Nchi za mabeberu wana Ramani zinazoonyesha maliasili ilipo Tanzania na nchi nyingine mbili. Wao wanaamini walitukabidhi tuwatunzie lakini si zetu

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,399
Nchi za Tanzania, Angola na Congo DRC ni nchi muhimu katika mstakabali mapinduzi ya viwanda barani Ulaya na Marekani.

Mwaka 2020 Uingereza walitangaza kuachana na magari yatumiayo mafuta ya diseli na petroli kufikia mwaka 2030 na wameazimia kuanza kutengeneza magari zaidi yatumiayo betri.

Hata hivyo tayari magari yatumiayo betri tayari yanatengenezwa katika nchi mbalimbali barani Ulaya.

Nchi za kibeberu au maadui wa maendeleo hawawezi kuiruhusu Tanzania iendelee kwa kuwa na viwanda vyake .

Pia Tanzania ina malighafi zote kutengeneza hata seti za televisheni, vioo vya madirisha na balbu.

Kuna mambo matatu makuu ambayo sisi binadamu twapaswa kufahamu.

Mambo hayo ni technical know what, technical know how and technical know why.

Darasani mwalimu hutufundisha kuhusu somo la jiografia, kisha kuingia ndani kufanya tathmini kutumia kifaa maalum cha Compass kwa kutumia ramani na hiyo ni technical how.

Pale uanzapo kujiuliza hii Compas imetengezwa vipi ndipo unapoingia kwenye technical know why.

Mabeberu wanakuambia kuwa Afrika kuna dhahabu tatu ambazo ni Tanzania, Angola na Congo DRC.

Mabeberu wanaendelea kuziangalia nchi tatu ambazo nchi za Tanzania, Angola na Congo DRC ambazo wana malengo ya muda mrefu hadi miaka 50.

Katika nchi hizo ni Tanzania ambayo wao mabeberu wana uwezo wa kuingia na kujichotea maliasili watakavyo.

Kutokea bandari ya Lobito iliopo Benguela kupitia Lusaka, Lubumbashi ni ukanda maalum ulojaa madini, mafuta na madini ya uranium ambavyo ni malighafi muhimu kwa utengenezaji wa betri za magari, simu za mkononi na mabomu ya nyuklia na mitambo yake.

Lango kuu la kuingia kwenda huko ndani au (interior) na kutokea ni Bagamoyo na ni njia rahisi kuliko kuzunguka Cape Town.

Ila mabeberu hao wakadai kuwa watakuja kwa mazungumzo na ikiwa mazungumzo yatashindikana basi watatumia mbinu zozote kuhakikisha wanafanikiwa azma yao.

Wazungu hao wanasema kuwa Tanzania ni nchi ya kuingia na kutokea Afrika kupitia Bagamoyo. Pia wanasema kuwa asilimia 60 ya biashara ya meli kuanzia mwaka 2050 itakuwa ndani ya bahari ya Hindi na hiyo ndio itakuwa Ocean of the future.

Hivyo, meli yaweza kutoka bandari ya Lobito kupitia Dar-es-Salaam hadi mfereji wa Suez bila shida na kwa uharaka zaidi.

Na hivyo ndivyo mfalme Leopold wa pili wa Belgium alivyokubaliana na wakoloni wa kijerumani kujenga reli ya kati ambayo ingesafirisha bidhaa zote za malighafi kutoka katikati ya Tanzania na Afrika kuelekea bahari ya Hindi.

Mfalme huyo alikuwa akivuna zao la mpira na kulisafirisha kwenda Ulaya kutengeneza bidhaa mbalimbali kama matairi ya magari, baiskeli na zingine yaani alikuwa "supplier" mkubwa.

Moja ya viwanda vikubwa ambavyo mfalme huyo alikuwa akiviuzia malighafi ya mpira ni kiwanda kinachotengeneza bidhaa za Dunlop.

Waafrika wengi sana raia wa Congo walikufa wakivuna zao hilo na wengine kukatwa mikono kwa kushindwa kufanya hivyo.

Bahari ya Hindi ni bahari ilojaaliwa kila aina ya maliasili kuanzia mafuta, gesi asilia na uranium. Leo hii twashuhudia jinsi magaidi wa kupandikizwa nchini Msumbiji wakitumika kama kivuli cha wizi wa maliasili hizi zinazoibwa usiku na mchana.

Mwandishi Robert Kaplan katika kitabu chake cha Monsoon - "The India Ocean and Future of American Power" anaitaja bahari ya Hindi kama New Great Game kama ndo njia ya China ikitumia meli zake kubwa za mafuta kusaka maliasili hiyo ndani ya bahari ya Hindi.

