Nchi za Afrika zinaunga mkono Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
VCG111366651594.jpg

Hassan zhou

Awamu ya 24 ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi itafunguliwa Beijing mnamo Februari 4. Kutokana na hali ya hewa ya joto kwa mwaka mzima katika maeneo mengi ya Afrika, inaeleweka kuwa ni nchi chache tu, zikiwemo Eritrea, Ghana, Madagascar, Morocco na Nigeria ndizo zitakazopeleka wachezaji kwenye michezo hiyo. Lakini, hii haizuii nchi za Afrika kuunga mkono Michezo hiyo. Hivi karibuni, ili kukabiliana na kauli zisizofaa zilizotolewa na nchi chache za magharibi zikiongozwa na Marekani, nchi nyingi duniani zikiwemo za Afrika zilitoa kauli za kutounga mkono kauli hizo mbaya, zikitahadharisha kwamba Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi haipaswi kuwa ya kisiasa, na badala yake itasaidia kuleta watu pamoja.

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari tarehe 25 alitoa taarifa akisema anaunga mkono kwa dhati Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing ya 2022 na anaamini kuwa itakuwa ya kipekee na kufanyikiwa. Licha ya kutotuma timu katika mashindano hayo, rais wa Tanzania Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema olimpiki ni tamasha kubwa la michezo duniani, hivyo haipaswi kuingizwa mambo ya siasa na kwa kusheshimu moyo wa olimpiki tu ndipo tunaweza kutimiza umoja wa kimataifa na kauli mbiu ya olimpiki: kasi zaidi, juu zaidi na nguvu zaidi. Mwenyekiti wa Kamati ya Olimpiki ya Zimbabwe, Tabani Gunye, alisema Michezo ya Olimpiki ni fursa ya "kuunganisha dunia" na kwamba "michezo na siasa hazipaswi kuchanganywa". Katika mkutano wa nane wa mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC uliofanyika mwezi Novemba mwaka jana, nchi za Afrika zote zilielezea dhamira yao ya kukuza maendeleo endelevu na yenye afya ya Olimpiki na kupinga kuingiza siasa kwenye michezo.

Katika kipindi cha nyuma, Marekani iliongoza kundi la washirika ikiwa ni pamoja na Australia, Uingereza na Canada kufanya kile kilichoitwa "kususia kisiasa" kwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing kwa misingi inayoitwa "haki za binadamu", na kutangaza kwamba haitatuma maafisa wa serikali au wanadiplomasia kwenye Michezo hiyo. Hata hivyo, ndani ya mwezi mmoja baada ya kutoa kauli hii, Marekani "ilijidhalilisha" na kuomba viza kwa maafisa wake kuja China, na kuacha washirika wake katika hasara ya kutojua la kufanya. Wakati huo huo, mashirika ya kimataifa kama vile Umoja wa Mataifa, Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki, na watu wa nchi nyingi wameonyesha uungaji mkono na matarajio yao kwa Michezo ya Olimpiki na kupinga siasa za michezo. Hii ina maana kwamba mpango wa itikadi kali ulioanzishwa na nchi za Magharibi dhidi ya China umeshindwa, kwa sababu idadi ndogo ya nchi za Magharibi haiwakilishi jumuiya ya kimataifa.

Kama alivyosema Susan Brownell, profesa wa anthropolojia katika Chuo Kikuu cha Missouri huko St. Louis, Marekani, China haitarudi nyumba hata kidogo kutokana na shinikizo la nchi za Magharibi kuhusu masuala ya maslahi ya kitaifa. Kwa baadhi ya masuala yenye uelewa tofauti, China iko tayari kufanya mazungumzo ya maana na yenye kujenga na nchi za Magharibi, lakini kuingiliwa katika masuala ya ndani kamwe hakukubaliwi. China inajitahidi kuimarisha na kudumisha sifa yake kama mwenzi anayewajibika na mwaminifu, na kupata kuungwa mkono na nchi nyingine kwa kanuni yake ya msingi ya kutoingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine, zikiwemo nchi nyingi zinazoendelea za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.
 
Back
Top Bottom