Nchi za Ulaya, Marekani na asia ziliendelea kiuchumi na kiteknolojia kutokana na kuwafuta kwenye mfumo wapinga maendeleo aina ya Zitto Kabwe

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,866
5,742
Imeelezwa na mojawapo ya Magazeti makubwa duniani la Financial Times kwamba, mbunge wa Kigoma mjini Mhe. Zitto Kabwe, ameiandikia Benki kuu ya dunia barua ya siri, ambayo pamoja na mambo mengine anaiomba Benki hiyo kutoipa Tanzania mkopo wa dola milioni 500 kwa ajili ya kuboresha Elimu nchini, huku miongoni mwa sababu alizozitoa ni pamoja na kuitaka Tanzania iruhusu wanafunzi wa kike wanaopata ujauzito kuruhusiwa kuendelea na masomo.

Huyu ndiye mbunge na kiongozi wa Chama cha siasa chenye matarajio ya kushika dola anayeamini kwamba, anaikomoa serikali kwa kuomba nchi inyimwe mkopo wa kuboresha elimu, kumbe anawakomoa watanzania masikini wakiwemo wa jimbo lake la Kigoma mjini.

Tarehe 11 November, 2018 niliwahi kuandika kuhusu dhambi ya usaliti kwa nchi pamoja na umuhimu wa kuwa na sheria inayowadhibiti watu wanaokiuka viapo vyao vya utii na uaminifu kwa nchi baada ya kuapa. Hii ni kwa sababu, sasa yamekuwa mazoea kwa mtu hususani kiongozi kuapa kuwa mwaminifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na baada ya kiapo, anafanya mambo kinyume na kiapo chake na hakuna hatua zinazochukuliwa dhidi yake.

Kwa mfano kiapo cha Uaminifu anachoapa mbunge mbele ya Spika Bungeni, kinasema:-
Nanukuu:- Mimi nathibitisha kwamba, nitakuwa mwaminifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuitumikia kwa moyo wangu wote, na kwamba, nitahifadhi, nitailinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa mujibu wa sheria iliyowekwa, Ewe Mwenyezi Mungu nisaidie Mwisho wa kunukuu.

Kwa kiongozi wa umma akiwemo mbunge anayeapa kiapo hiki, halafu baada ya kiapo anathubutu kuiandikia barua Benki ya dunia kuiombea nchi yake mabaya ikiwa ni pamoja na kunyimwa misaada kama alivyofanya Tundu Lissu au kuomba nchi inyimwe mkopo kama alivyofanya Zitto Kabwe.

kwa tafsiri nyepesi, maana yake ni kwamba, amekiuka kiapo cha kuwa mtiifu na mwaminifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kama kungekuwa na sheria inayowajibisha watu wanaokiuka viapo vyao baada ya kuapa, huyu Zitto Kabwe alipaswa kushughulikiwa ikiwemo kuvuliwa ubunge. Hakuna namna yoyote ya kuweza kumbadilisha tabia mhalifu aliyoizoea kuvunja sheria bila kumshurutisha kupitia sheria nyingine.

Tunaposhuhudia maendeleo ya kiuchumi na teknolojia katika nchi za Ulaya, Marekani pamoja na Asia, si kwamba, wapinga maendeleo aina ya Zitto Kabwe hawakuwepo, bali walikuwepo, isipokuwa kilichotumika ni kuwafuta kwenye mfumo kwa kuwaondolea nafasi za ushawishi katika jamii, na kwenye baadhi ya nchi mfano China na Korea, walitengenezewa sheria kali za kuwanyamazisha ikiwemo kupewa adhabu ya kifo kwa kupigwa risasi hadharani.

Swala la nchi kupiga hatua mbele za kiuchumi na kimaendeleo si jambo la lelemama wala si jambo la kuchekeana hata kidogo, bali ni vita, na siku zote vita huwa haina macho. Ndiyo maana kwenye kilimo cha jembe la kukokotwa na ng'ombe, wakati mwingine mkulima hulazimika kutumia mijeredi ili ng'ombe asiyetaka kwenda kwa hiyari aende kwa shuruti.

Taifa linapokuwa na wapinga maendeleo aina ya Zitto Kabwe pamoja na wengineo wanaojiita wanaharakati, dawa yake si kucheka na watu hao, kwa sababu kuwepo kwao katika taifa ni sawa na kuwepo kwa sumu katika mwili. Hatuwezi kuendesha nchi kwa mfumo wa kuchekeana na wapinga maendeleo.

Tumedhamiria nchi hii isonge mbele kwa haraka kwa kuwa tulichelewa, hivyo njia ya pekee kwa anayetaka kuikwamisha nchi isiendelee ni kumkwamisha yeye kwanza kabla nchi haijakwama.

Ni lazima tuwe na dola inayoogopwa na wahalifu, dola inayoogopwa na wahujumu uchumi, dola yenye kuogopwa na wapinga maendeleo, dola inayoogopwa na wasaliti, iwe ni kupinga maendeleo kwa wazi au kwa usiri. Tusiruhusu maslahi ya wengi kuangamizwa kwa kigezo cha kulinda maslahi ya wachache. Ni bora wachache waumie ili kuumia kwao kulete ukombozi wa wengi kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Umefika wakati ni lazima wananchi tuzungumze kwa lugha ya kikakamavu. Tumeteseka kiasi cha kutosha huku Zitto Kabwe na kundi lake wakinufaika kupitia kodi zetu, na bado pamoja na kunufaika huko, wanadiriki kuomba Benki ya dunia ituumize zaidi wakati tunayo serikali iliyodhamiria kututoa utumwani.

Hakika hili halikubaliki. Tunasubili kuona serikali itafanya nini kwa upande wake. Hatuwezi kuwa na wanasiasa wasioitakia nchi mema kwa kiwango hiki halafu kila uchao tunawalipa posho na kuwapigia makofi ili waonekane mashujaa katika nchi kwa maslahi ya mabwana zao.

Kama hatuna sheria inayowajibisha viongozi wanaokiuka kiapo chao cha utii na uaminifu kwa nchi, serikali ipeleke muswada wa sheria hiyo bungeni kwa hati ya dharula ili kuwashughulikia wanaokiuka viapo vyao mara baada ya kuapa, ikiwemo kuvuliwa ubunge endapo aliyekiuka kiapo chake ni mbunge kama alivyo Zitto Kabwe.

Kwa upande wa Asasi za kiraia zinazopiga vita ustawi wa nchi huku zikiwa na hati za usajili zinazowaruhusu kuendesha shughuli zao kutoka serikalini, hizi nazo ziangaliwe upya. Hata kama si utamaduni wetu, lakini kwa kuwa tumeamua nchi iende, kwenye vita vya kiuchumi, kuna wakati utafika lazima wachache tuwatose ili chombo kifike salama na walio tayari kwa safari. Hakuna namna.

Taifa haliwezi kuwa na kiongozi (mbunge) aliyepelekwa Jeshini kufundishwa uzalendo, akaapa lakini bado akatoka ziro, kisha akaapa bungeni na bado tena akatoka ziro. Si bure, ni kumfuta tu kwenye mfumo ili wapatikane walio tayari kukipeleka chombo na kukifikisha salama.

Kwa leo niishie hapo.

Kabla ya Lisu kupigwa risasi zilianza kauli za namna hii.

Hata Kama mtu kakosea bado capital punishment hairuhusiwi. Kuna Sheria na taratibu ashitakiwe Kama atakuwa na kosa atapewa adhabu kulingana na kosa lake.

Naanza kuwa na wasiwasi
 
Kwa hiyo na wewe unachukia watoto wanaojazwa mimba kuendelea kupata elimu ama?

Hawa wasichana wamekukosea nini kwa mfano?
 
