Nchi yetu inaruhusu ndoa za mikataba kwa muda mfupi?

Mfiaukweli

JF-Expert Member
Aug 30, 2018
5,636
8,774
Wanasheria; hivi nchi yetu inaruhusu ndoa za mikataba kwa muda mfupi?
Nauliza hivi kwa kuwa cheti cha ndoa ni cha aina moja tu nchini - I stand to be corrected - (na ndoa inakuwa specified kama ya kiserikali, kidini au kimila).

Kwa mfano wana ndoa wakisema wanataka kufunga ndoa kwa mujibu wa dini ya Kikristo basi automatically ndoa hiyo itajulikana kuwa ni ya mume na mke mmoja.
Shida inakuja kwenye ndoa za Kiislamu, wenzetu wana aina ya ndoa za muda mfupi (mutaa'h nikah kwa Shia na Misyar kwa Sunni), ambapo ndoa inaweza ikawa ya hata saa moja kulingana mahitaji ya mume.

Je sheria ya ndoa inazitambua ndoa hizo za mkataba?
 
Ndoa ni makubaliano ya kudumu ya kuishi pamoja kati ya mwanamke na mwanaume. Kinyume cha hapo hiyo haisabiki kama ni ndoa. Yapo mambo mengi katika hizo ndoa unazosema yaani mutaah. Ni vyema ujue historia yake na misingi ya sheria ya Kiislamu kabda hujaipitisha na kuitumia kama refernce ya kujenga hoja yako

Ni kama vile leo hii mtu akurupuke na kuanza ku refer ndoa za watu wa jinsia moja zinazofungishwa na baadhi ya makanis aya ulaya na Marekani kua ndio Ukristo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom