Nchi za Magharibi na vyombo vya habari vinashindilia pamoja msumari kwenye mzozo wa Ukraine

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
微信图片_20220330094747.png

Hassan Zhou

Tangu kuzuka kwa mzozo wa Ukraine mwishoni mwa Februari, nchi za magharibi na vyombo vya habari vimeshirikiana kushindilia pamoja msumari na kujaribu kugeuza macho ya watu wanaotaka kujua chanzo cha mzozo huo, na pia kuzipaka matope baadhi ya nchi ambazo zinataka kufikiwa kwa amani.

Kwanza haipingiki kuwa NATO kuendelea kupanuka kuelekea Ulaya Mashariki ikiongozwa na Marekani kumevuruga amani na utulivu wa kanda hiyo, na ndio chanzo cha mzozo huu. Lakini, baada ya mzozo huo kubadilika kuwa operesheni ya kijeshi, nchi hizo ziliendelea kuchezea vita vya wakala na siasa chafu, zikijaribu kuizungusha Russia na hata kupindua serikali ya nchi hiyo (Biden hivi karibuni alitoa kauli kali huko Poland kuwa, "Mtu huyu (yaani Putin) hawezi kuendelea kuwa madarakani."

Baada ya ghasia kutokea baadaye, Ikulu ya White House ilieleza haraka kwamba Marekani haitafuti mabadiliko ya utawala nchini Russia), kwa hivyo vitendo vya nchi za magharibi vimefanya mzozo huo kushindwa kusimamishwa ndani ya muda mfupi.

Hivi karibuni, hata gazeti la New York Times limeshindwa kuvumilia unafiki wa nchi za magharibi, likisema, "machoni mwa baadhi ya watu, msimamo wa nchi za magharibi kuhusu vita vya Ukraine unanuka unafiki." Kutoka Vietnam, Afghanistan hadi Afrika Kusini, gazeti la New York Times liliwahoji makumi ya watu kuhusu mzozo wa sasa wa Ukraine, na majibu yao yameonyesha kwamba "wakati wengi wanasikitishwa na vita na vifo vya watu wasio na hatia, hawakubali kile kinachoitwa 'haki’ na ‘uovu’ kwa mujibu wa vigezo vya Marekani na Ulaya. Hawawezi kusimama na nchi za magharibi kinafiki." Naresh Chand, Luteni Jenerali mstaafu wa Jeshi la India ambaye alipata mafunzo nchini Russia na Ukraine alisema: "Popote wanapokwenda (Marekani), mwisho wanapoondoka, wanaacha fujo.”

Hata hivyo, ripoti kama iliyotolewa na gazeti la the New York Times ni nadra kuchapishwa katika vyombo vya habari vya magharibi. Hali halisi ni kuwa baada ya mgogoro huo kuibuka, nchi za magharibi, kupitia nguvu zake kubwa kwenye sekta ya vyombo vya habari, zilianzisha kampeni ili kufikia “ushirikiano”. Kupitia utendajikazi wa kauli mbiu kama vile uhuru, haki za binadamu na kile kinachoitwa "mfumo wa kimataifa unaozingatia kanuni", vyombo vingi vya habari vimezielezea nchi za magharibi kama "walinzi" wa maadili, haki za binadamu na uhuru, huku vikipuuza kwa makusudi malengo yaliyojificha nyuma kama vile jiografia ya kisiasa na ajenda ya kiuchumi. Hata hivyo, cha kuchukiza zaidi ni kwamba katika nchi za magharibi ambako kile kinachoitwa “uhuru wa kujieleza” ni muhimu zaidi, huku nchi hizo zikitumia vyombo vyao vya habari kueneza habari zao, vyombo vya habari vya Russia na mashirika ya habari yamepigwa marufuku kutoa maoni yao kwenye vyombo vya habari vya nchi hizi. Mnamo Machi 12, YouTube ilitoa taarifa ya kuzuia kabisa akaunti za vyombo vya habari vya serikali ya Russia ikiwemo "Russia Today", shirika la habari la Russia Sputnik, na Red Star TV kwa msingi wa "kukanusha, kupunguza au kudharau vurugu zilizothibitishwa"; mbali na hayo, YouTube pia imeongeza usimamizi na kwamba video yoyote inayokwenda kinyume na mitazamo ya magharibi katika mzozo huo itazuiliwa.

Hasa baada ya Russia kupata ushahidi wa silaha za maangamizi makubwa huko Ukraine, hatua ya kufumba midomo ya Russia ilizidi kushangaza. Ni wazi kuwa nchi za magharibi zinawafanyia hila watu wa dunia kwa kadri wanavyoweza.

Kwa miongo kadhaa, Marekani inaendesha kwa remoti “Arab Spring” yaani mfululizo wa maandamano, maasi, na uasi wa kutumia silaha dhidi ya serikali ulioenea sehemu kubwa ya ulimwengu wa Kiarabu mwanzoni mwa miaka ya 2010 na kuongoza “Colour revolution” yaani harakati mbalimbali za kupinga serikali na kuandamana katika Ulaya na Asia…kwa ajili ya maslahi yake binafsi, imeshambulia nchi nyingi duniani, ikiwa ni pamoja na Iraq, Afghanistan, Syria na nchi za Afrika, na kuwaua maelfu ya watu wasio na hatia wakiwemo watoto na watu wanyonge. Na sasa mzozo wa Ukraine umewawezesha watu kutambua tena unafiki na sera ya umwamba iliyo nayo nchi hiyo.
 
Huo ndio ukweli mkuu, wamarekani na nato ni wanafiki sana, Putin ametusaidia sana kila nchi iwe ba mifumo yake sio kila kitu kutegemea nchi nyingine
Yaani Vita vya Ukraine vimefichua uovu wa vyombo vya habari vya magharibi Kama BBC, Aljazeera, CNN, Fox News, Sky News na kadhalika....yaani kwa kiasi kikubwa vyombo hivi vkmedharaulika mno sehemu mbalimbali duniani...habari zake ni news spinning, propaganda...no objective reporting...it is totally biased reporting...stupid Western media...
 
Hakika hii vita imetufunza mengi ,lakini wapo popoma akina 254 watakuja pinga hii facts kwa evidence za west media
 
Bandiko Safi sana nchi za Magharibi na USA zimeja unafiki mkubwa Sana na mwisho watu wamekuja kuona unafiki wao kwa mlango wa nyuma wa haki za watu na demokrasia
 
Back
Top Bottom