Tatizo kubwa la Tanzania ni CCM mtu anafanya miradi apate sifa za kisiasa ila anaacha kutatua matatizo yale yanaoumiza wananchi kabisa

Tatizo la wanasiasa wa bongo wanatumia matatizo ya wananchi kama mtaji wao kisiasa wakiyamaliza hayo matatizo watahaidi nini wakati wa kampeni Bongo titaendelea kuwa masikini tu mpaka tukome

Hata mikataba ya madini wamesaini na wamefichaficha tu huko nakutoa maneno mazuri ila ukweli haujulikani kabisa
Maneno ya wanasiasa hayahaminiki kabisa hata yakiwa mazuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku watu wa aina yako wakianza kupungua nafikiri itakuwa ni ishara ya kwanza kuwa nchi yetu itakuwa imeanza kuendelea.
Binadamu anayefikiri ili aendelee anahitaji kuwamaliza wenye mawazo tofauti na yeye ana safari ndefu kuufikia ustaarabu na maendeleo yake
Imeelezwa na mojawapo ya Magazeti makubwa duniani la Financial Times kwamba, mbunge wa Kigoma mjini Mhe. Zitto Kabwe, ameiandikia Benki kuu ya dunia barua ya siri, ambayo pamoja na mambo mengine anaiomba Benki hiyo kutoipa Tanzania mkopo wa dola milioni 500 kwa ajili ya kuboresha Elimu nchini, huku miongoni mwa sababu alizozitoa ni pamoja na kuitaka Tanzania iruhusu wanafunzi wa kike wanaopata ujauzito kuruhusiwa kuendelea na masomo. Huyu ndiye mbunge na kiongozi wa Chama cha siasa chenye matarajio ya kushika dola anayeamini kwamba, anaikomoa serikali kwa kuomba nchi inyimwe mkopo wa kuboresha elimu, kumbe anawakomoa watanzania masikini wakiwemo wa jimbo lake la Kigoma mjini.

Tarehe 11 November, 2018 niliwahi kuandika kuhusu dhambi ya usaliti kwa nchi pamoja na umuhimu wa kuwa na sheria inayowadhibiti watu wanaokiuka viapo vyao vya utii na uaminifu kwa nchi baada ya kuapa. Hii ni kwa sababu, sasa yamekuwa mazoea kwa mtu hususani kiongozi kuapa kuwa mwaminifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na baada ya kiapo, anafanya mambo kinyume na kiapo chake na hakuna hatua zinazochukuliwa dhidi yake.

Kwa mfano kiapo cha Uaminifu anachoapa mbunge mbele ya Spika Bungeni, kinasema:-
Nanukuu:- Mimi........ nathibitisha kwamba, nitakuwa mwaminifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuitumikia kwa moyo wangu wote, na kwamba, nitahifadhi, nitailinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa mujibu wa sheria iliyowekwa, Ewe Mwenyezi Mungu nisaidie Mwisho wa kunukuu.

Kwa kiongozi wa umma akiwemo mbunge anayeapa kiapo hiki, halafu baada ya kiapo anathubutu kuiandikia barua Benki ya dunia kuiombea nchi yake mabaya ikiwa ni pamoja na kunyimwa misaada kama alivyofanya Tundu Lissu au kuomba nchi inyimwe mkopo kama alivyofanya Zitto Kabwe, kwa tafsiri nyepesi, maana yake ni kwamba, amekiuka kiapo cha kuwa mtiifu na mwaminifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kama kungekuwa na sheria inayowajibisha watu wanaokiuka viapo vyao baada ya kuapa, huyu Zitto Kabwe alipaswa kushughulikiwa ikiwemo kuvuliwa ubunge. Hakuna namna yoyote ya kuweza kumbadilisha tabia mhalifu aliyoizoea kuvunja sheria bila kumshurutisha kupitia sheria nyingine.

Tunaposhuhudia maendeleo ya kiuchumi na teknolojia katika nchi za Ulaya, Marekani pamoja na Asia, si kwamba, wapinga maendeleo aina ya Zitto Kabwe hawakuwepo, bali walikuwepo, isipokuwa kilichotumika ni kuwafuta kwenye mfumo kwa kuwaondolea nafasi za ushawishi katika jamii, na kwenye baadhi ya nchi mfano China na Korea, walitengenezewa sheria kali za kuwanyamazisha ikiwemo kupewa adhabu ya kifo kwa kupigwa risasi hadharani.

