sammosses
JF-Expert Member
- Jan 24, 2011
- 1,682
- 1,110
Jana nimefuatilia impeachment abuse of power zikiwakilishwa hoja za kumuondoa rais Trump madarakani, nimekiri bado Waafrika wana Safari ndefu kuishi kwenye utawala wa sheria.
Ushahidi wa matumizi mabaya ya madaraka uliwasilishwa kwa hoja nzito,ukiwepo tuhuma mbali mbali za rushwa.
Pamoja na upinzani mkali wa kihoja kwa pande zote mbili republican na democratic wote wanakiri kuwa rais hayupo juu ya sheria.
Wakati democratic wanaamini kuwa rais anajiona yupo juu ya sheria ndiyo maana anatumia madaraka yake vibaya hali itakayo athiri national security. Republican hawaamini kuwa yupo juu ya sheria kwa kuwa alichokifanya utekelezaji wa majukumu yake.
#Hojayangu
Uwazi huu wa kumkosoa na kutokuwa na imani na Rais kwa kutumia madaraka yake vibaya, waafrika hatuna ubavu huo.
Wenzetu Rais ni mtumishi wa umma ana wajibika kwa maslahi ya umma pia, akienda kinyume wana vyombo vyenye mamlaka ya kumhoji ambavyo huku kwetu ni bunge.
Ukisoma katiba yetu kuna mgawanyo wa madaraka katika mihimili mitatu,ambayo ni Bunge,serikali na mahakama.
Mwingiliano uliopo ni mkubwa sana na mhimili unaonekana kuhodhi mamlaka ya mihimili mingine ni serikali.
Leo Rais anaweza kumuagiza speaker wa bunge kufanya jambo, na bunge likaona sawa.
Serikali inaweza kulidhoofisha bunge kwa kuwa tu rais ambaye ndiye mwenyekiti wa chama kinachoongoza dola ana mamlaka ndani ya chama kumpitisha speaker kuwa mgombea wa ubunge na mgombea wa kiti cha speaker kupitia chama chake kama zawadi ili kukidhi matakwa ya chama na rais bila kudhibitiwa na chombo chochote.
Hali hii imetokea kwa speaker kuwatishia wabunge tena bungeni kuwa wasipopitisha bajeti ya serikali rais atavunja bunge,ana uhakika wabunge wengi hawatarudi hususani wa chama chake.
Haya ni matumizi mabaya ya madaraka, ni rushwa ya kimamlaka kwa wabunge wanao toka ndani ya chama chao wakihofia kulinda ubunge.
Wanao umia ni wananchi kwa kuwa wanapoteza national security yao kwa maslahi ya watu wachache wenye malengo ya kung'ang'ania madaraka na kugawana vyeo.
Rais akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kuingia madarakani, akijibu swali la separation of power, alisema serikali ndiyo mhimili mkuu ambao unaweza kuingilia mipaka ya mihimili.
Kwa majibu hayo hata kama rais ni sehemu ya bunge alipaswa kuheshimu na kuilinda katiba aliyoapa kuilinda na kuhifadhi.
Kilicho fanyika kwenye kikao cha Congress hapo jana kinapaswa kuwa fundisho kwa nchi zetu za dunia ya tatu.
Ili viongozi wa Afrika wasimamie maslahi ya wananchi, lazima tuwe na vyombo madhubuti visivyo hofia nguvu ya dola kwa maslahi ya wananchi.
Tuna bezwa sana kuwa tuna tumia mamlaka tuliyopewa na wananchi kubadili katiba zetu kwa maslahi binafsi.
Tupo kwenye karne ya 21 bado tawala zetu hazina mwelekeo tunaongozwa kwa mujibu wa nini. Tuamke saa ya mabadiliko ni sasa.