Lakini safari hii upo uwezekano mkubwa wa vita ndani ya bahari hiyo baina ya nch iza kibeberu yaani Marekani na China.

Kaplan anaelezea muungano wa nchi za Marekani, China na India katika bahari ya Hindi katika kufanya biashara, kuzuia vitendo vya utekaji meli yaani Piracy, kulinda njia za usafiri wa meli na kuitikia wito wa majanga ndani ya bahari hiyo.

Bila shaka kelele za ujenzi wa bandari ya Bagamoyo ni moja ya vielelezo vya mpango wa nchi za kibeberu.

Mkataba wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo ulofumuliwa na hayati John Magufuli haukuwa mkataba uloweka maslahi ya taifa mbele na ulikuwa ni wa miaka 99.

Mkataba huo pia haukuwa unaruhusu maendelezo yoyote ya bandari zingine kama bandari ya Dar-es-Salaaam, Tanga, Zanzibar.

Hiyo ni kwasababu Bagamoyo ndo lango kuu la kuingiza na kutoa rasilimali zote zinatoka ndani ya Tanzania na maliasili zingine zinazotoka ndani ya Congo DRC na Angola.

Kwa vile nchi za kibeberu tayari wana ramani ya Afrika na sehemu zilipo maliasili basi Tanzania pamoja na Angola na Congo DRC na wanafahamu kuwa sasa hivi ujazo wa Uranium na madini mengine umefikia kiwango cha juu kiasi cha kuweza kuvunwa, basi sisi hatuna ujanja.

Tanzania tunapaswa kueleza wazi msimamo wetu na pia kueleza ni nini tunataka kwani mali tunayo.

Tanzania haina budi kulinda ukanda wa bahari ya Hindi hadi Msumbiji kuhakikisha usalama wake hauingiliwi kirahisi. Serikali pia inawajibika kueleza msimamo wake kuhusiana na mkataba wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo.

Lakini si kuanza kuzunguka mbali na kuanza mijadala ya kupoteza muda huku tayari wenzetu wachache wamekaa tayari na mabeberu na wamepanga nini kinachofuata.

La sivyo tunakubali kuwa sie ni waangalizi tu wa rasilimali tulozikalia na tupo tayari kuzigawa bure au kwa ujira kiduchu.
 
Nchi za Tanzania, Angola na Congo DRC ni nchi muhimu katika mstakabali mapinduzi ya viwanda barani Ulaya na Marekani.

Mwaka 2020 Uingereza walitangaza kuachana na magari yatumiayo mafuta ya diseli na petroli kufikia mwaka 2030 na wameazimia kuanza kutengeneza magari zaidi yatumiayo betri.

Hata hivyo tayari magari yatumiayo betri tayari yanatengenezwa katika nchi mbalimbali barani Ulaya.

Nchi za kibeberu au maadui wa maendeleo hawawezi kuiruhusu Tanzania iendelee kwa kuwa na viwanda vyake .

Pia Tanzania ina malighafi zote kutengeneza hata seti za televisheni, vioo vya madirisha na balbu.

Kuna mambo matatu makuu ambayo sisi binadamu twapaswa kufahamu.

Mambo hayo ni technical know what, technical know how and technical know why.

Darasani mwalimu hutufundisha kuhusu somo la jiografia, kisha kuingia ndani kufanya tathmini kutumia kifaa maalum cha Compass kwa kutumia ramani na hiyo ni technical how.

Pale uanzapo kujiuliza hii Compas imetengezwa vipi ndipo unapoingia kwenye technical know why.

Mabeberu wanakuambia kuwa Afrika kuna dhahabu tatu ambazo ni Tanzania, Angola na Congo DRC.

Mabeberu wanaendelea kuziangalia nchi tatu ambazo nchi za Tanzania, Angola na Congo DRC ambazo wana malengo ya muda mrefu hadi miaka 50.

Katika nchi hizo ni Tanzania ambayo wao mabeberu wana uwezo wa kuingia na kujichotea maliasili watakavyo.

Kutokea Lobito kupitia Lusaka, Lubumbashi hadi Benguela ni ukanda maalum ulojaa madini, mafuta na madini ya uranium ambavyo ni malighafi muhimu kwa utengenezaji wa betri za magari, simu za mkononi na mabomu ya nyuklia na mitambo yake.

Lango kuu la kuingia kwenda huko ndani au (interior) na kutokea ni Bagamoyo na ni njia rahisi kuliko kuzunguka Cape Town.

