Nchi yetu inawezaje kuwa Tanzania ya viwanda bila kupitia daraja liitwalo mapinduzi ya Kilimo?

Bushmamy

JF-Expert Member
Aug 18, 2019
8,848
15,219
Nchi nyingi zilizoendelea duniani zote zilipitia katika mfumo wa mapinduzi ya kilimo kwanza kabla ya viwanda.

Katika karne ya 18 huko uingereza na marekani mapinduzi ya kilimo ndio yaliyoleta mapinduzi ya viwanda hadi hii leo tunaziita nchi za viwanda.

Je mapinduzi ya kilimo ni nini?

Ni tekniki mpya na kisasa. katika kilimo na ufugaji hivyo kusababisha au kuleta wingi wa chakula, afya njema na ongezeko la watu.

Je ni kwa jinsi gani au namna gani Mapinduzi ya kilimo yanaweza kuleta mapinduzi ya viwanda Nchini?

Masoko ya nje,
Tukiwa na wingi wa mazao mengi ni rahisi kuuza nje ya nchi na hivyo kupata fedha za kigeni ambapo tutakuza pato la taifa let na Fedha hizo hizo tutazitumia katika ujenzi wa viwanda.

Mali ghafi.
Mali ghafi toka shambani zitatumwa au kutumika viwandani. Mfano mazao kama nyanya zitasindikwa na kutengeneza bidhaa kama sosi ya nyanya (tomatoes source).

Viatu vya ngozi kutoka kwa wanyama kama ng'ombe nk. Na hii itachochea ongezeko la viwanda aina kwa aina.

Viwanda vya Trekta za kilimo na mashine za uvunaji zitaanzishwa pamoja na Dhana mbalimbali za kilimo.

Viwanda /makampuni ya usafirishaji yatazaliwa kutokana na wingi wa malighafi pamoja na wingi wa watu,na hii yote ni kutokana na kilimo.

Miundombinu kama vile njia za treni, pamoja na barabara itajengwa zaidi na zaidi kutoka vijijini huko kwenye mashamba hadi mjini kuliko na viwanda ili kurahisisha usafirishaji wa bidhaa pamoja na watu kwa haraka.

Ujenzi wa viwanda vijijini huko ambako ndio malighafi hutokea na hivyo kuchochea ongezeko la viwanda mjini na vijijini.

Viwanda vya vyakula vya mifugo pamoja na kilimo kuongezeka kila pande kutokana na wingi wa kilimo na ufugaji wa kisasa.

Pamoja na mambo mengine mengi tunaona ni kwa namna gani nchi yetu inaweza kupiga hatua kutoka hapa tulipo hadi kuwa katika nchi ya viwanda na sio kuhubiri tu mdomoni habari ya Tanzania ya viwanda bila kushirikiana na kuwawezesha vijana katika kilimo chenye tija ili kuleta mapinduzi ya viwanda ambapo idadi kubwa ya vijana wangejiajiri na kuajiriwa huko.

Ni ukweli kuwa wanasiasa wa leo katika nchi yetu hawatufikishi popote bali wapo kwa ajili ya maslahi yao tu na ndio maana hali ya wananchi wa kawaida inazidi kuwa ngumu kila uchwao.
00202.jpg
 
Mimi nashangaa,tangia tupige kelele humu tunahitaji mapinduzi ya kilimo tuna ardhi kubwa tu haitumiki ipasavyo,hakuna linalofanyika,inaelekea ni mkakati maalumu watanzania tubaki na umaskini kwa sababu zao
 
Tanzania kiasili ilikua ni nchi ya wakulima na wafanyakazi lakini alipokuja kulikoroga ni huyu mwendazake akashift kwenye machinga huku watu wakishangilia na kusifu akasahau kuwa hawa watu hawainui viwanda vya ndani ila zaidi kujaza bidhaa za nje na kuharibu mipangalio ya miji kama tunavyoona leo kilimo kimebaki cha chakula na mazao ya biashara yanakufa ie chai,korosho,katani n.k
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom