Nchi za Kiafrika zitaendelea kutawaliwa kwa muda mrefu zaidi

Unknown2

JF-Expert Member
Oct 16, 2016
2,344
4,981
Baada ya kutusoma akili zetu wazungu waliamua kutafuta njia nzuri za kututawala bila sisi wenyewe kujua huku wakiendelea kutuvuna kadiri wanavyoweza, kadiri ya fursa iliyopo katika eneo husika. Baada ya kutafakari kwa kina wakaamua kutumia chocho zifuatazo:

1. Kutumia viongozi wasio waaminifu kwa kuwahakikishia kula nao na kuwalinda.

Nchi nyingi zimeangukia hapa. Kama ulisoma hadithi ya The Bold iitwayo Vipepeo Weusi basi jua kuwa kila nchi ya kiafrika kuna taasi kama The Board au inayofanania. Ukiwa mbishi unaonyeshwa kuzimu chap kwa haraka sana.

2. Kuwagombanisha huku wao wakiendelea kuvuna kadiri wawezavyo.

Nchi kama Kongo, Africa ya Kati na Libya zimeangukia hapa. Msubiji baada ya ugunduzi wa gesi iko kwenye hatihati ya kuangukia kundi hili.

3. Kutumia taasisi za kidini.

Hapa huwatumia waumini wasioelewa dunia inavyoendeshwa kupigana au kufanya maamuzi kwenye taasisi wanazofanyia kazi kwa kudhani wanampigania Mungu wao. Nchi kama Nigeria ni kati ya waathirika wakubwa wa njia hii.

4. Kumiliki njia zote za kiuchumi.

Hapa inabidi uwategee wao ili uchumi wako uweze kuendelea kuwa hai. Ukibishana nao hawachelewi kukuwekea vikwazo vya kiuchumi na hapo lazima utetereke.

5. Kuwekeza kwenye teknolojia na kumiliki silaha zote kali za kivita.

Hapa mwafrika unalazimika kununua silaha kwao iwapo utataka silaha zenye ufanisi.
Katika hali ya kawaida vitu kama ndege za kivita na rada wanakuwa wana uwezo wa kuviendesha wakiwa kwao hivyo ni wazi kwamba utavitumia iwapo havitakuwa na athari kwao.

Uwezo wako wa kivita hasa silaha wanakuwa wanaujua kwani unakuta kila nyenzo muhimu unanunua kwao wakati huohuo hawakuruhusi kumiliki silaha kali kama vile zile za nyuklia. Hii ni kumaanisha kuwa hakuna namna utaweza kupambana na kivita.

Bahati mbaya kwetu hawa watu hushirikiana. Mchina akitaka kitu kwa Mmarekani atapewa hata kama ni kwa kubadilishana kwa kitu kingine.
Usipoangukia upande wa Mmarekani na washirika wake basi utaangukia upande wa Mchina/Mrusi na washirika wao.

Binafsi naamini kuwa hakuna kiongozi mzalendo katika ya kiafrika yenye manufaa (madini, gesi, mafuta nk )kwa Mzungu atakuja kudumu katika uongozi.

Viongozi wengi wamejikuta wakisaliti nchi zao kwa tamaa zao au kwa ajili kulinda uhai wao.

Wakati tukihangaika na katiba mpya na kupingana na ufisadi nadhani ni vema tukaangalia kwa undani cha tatizo.

Sio rahisi wanaotutawala (Ukoloni wa kisasa/Ukoloni mamboleo) kutuachia kirahisi. Kuna kazi ya ziada ya kufanya ambayo sio rahisi kama kweli tunataka kujitawala.

Wakati tukiwaza na kutafuta suluhisho tuendelee kuwa wazalendo kwa nafasi tunazozitumikia, ya Mungu mengi, huenda siku moja tukajitawala kama ilivyo kwa hao tunaowaita Mabeberu.
 
Andiko lako zuri ingawa halina pendekezo la suluhu au halioneshi kisa kilichoifikisha Afrika hapa tangu awali wakati wa utumwa na ukoloni ili tuanze kujihami. Tatizo siyo ukali na wingi wa silaha. Ni uwezo wetu wa kufikiri na kuchukua hatua. Tazama Israel au Korea zote mbili. Tunahitaji akina Nyerere 50 hivi kwenye nchi moja ambao wanashirikiana kwenye uongozi. Lakini tazama wengi wetu hata Nyerere mwenyewe hatukumwelewa wala kumwuunga mkono kwa dhati karika fikra za kiwango cha juu na utekelezaji wake. Shukran sana mkuu!
 
Tumepewa uhuru muda mrefu sana lakini hatuachi kulalamika kila siku.
 
Wenzetu kama Korea Kusini, Singapore na Vietnam ambao tulikuwa nao sawa miaka ya 60 sasa hivi wako mbali sana, sisi bado tunalalamika na kujificha kwenye kichaka cha "mabeberu".Upuuzi mtupu.
 
Back
Top Bottom