Nchi za D8 zaipiga teke dollar kuanza kutumia sarafu zao kwenye biashara

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,991
17,888
Nchi za D8 zataka kutumia sarafu ya taifa katika biashara zao
Katibu Mkuu wa kundi la nchi 8 za Kiislamu zinazostawi maarufu kwa kifupi kama D8 amesema nchi wanachama zinafanya jitihada za kufikia mapatano ya kutumia sarafu za taifa katika miamala ya kibiashara baina ya nchi hizo.
Dato' Ku Jafaar Ku Shaari amesema kuwa, uchunguzi wa pendekezo hilo lililotolewa na Rais Recep Tayyip Erdoğan wa Uturuki katika mkutano wa D8 Oktoba mwaka 2017 tayari umeanza. Katibu Mkuu wa D8 ameashiria uwezekano wa kuanzisha kituo cha kubadilishana bidhaa kwa bidhaa baina ya nchi wanachana katika siku zijazo na kuongeza kuwa, kumeanzishwa mazungumzo na kampuni moja ya teknolojia ya masuala ya elektroniki kwa ajili ya kubuni kadi za miamala ya kifedha za D8 ambazo zinaweza kuharakisha miamala ya aina hiyo.
Kundi la D8 la nchi za Waislamu zinazostawi ni kundi la kiuchumi linalozijumuisha pamoja nchi za Iran, Uturuki, Pakistan, Bangladesh, Indonesia, Malaysia, Misri na Nigeria. Kundi hilo liliundwa tarehe 15 Juni mwaka 1997 kwa pendekezo la aliyekuwa waziri mkuu wa Uturuki na kiongozi wa chama cha Kiislamu cha Refah, marehemu Necmettin Erbakan kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi za Waislamu.
Inaonekana kuwa, nchi za D8 zimeelewa vyema kwamba, kuna udharura mkubwa wa kutumia sarafu za mataifa yao katika mialama yao ya kibiashara. Hii ni kutokana na ukweli kwamba, kutumia safari mashuhuri zinazotumiwa sasa katika biashara ya kimataifa kama safaru ya dola ya Marekani kunazifanya nchi hizo zikabiliwe na madhara makubwa katika masoko ya fedha ya kimataifa.
Katika upande mwingine ni kuwa, kutotumia safari za kitaifa kunazifanya nchi za D8 zikabiliwe na hatari kubwa ya athari mbaya za vikwazo vya upande mmoja vya Marekani kama inavyoshuhudiwa sasa ambapo serikali ya sasa ya Washington imeziwekea vikwazo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Uturuki kwa visingizio visivyo na maana wala msingi wowote.
Vilevile kutumia safari za kitaifa katika miamala ya kibiashara na kichumi kutazidisha thamani ya sarafu za mataifa hayo kutokana na kupungua haja ya kutumia safaru za kigeni, suala ambalo pia litazuia mfumuko wa bei na ughali wa maisha.
Suala hilo pia katika upande mwingine litathabitisha uchumi wa mataifa hayo ya Waislamu ya kuvutia uwekezaji wa kimataifa katika masoko ya D8.
Kwa msingi huo kuna udharura kwa nchi wanachama katika D8 zizidishe ushirikiano wa kiuchumi, kurahisisha miamala ya kibiashara na kubuni stratijia na sera imara za kuweza kukabiliana na mashinikizo ya kiuchumi ya madola ya Magharibi na vikwazo dhalimu vya nchi hizo.
4bpw9d258847611bb5r_800C450.jpg
4bpwb121c0af241bb69_800C450.jpg
 
Unawezaje kuzungumzia nchi za kiislam ukaiacha Saudia? Hicho kiumoja automatically kitasambaratika chenyewe maana kimekaa kidinidini zaidi! Hakuna kitu kibaya kama kujibagua hususan kwa mlengo wa kidini maana mnajiona ninyi ni bora kuliko wao wakati huo huo mnawahitaji wao ili mambo yenu yaende. Hopeless cartel!
 
Unawezaje kuzungumzia nchi za kiislam ukaiacha Saudia? Hicho kiumoja automatically kitasambaratika chenyewe maana kimekaa kidinidini zaidi! Hakuna kitu kibaya kama kujibagua hususan kwa mlengo wa kidini maana mnajiona ninyi ni bora kuliko wao wakati huo huo mnawahitaji wao ili mambo yenu yaende. Hopeless cartel!
Inaonekana hii taarifa imekuumiza kweli
 
Hata € walisuasua na ilipoanza ilikuwa chini kwa thamani, lakini ilipanda.
Kila kitu ni uthubutu tu
Africa labda turudi kwenye burter trade system muhogo kwa samli
 
Mbona wakina Magu na wenzie hapo juzi huko Arusha wamelijadili hilo suala
Km kujadili walishajadili sana tena tokea kipindi cha mkapa sema utekelezaji ndyo mtihani

Same to AU kila siku kwenye mikutano yao wanatoka na maadhamio kibao, ila utekelezaji ni zero

Hilo suala la kuwa na sarafu moja karibia mwaka wa ishirini wanalizungumzia lakini utekelezaji hakuna
 
Nchi za D8 zataka kutumia sarafu ya taifa katika biashara zao
Katibu Mkuu wa kundi la nchi 8 za Kiislamu zinazostawi maarufu kwa kifupi kama D8 amesema nchi wanachama zinafanya jitihada za kufikia mapatano ya kutumia sarafu za taifa katika miamala ya kibiashara baina ya nchi
Kichwa cha habari na contents tofauti.
 
Ina population kubwa ya muslim
Mengine hata sielewi
Religious composition nchini Nigeria ni Christians-48%; Muslims-46% na wengineo ni "Animists".

Nigeria ilijiunga na jumuia za kimataifa za kiislam kama OIC pale nchi ilipokuwa chini ya General Ibrahim Babangida (Mwislamu) lengo likiwa ni kupata "Handouts" fulani fulani kutoka kwa waarabu lkn sio eti kwa kuwa nchi ilikuwa na waislamu wengi.

Kuna mataifa mengine kama Uganda ambayo pia Iddi Amin aliwapeleka huko OIC japo waislamu ktk Uganda walikuwa ni 10% tu.
 
Hili la mataifa hayo kujaribu kubuni namna ya kufanya biashara pasipo kutumia USD ni rahisi sana kuiongea hivyo lkn kiutekelezaji ina "Technicalities" fulani fulani ambazo lazima zitawakwamisha tu mbele ya safari.

Nchi hizi zina chumi ambazo ni tegemezi sana na sarafu ambazo ni very volatile kuweza kuaminika ktk biashara ya kimataifa na hata wakisema wafanye (Barter Trade) bado itahusu bidhaa fulani chache tu.

Ni ngumu sana kwa Barter Trade kuweza kufanyika kwa ufanisi ktk dunia ya leo kwani kuna vitu lazima utahitaji kununua kwingineko ambako Barter Trade sio choice na lazima utatumia tu dola. Watakaojaribu huo mfumo watakwama na watarejea tena kwenye "Convention", hawana namna.
 
Back
Top Bottom