Swala la nchi kupiga hatua mbele za kiuchumi na kimaendeleo si jambo la lelemama wala si jambo la kuchekeana hata kidogo, bali ni vita, na siku zote vita huwa haina macho. Ndiyo maana kwenye kilimo cha jembe la kukokotwa na ng'ombe, wakati mwingine mkulima hulazimika kutumia mijeredi ili ng'ombe asiyetaka kwenda kwa hiyari aende kwa shuruti. Taifa linapokuwa na wapinga maendeleo aina ya Zitto Kabwe pamoja na wengineo wanaojiita wanaharakati, dawa yake si kucheka na watu hao, kwa sababu kuwepo kwao katika taifa ni sawa na kuwepo kwa sumu katika mwili. Hatuwezi kuendesha nchi kwa mfumo wa kuchekeana na wapinga maendeleo.

Tumedhamiria nchi hii isonge mbele kwa haraka kwa kuwa tulichelewa, hivyo njia ya pekee kwa anayetaka kuikwamisha nchi isiendelee ni kumkwamisha yeye kwanza kabla nchi haijakwama.

Ni lazima tuwe na dola inayoogopwa na wahalifu, dola inayoogopwa na wahujumu uchumi, dola yenye kuogopwa na wapinga maendeleo, dola inayoogopwa na wasaliti, iwe ni kupinga maendeleo kwa wazi au kwa usiri. Tusiruhusu maslahi ya wengi kuangamizwa kwa kigezo cha kulinda maslahi ya wachache. Ni bora wachache waumie ili kuumia kwao kulete ukombozi wa wengi kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Umefika wakati ni lazima wananchi tuzungumze kwa lugha ya kikakamavu. Tumeteseka kiasi cha kutosha huku Zitto Kabwe na kundi lake wakinufaika kupitia kodi zetu, na bado pamoja na kunufaika huko, wanadiriki kuomba Benki ya dunia ituumize zaidi wakati tunayo serikali iliyodhamiria kututoa utumwani. Hakika hili halikubaliki. Tunasubili kuona serikali itafanya nini kwa upande wake. Hatuwezi kuwa na wanasiasa wasioitakia nchi mema kwa kiwango hiki halafu kila uchao tunawalipa posho na kuwapigia makofi ili waonekane mashujaa katika nchi kwa maslahi ya mabwana zao.

Kama hatuna sheria inayowajibisha viongozi wanaokiuka kiapo chao cha utii na uaminifu kwa nchi, serikali ipeleke muswada wa sheria hiyo bungeni kwa hati ya dharula ili kuwashughulikia wanaokiuka viapo vyao mara baada ya kuapa, ikiwemo kuvuliwa ubunge endapo aliyekiuka kiapo chake ni mbunge kama alivyo Zitto Kabwe.

Kwa upande wa Asasi za kiraia zinazopiga vita ustawi wa nchi huku zikiwa na hati za usajili zinazowaruhusu kuendesha shughuli zao kutoka serikalini, hizi nazo ziangaliwe upya. Hata kama si utamaduni wetu, lakini kwa kuwa tumeamua nchi iende, kwenye vita vya kiuchumi, kuna wakati utafika lazima wachache tuwatose ili chombo kifike salama na walio tayari kwa safari. Hakuna namna.

Taifa haliwezi kuwa na kiongozi (mbunge) aliyepelekwa Jeshini kufundishwa uzalendo, akaapa lakini bado akatoka ziro, kisha akaapa bungeni na bado tena akatoka ziro. Si bure, ni kumfuta tu kwenye mfumo ili wapatikane walio tayari kukipeleka chombo na kukifikisha salama.

Kwa leo niishie hapo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika nchi yeyote ile kuna watu aina ya Zitto, hata katika chama chochote cha siasa kuna watu kama wakina Nappe na Makamba . Hii hali huwezi kuiepuka
 
Bwashee huyo Zitto hana uwezo wa kuzuia mkopo!
Ni kweli kabisa. hata mimi ninaona kumpa uwezo eti wa kuzuia pesa za mikopo ya nchi ni uongo kabisa. mtu mmoja eti anashinikiza nchi ikose mikopo tunamsingizia. Ila haya mambo yameenda na yanaendelea na hatujui mwisho wake. In short tuna hali mbaya sana kidiplomasia na marekani na nchi za ulaya. na hili ni lazima tujue kuna gharama yake tutailipa soon.
 
Back
Top Bottom