Ila mabeberu hao wakadai kuwa watakuja kwa mazungumzo na ikiwa mazungumzo yatashindikana basi watatumia mbinu zozote kuhakikisha wanafanikiwa azma yao.

Wazungu hao wanasema kuwa Tanzania ni nchi ya kuingia na kutokea Afrika kupitia Bagamoyo. Pia wanasema kuwa asilimia 60 ya biashara ya meli kuanzia mwaka 2050 itakuwa ndani ya bahari ya Hindi na hiyo ndio itakuwa Ocean of the future.

Hivyo meli yaweza kutoka bandari ya Lobito kupitia Dar-es-Salaam hadi mfereji wa Suez bila shida na kwa uharaka zaidi.

Na hivyo ndivyo mfalme Leopold wa pili wa Belgium alivyokubaliana na wakoloni wa kijerumani kujenga reli ya kati ambayo ingesafirisha bidhaa zote za malighafi kutoka katikati ya Tanzania na Afrika kuelekea bahari ya Hindi.

Mfalme huyo alikuwa akivuna zao la mpira na kulisafirisha kwenda Ulaya kutengeneza bidhaa mbalimbali kama matairi ya magari, baiskeli na zingine yaani alikuwa "supplier" mkubwa.

Waafrika wengi sana raia wa Congo walikufa wakivuna zao hilo na wengine kukatwa mikono kwa kushindwa kufanya hivyo.

Bahari ya Hindi ni bahari ilojaaliwa kila aina ya maliasili kuanzia mafuta, gesi asilia na uranium. Leo hii twashuhudia jinsi magaidi wa kupandikizwa nchini Msumbiji wakitumika kama kivuli cha wizi wa maliasili hizi zinazoibwa usiku na mchana.

Mwandishi Robert Kaplan katika kitabu chake cha Monsoon - "The India Ocean and Future of American Power" anaitaja bahari ya Hindi kama New Great Game kama ndo njia ya China ikitumia meli zake kubwa za mafuta kusaka maliasili hiyo ndani ya bahari ya Hindi.

Lakini safari hii upo uwezekano mkubwa wa vita ndani ya bahari hiyo baina ya nch iza kibeberu yaani Marekani na China.

Kaplan anaelezea muungano wa nchi za Marekani, China na India katika bahari ya Hindi katika kufanya biashara, kuzuia vitendo vya utekaji meli yaani Piracy, kulinda njia za usafiri wa meli na kuitikia wito wa majanga ndani ya bahari hiyo.

Bila shaka kelele za ujenzi wa bandari ya Bagamoyo ni moja ya vielelezo vya mpango wa nchi za kibeberu.

Mkataba wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo ulofumuliwa na hayati John Magufuli haukuwa mkataba uloweka maslahi ya taifa mbele na ulikuwa ni wa miaka 99.

Mkataba huo pia haukuwa unaruhusu maendelezo yoyote ya bandari zingine kama bandari ya Dar-es-Salaaam, Tanga, Zanzibar.

Hiyo ni kwasababu Bagamoyo ndo lango kuu la kuingiza na kutoa rasilimali zote zinatoka ndani ya Tanzania na maliasili zingine zinazotoka ndani ya Congo DRC na Angola.

Kwa vile nchi za kibeberu tayari wana ramani ya Afrika na sehemu zilipo maliasili basi Tanzania pamoja na Angola na Congo DRC na wanafahamu kuwa sasa hivi ujazo wa Uranium na madini mengine umefikia kiwango cha juu kiasi cha kuweza kuvunwa, basi sisi hatuna ujanja.

Tanzania tunapaswa kueleza wazi msimamo wetu na pia kueleza ni nini tunataka kwani mali tunayo.

Tanzania haina budi kulinda ukanda wa bahari ya Hindi hadi Msumbiji kuhakikisha usalama wake hauingiliwi kirahisi. Serikali pia inawajibika kueleza msimamo wake kuhusiana na mkataba wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo.

Lakini si kuanza kuzunguka mbali na kuanza mijadala ya kupoteza muda huku tayari wenzetu wachache wamekaa tayari na mabeberu na wamepanga nini kinachofuata.

La sivyo tunakubali kuwa sie ni waangalizi tu wa rasilimali tulozikalia na tupo tayari kuzigawa bure au kwa ujira kiduchu.
LOOoo, unachosha sana na mizunguko isiyokuwa na maana aiseee!
Para mbili tatu zingetosha kabisa kueleza kitu.

