Nchi zaidi za Afrika zaunga mkono uamuzi wa China kuhusu Hong Kong

CRI Swahili

Member
Dec 21, 2013
19
42
Mkutano wa tatu wa Bunge la 13 la Umma la China hivi karibuni umepitisha Muswada wa Kujenga na Kukamilisha Mfumo wa Sheria wa Kulinda Usalama wa Taifa Katika Mkoa wenye Utawala Maalumu wa Hong Kong na Utekelezaji wa Mfumo huo. Nchi za Afrika zimeunga mkono hatua hiyo, zikisema ni hatua imara iliyopigiwa na China katika kutunga sheria ya usalama wa taifa mkoani Hong Kong, na itatoa uhakikisho kwa ustawi na utulivu wa muda mrefu wa mkoa huo.

Serikali ya Tanzania imesema inafuatilia kwa karibu suala la Hong Kong, na msimamo wake kuhusu suala hilo ni kama zamani, yaani kuunga mkono sera ya "Nchi Moja, Mifumo Miwili". Nchi hiyo inaona kuwa, utekelezaji wa sheria ya usalama wa taifa si kama tu utamaliza ukosefu wa sheria hiyo katika mkoa wa Hong Kong, bali pia utasaidia sehemu hiyo kurejesha utaratibu wa kawaida.

Katibu mkuu wa Chama tawala cha Kenya Jubilee Raphael Tuju amesema, Hong Kong ni sehemu ya China, na kuingilia kati suala la sehemu hiyo ni kama kuingilia kati mambo ya ndani ya China, kitendo ambacho kinakiuka Makubaliano ya Kimataifa ya Vienna.

Serikali ya Burundi imetoa taarifa kuhusu sheria hiyo ya China, ikisema inaunga mkono Bunge la Umma la China kupitisha uamuzi kuhusu sheria hiyo, ambayo itakuwa na ufanisi wa kulinda usalama wa taifa katika sehemu ya Hong Kong. Taarifa hiyo pia imesisitiza kuwa Burundi inapinga nguvu yoyote ya nje kuingilia kati mambo ya ndani ya China.

Serikali ya Uganda imesema Hong Kong ni sehemu isiyotengeka ya China, na suala la sehemu hiyo ni mambo ya ndani ya China. Uganda inafuata sera ya kuwepo kwa China moja duniani, na kuunga mkono kwa nguvu zote China kuzuia ufarakanishaji, na kulinda ustawi na utulivu wa Hong Kong, na kwamba hila ya nchi za Magharibi ya kufarakanisha China haitafanikiwa.

Msomi maarufu nchini Nigeria Arad Fowler kwenye Gazeti la The Nation la nchi hiyo ametoa makala akifichua unafiki wa nchi za Magharibi, na kusema usalama wa taifa ni suala kuu zaidi, na sheria ya usalama wa taifa iliyopitishwa na Bunge la Umma la China itaokoa Hong Kong.

Spika wa bunge la Mali Moussa Timbiné amesema, suala la Hongkong ni mambo ya ndani ya China, na nchi nyingine hazina haki ya kuingilia kati suala hilo. Amesisitiza kuwa Mali inaunga mkono kithabiti China kulinda mamalaka na ukamilifu wa ardhi zake, na kutekeleza sera ya "Nchi moja, Mifumo miwili.
Screenshot_20200604-210903~2.png
Screenshot_20200604-210903~3.png
Screenshot_20200604-210903~4.png
 
Mpaka dunia iishe ndio bin adamu ataacha kupigania uhuru.
 
Naunga mkono sheria hiyo kupitishwa pia. Marekani na washirika wake wanafurukuta kwa kila namna kuyumbisha China ili kusiwe na wa kuwakemea.

Mafanikio ya China ni mafanikio ya dunia kwa ujumla, kinyume chake mafanikio ya mabeberu ni umasikini mbaya kabisa kwa mataifa yanayoendelea
 
Ushawishi na kuogopewa kwa US duniani kunazidi kusambaratika

TURAMPET miongoni mwamarais wahovyo kabisa kuwahi kumshuhudia akiitawala US ila safi sana hiii kongole ijapokua mataifa mengi ya AFRIKA yameikubali hii sheria kwamaslahi yawanasiasa zaidi kuliko wananchi wao ila KONGOLE sana kwa UCHINA
 
Waafrika hawataishiwa na kasumba ya utumwa, leo hii hata mchina awakojolee usoni bado tu watamsujudia.

Wachina hawaamini kama waafrika ni binadamu kamili. Majuzi tu kuna kijana raia wa Zambia aliuliwa China lkn hakuna aliyeguna...!!!

Waafrika kuna kosa fulani tulilomkosea Mungu lkn hataki kutusamehe. Afrika ni bara linalofahamika kwa mambo mabaya tu duniani tofauti kabisa na mabara mengine. Sijui tuna nini cha maana cha kujivunia.
 
Waafrika hawataishiwa na kasumba ya utumwa, leo hii hata mchina awakojolee usoni bado tu watamsujudia.

Wachina hawaamini kama waafrika ni binadamu kamili. Majuzi tu kuna kijana raia wa Zambia aliuliwa China lkn hakuna aliyeguna...!!!

Waafrika kuna kosa fulani tulilomkosea Mungu lkn hataki kutusamehe. Afrika ni bara linalofahamika kwa mambo mabaya tu duniani tofauti kabisa na mabara mengine. Sijui tuna nini cha maana cha kujivunia.
tatizo lenu mnasumbuliwa na unafiq na choyo Africa wakiungana na UCHINA maneno mnayamaliza wakiungana na WAZUNGU mnakaa kimya

Siasa naubaguzi wakipumbavu(SIO TUSI) ndio unatupelekesha pelekesha tu

Kwahio ulitaka waafrika wafanye kipi ?!
 
Waafrica wanapaswa waangalie "what is right" na si "who is right"
hakika MKUU ila wanaongozwa kinafiq nasijui wanaangalia nini hasa

Kiufupi wanapelekeshwa pelekeshwa nayote kwakuangalia maslahi ya Wachache kwakupata sapoti

Kama sasa wengi wanamuunga mkono sababu anatoa pesa namambo mengine ambayo baadae huenda yakayagharimu mataifa husika

Wanatakiwa waangalia kilicho sahihi kiwe cha MCHINA ama YEYOTE namwisho kabisa wanatakiwa wawe nasauti moja kwakila jambo kwamaslahi ya AFRIKA wasiwe wanafiq kama walivyomfanyia GADAFI akauliwa kama PANYA
 
Back
Top Bottom