Nchi zilizoendelea kama marekani, japan, n.k, huwa zinafanya maadhimisho kila mwaka?

jzm-teak

JF-Expert Member
Jun 23, 2013
1,770
319
WanaJF, ningependa kufahamu kama nchi zilizoendelea kama huadhimisha sikukuu kama zetu kila mwaka.
Pia pamewahi kutafutwa tathimini ya faida au hasara ya kufanya hizi sherehe kila mwaka?
Mimi naona sherehe kama hizi tufanye baada ya miaka mitanomitano ili pesa inayotumika tununue madawa na madawati ya shule.
 
Tanzania ina sikukuu za kitaifa (ambazo wafanyakazi hupumzika) 17, Uingereza inazo 8!
 
Maadhimisho kawaida kimya kimya ikulu. Maskini ndio tunayo tabia ya kufuja hela kwenye visherehe sherehe.
 
Tanzania ina sikukuu za kitaifa (ambazo wafanyakazi hupumzika) 17, Uingereza inazo 8!

nimekupata mkuu, ila najua kuna siku za mapumziko bila gharama za maadhimisho, hizi za gharama ya mojakwa moja ndo nauliza nchi zilizoendelea hufanya kila mwaka?
 
nimekupata mkuu, ila najua kuna siku za mapumziko bila gharama za maadhimisho, hizi za gharama ya mojakwa moja ndo nauliza nchi zilizoendelea hufanya kila mwaka?

Ni kweli kaka, kuhusu gharama sina uhakika. Lkn hata kitendo cha wafanyakazi nchi nzima kukaa majumbani siku 17 lina athari ktk uzalishaji. Mfano, nikwanini tuwe na siku ya Nyerere, Karume na ya mashujaa? Hizi ilitakiwa iwe moja tena watu waende maofisini. Hata nane nane na sabasaba ingekuwa moja, bidhaa za kilimo na za viwandani kwa pamoja, alafu wafanyakazi wasioshiriki moja kwa moja wanaenda makazini angalau nusu siku.
 
Back
Top Bottom