do you force people to be Arabs??..kuna jamaa alishasema humu..when the only available thing is injustice..the only wise thing to do is resistance (not sure of proper quote)..

  Well, what I can say is: WAAFRIKA TUFIKE MAHALA..TUACHE SPINNING. Ujinga tunafanya sisi..harafu hapa eti tunasingizia mafuta na wachina! Mafuta yamegunduliwa, tena Southern Sudan, 1970s..wakati China bado anahangaika kama sisi..Afrika hajaijua.Leo..Baradhuli Bashir anaua watu wake..tunasema eti wazungu wamenyimwa mafuta! Unajua Chevron alikuwa Sudan tangu lini??? miaka ya 70...walikuwa wanafanya exploration ya hayo mafuta.... na waliamua kuondoka wala hawakufukuzwa kwa sababu ya siasa.......Anyhow, BOB, NAJUA wewe ni kichwa..labda umepitiwa..ila hizi generalization si sahihi. Tatizo la Africa ni sisi wenyewe. Huwezi kulazimisha wanachi wote wavae kanzu waende msikitini...wananchi wakose kuresist...

  Kuhusu swala la mtoa mada, nadhani hajakosea...kila sehemu France alikopita kuna instability na political unrest. Haina maana kwamba in Anglophone we are better..ila wafaransa wamezidi. Mpaka leo..CHAD, CONGO, Ivory Cost, Togo, MAURITANIA, Niger nk..wanahangaika. Na bado France ana support rebels na government. Mfano mzuri ni Chad....Ufaransa wanamsaidia Derby na wakati huo huo wanawasaidia waasi wa Derby.

  In all, I will be the last person to blame the west on the tragedy in Darfur and Sudan in general. Ni huu ujinga wakina Turabi na Bashir wa kutaka watu wote wawe waislamu against all basic norms of decorum of humanity.

  Unajua Sudan kuna msemo unasema hivi: A slave is a slave..no matter how long his/her tunic is. Ikimaanisha kwamba mtu mweusi ni mweusi tuu hata kama angevaa kanzu yenye urefu wa aina gani. Na kumbuka kwa sababu ya historia..mweusi alikuwa (mpaka leo) anaonekana na kuchukuliwa kama mtumwa)..ndo vitu kama hivyo vina-fuel instability..kuwaona raia wenzako kama second class citizens. kWA SABABU HATA KAMA MWEUSI AKIWA MUISLAM bado anadharaurika.....Maana siyo "mwaarabu" and you wonder uarabu wa msudani uko wapi (maana na yeye akienda Saudia anadharauriwa kama kiazi...) Hakika waafrika ndivyo tulivyo...

  Ya Darfur ni mengine..yanahitaji thread yake.

  Masanja
   
  Last edited: Sep 7, 2009
 9. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #9
  Sep 7, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Hapa kaka punguza jazba kidogo... Hivi hao wazungu wameanza kuwagombanisha waafrika 1956?
  Hao Wasudani na Historia yao sidhani hata kama unaifahamu vema, hapa nahisi kama mambo ya kijiweni tu... Eti wanawalazimisha kuvaa kanzu... lol ili iweje sasa? Na huo msemo wa kuwa "A slave is a slave..no matter how long his/her tunic is." sidhani hata kama unapatikana uko... Maana hata uko kaskazini kwenye serikali kuu kuna viongozi weusi wa kisudani.

  Tujaribu kuwa wakweli ngaa kidogo.
   
 10. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #10
  Sep 7, 2009
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,758
  Trophy Points: 280
  Kazi kweli kweli! Kweli wewe ni X-Paster

  Sasa wewe historia unayoifahamu kwanini usiiweke hapa? everything ni nadhani..duh!..Iam sure ungeijua Sudan (in a social, economic and political context) hata robo ya ninavyoifahamu..usingeandika haya uliyoyaandika...BASED ON YOUR POST HERE.

  Bro, next time get your facts correctly
   
 11. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #11
  Sep 7, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Sawa Masanja, nasikia uliwahi ishi maeneo ya Omdurman Khartoum.
   
 12. A

  Alvin Member

  #12
  Sep 7, 2009
  Joined: Sep 7, 2009
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  unajua bwana mfaransa hana direction yeyote ile duniani wala hajiamini kabisa nimeona hata juzi huyu huyu alikua anapinga vita kumng'oa jamaa kule iraq baada ya vita kuisha anaanza kuhaha kuomba kazi ya ukandarasi aafadhali jamaa yeye ameamua kutawala kwa kupitia utawala mambo leo kipindi hiki
   
Loading...