Haya, 'source' yako ya haya mambo ni ipi?

Haya mambo ya kukazania 'Mabeberu,.... mabeberu' kila wakati na kusahau kuwasilisha habari muhimu ya taarifa inazingua sana.

Sasa sijui hapa kijadiliwe kipi, mabeberu, au njia tunazoweza kuzifanya tunufaike na hizi mali zetu?

Utanisamehe kama nitakukwaza kwa haya niliyoandika, lakini ukweli nimekwazwa na njia yako ya uwasilishaji wa habari yenyewe, ambayo nadhani ni habari muhimu.

Andiko la Hovyo kabisa nililopata kusoma!
 
Hata hiyo mikataba tukipewa tuisome yachosha hivyohivyo na ndo twaishia kusaini bila kusoma hadi mwisho na kuelewa.
 
Hii Ni hotuba?utenzi?, Hadithi au kitu gani mbona sijaelewa ila Ni km vile kimetafsiriwa
Soma na urudie tena na tena.

Hayo ni mawazo yangu "pure and simple".

Ni aina ya uwasilishaji ndo umekuchanganya.

Mikataba huja kwa mtindo huohuo na hautelewi twasema sawa na twaambiwa saini hapa waanguka kusaini.
 
Kiwango cha elimu waliyokuwanayo wakati wanatutawala kilikua ni cha juu sana kulinganisha na uelewa wetu wa mambo. Wakiona udongo tu wanafahamu madini yanayopatikana katika udongo ule.

Kuna siku mmoja nilimjonyesha picha ya Tanzania sehemu yenye udongo mwekundu. Aliniambia chini ya hii ardhi kuna copper nyingi sana.
 
Kiwango cha elimu waliyokuwanayo wakati wanatutawala kilikua ni cha juu sana kulinganisha na uelewa wetu wa mambo. Waliona udongo tu wanafahamu madini yanayopatikana katika udongo ule.

Kuna siku mmoja nilimjonyesha picha ya Tanzania sehemu yenye udongo mwekundu. Aliniambia chini ya hii ardhi kua copper nyingi sana.
Hawa hawakukaa bure mkutano wa Berlin Conference tena miezi mitatu tarehe 15 November1884 hadi tarehe 26 February 1885
 
Adui yetu sio beberu, adui yetu ni yule anaewapa beberu rasilimali zetu kwa kusign mikataba ya hovyo na kupokea 10%
Nini kifanyike pale unapokuwa kiongozi wa nchi ya kiafrika na wapigiwa simu mbalimbali kutoka kwa mabebru wanokwambia twataka uranium.

Au baadae watakuja watasema rekebisheni sheria ya madini ya 2017 ni ngumu sana yatubana.

Sisi twataka tuchote kwanza kisha tuanze kuwalipa baada ya 5 years.

Nini kinapaswa kifanyike?
 
Hawa hawakukaa bure mkutano wa Berlin Conference tena miezi mtatu terehe 15 November1884 hadi tarehe 26 February 1885
Ule mkutano niliona video yake, fikiria wakati ule walikua na uwezo wa kujirekodi. Uingereza iliwakilishwa na mwanasheria. Walimuonea wivu sana Mjerumani kuipata Tanganyika maana ilimtajirisha katika kipindi cha muda mfupi.
 
Kutokea Lobito kupitia Lusaka, Lubumbashi hadi Benguela ni ukanda maalum

Lobito katika mkoa / jimbo la Benguela nchini Angola.

Lobito ni bandari na mji katika jimbo la Benguela Angola.

Lobito–Dar es Salaam Railway​

Railway Line
The Lobito–Dar es Salaam Railway, is a planned Narrow gauge railway line that connects the Angolan port city of Lobito to the Tanzanian port city of Dar es Salaam, through the Zambian city of Kapiri Mposhi

The justification for this railway line is to promote exports of the three countries, through which the railway passes, to the continents of Europe, the Americas and Asia. The line would also increase tourism into those three countries, in addition to creating jobs and improving local economies.

The railway link would also allow the distribution of imported goods from overseas into the three African countries, as well as promote intra-African trade, among those countries.

The government of Angola is prepared to spearhead the efforts to build the Lobito-Kapiri Mposhi section of the railway line and is looking upon Zambia and Tanzania to harmonize the integration of the new construction with the existing Tazara Railway. No timelines have been made public, as of December 2020.
Source : Plans to build Angola-Tanzania trans-African railway picks up pace
 
Lobito katika mkoa / jimbo la Benguela nchini Angola.

