figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,485
Zaidi ya nchi 140 barani Afrika waiomba serikali ya Tanzania kuangalia upya tozo za kodi zinazotozwa kwa watalii waingiapo nchini.
============
Zaidi ya nchi 140 za bara la Afrika na Bara la ulaya zaiomba serikali ya Tanzania kuangalia upya tozo ya kodi zinazotozwa kwa watalii waingia nchini.
Mawakala wa makampuni ya utalii katika nchi za Jumuiya ya afrika Mashariki wameiomba serikali ya tanzania kuangalia upya tozo ya kodi zinazotozwa watalii wanapoingia hapa nchini kutokana na watalii wengi wanaotoka nje ya nchi kwa kutumia usafiri wa ndege kushukua nchini kenya.
Wakizungumza wakati wa uzinduzi wa maonyesho ya siku tatu ya utalii ambayo yamehudhuriwa na nchi zaidi ya 140 kutoka katika bara la Afrika na Bara la ulaya, mawakala hao wanasema watalii wanaokuja Tanzania wanalazimika kushukia nchini Kenya na baadae kuja Tanzania kwa ajili ya kutembelea vivutio vya utalii.
Wamesema fedha zinazopotea kutokana na watalii hao kushukia nchi Kenya ni nyingi na kwamba kuna haja ya serikali ya Tanzania kutangaza vizuri vivutio vya utalii vilivyopo hapa nchi ili watalii wanaotoka nje ya nje washukie Tanzania badala ya kushukuia nchini Kenya kwa kuwa mapato yanayopotea ni mengi.
Kwa upande wake Waziri wa Maliasili na Utalii Mh.Jumanne Maghembe amesema idadi ya watalii wanaoingia hapa nchini imepungua na kwamba Tanzania inafanya jitihada za kuimarisha sekta ya utalii ili kuweza kuvutia watalii wengi kutoka nje ya nchi kupenda kuja nchini.
Naye Mkurugenzi wa kampuni ya uandaaji wa maonyesho hayo ya utalii kutoka nchi za Afrika na Bara la ulaya amesema tangu kuanzishwa kwa maonyesho hayo mwaka jano kumeleta mafanikio makubwa kwa wadau wa utalii hapa nchini.
Chanzo: ITV