Lobito ni bandari na mji katika jimbo la Benguela Angola.

Lobito–Dar es Salaam Railway​

Railway Line
The Lobito–Dar es Salaam Railway, is a planned Narrow gauge railway line that connects the Angolan port city of Lobito to the Tanzanian port city of Dar es Salaam, through the Zambian city of Kapiri Mposhi
Sawasawa nilimaanisha Lobito ipo Benguela.

Hiyo wao waiona ni njia muhimu kusafirisha bidhaa zao adimu hadi badari kubwa ya Bagamoyo.

Ndo maana Bagamoyo yatakiwa kujengwa.
 
Tupunguze woga, reli hii toka bandari ya mji wa Lobito ktk pwani ya bahari ya Atlantic nchini Angola ikiunganishwa na Dar es Salaam au hata Bagamoyo itakuza uchumi wa nchi za maeneo ya kusini mwa Afrika.

Tukumbuke hivi sasa kuna treni ya kitalii inatoka Cape Town mpaka stesheni ya TAZARA jijini Dar es Salaam.

Cape Town - Dar es Salaam Reli hiyo Ikipandishwa kutoa huduma kwa abiria wa kawaida, mizigo na biashara halafu ikawepo ya Dar es Salaam to Lobito Angola basi Tanzania itakuwa kitovu cha biashara kama enzi za kina Tip Tippu. Wakati Zanzibar ikiwa dola kubwa ilikuwa na wafanyabishara waliojipenyeza kibiashara, kijasusi, kijeshi mpaka Manyema DR Congo hadi bahari ya Atlantic Congo Brazaville na Angola.

Zanzibar kuwa Taifa kubwa la kibiashara muda huo Ikasababisha vita ya kijeshi na Ubelgiji. Vita 1892 / 1894 WHKMLA : History of the Belgo-Arab War, 1892-1894 ambayo ilichagizwa kwa ukubwa kuhusu maslahi ya kiuchumi hivyo majeshi ya kibelgiji ya King Leopold yaliyokuwa Congo na majeshi ya Dola Kubwa ya Zanzibar chini ya mwana wa Tippu Tip yaliyokuwa huko Congo yakisindikiza biashara maeneo hayo ya Afrika ya Kati kupambana.
The Congo–Arab War (also known as the Congolese–Arab War, Belgo–Arab War or Arab Wars) took place in what is now the Democratic Republic of the Congo between the forces of Belgian King Leopold II 's Congo Free State and various Zanzibari Arab slave traders led by Sefu bin Hamid, the son of Tippu Tip. Fighting occurred in the eastern Congo between 1892 and 1894.

Congo–Arab War | Military Wiki | F…

military.wikia.org/wiki/Congo%E2%80%93Arab_War

military.wikia.org/wiki/Congo%E2%80%93…

Turuke / fast forward 2021 Taifa kubwa la Tanzania likitumia diplomasia ya uchumi, umahiri ki Geopolitics na tukitengeneza ushawishi tulionao ulioanzishwa toka enzi za kina Tippu Tip , Julius Nyerere , Dr. Augustine Mahiga , Dr. Hussein Mwinyi na sasa utawala wa Samia Suluhu Hassan.

Tunaweza kutumia nafasi yetu hiyo kuinufaisha nchi na raia wake kujitanua kibiashara, kiviwanda, usafirishaji majini, reli na bandari na kurudia kuwa dola kubwa eneo la Ukanda huu na pia kuvutia wadau wa Maendeleo kuwekeza kwa wingi Tanzania ikawa Dubai au Singapore ya 'Afrika'.

Mwaka huu 2021 Tanzania imepata zawadi ya Mungu kutumia uwezo wake mkubwa, kututaka tuende kuwa nchi ya asali na maziwa (Dubai, Macao, Singapore, Uruguay, Luxembourg)hivyo tuachane na siasa zilizopita za udhanifu wa kuwepo mabeberu-maruhani, kunyanyasa waTanzania wanaofanya kazi kwa bidii na sasa tujielekeze kwenye Uhuru na Haki kutakochochea nchi na raia wake kuneemeka na kuwa mfano wa kuigwa kwa kubadilisha maisha ya watanzania kuwa matajiri na wenye furaha.
Placing 41st out of 152 in the ranking, Uruguay is the highest Latin American country on the list topped by Norway. The Sustainable Economic Development Assessment (SEDA) measures wellbeing in ten dimensions split across three categories; economics, investments and sustainability. Source: Uruguay is most prosperous Latin American country
 
Back
Top Bottom