Nchi ya wanasiasa na siasa toka juu Taifa hadi Kijijini: CCM mna dhamana

CalvinKimaro

JF-Expert Member
Sep 11, 2017
244
312
NCHI YA WANASIASA NA SIASA TOKA JUU TAIFA HADI KIJIJINI: CCM MNA DHAMANA

Tanzania imegeuka Taifa la ajabu sana. Ni Taifa pekee siasa inafanywa na kila mtu, kila mahali na kila muda.

Hakuna Taifa jingine duniani ambalo karibu kila mtu, kila kitu na kila sehemu kinachofanyika ni siasa. Na hali hii imeletwa na jambo moja ambalo halisemwi. Ni SIASA kuwa ndio njia nyepesi kujipatia utajiri.

Huko nyuma wakati siasa hailipi siasa ilibaki kufanywa vikaoni na ilikuwa shughuli ya watu waliojitolea kutumikia wenzao.
Mara tu tulipoweka mazingira ya mtu kutajirika kupindukia kila mtu akaona atanye siasa popote na wakati wote hata kama hakuna anachosaidia wenzake.

Ili tulirudishe Taifa kwenye mstari na kuliepusha na hatari iliyo dhahiri tunapaswa kuondoa mazingira haramu tajirishi kwenye siasa.

Na hapa ndio kuna mtihani wetu! Kwa nini?

Kwenye SIASA HELA watu wameunda a SILENT SYNDICATE! Ikifika hapo hakuna cha CCM, CHADEMA, CUF, NCCR, TADEA, TLD! Woote wanakuwa paka wa rangi na tabia moja! Hata wafuasi wao wanajiunga nao! Maana apatacho Kidawa humfikia Juma!

Sasa siasa hadi nyumba kwa nyumba! Kila mtu anaota zimfikie huko aliko! Baba CCM, mama CDM, mtoto ACT, mjukuu CUF hausigeli NCCR! Kila mmoja anacheza tombola!

Lakini nani anabeba lawama kuu? Hakika ni CCM!

Wanasiasa wa CCM ndio walituletea Azimio la Zanzibar! Likaua Azimio lilikomesha SIASA TAJIRISHI.

Kwa mantiki hii wa kututibu ni CCM. Kwanza ndiye aliyeleta hizi siasa na pili ndiye mwenye dhamana ya kuliongoza hili Taifa.

Miongoni mwa mambo yaliyosimika UTAJIRISHO kwenye siasa ni haya:

1. Mishahara na marupurupu ya ubunge. Wao wanaita POSHO! Kuna tofauti Kati ya MSHAHARA na POSHO. Bungeni ni MSHAHARA! Mwenye kulipwa posho halipwi pensheni! Wanazuga eti ni POSHO!
2. Mafao ya kila baada ya miaka 5. Haiwezekani umalize kazi mwaka 2000 ulipwe mafao urudi ufanye kazi ile ile ulipwe tena mafao makubwa zaidi mwaka 2005!
Halafu wengi wao wameshalipwa mafao makazini! Na wengine wanakula mafao ya Utumishi huko walikokuwa!
3. Mikopo: ubunge umekuwa sifa ya kulopea mamilioni ama mabilioni. Ubunge umekuwa fursa ya kukopa gari. Gari ambalo hata mtu angefundishwa Hadi awe profesa ataliona kwenye TV.
4. Mfuko wa jimbo: haingii akilini kwa nini maendeleo hayatokani na bajeti! Mfuko huu ni wizi mtupu. Inastaajabisha hata CAG aliyesifiwa hakutueleza matumizi ya huu mfuko wa miujiza!
5. Matibabu nje ya nchi: inashangaza kuwa ukiwa mbunge hospitali yako ni nje! Tena bure bilashi wakati wapiga kura unadai hawana huduma za matibabu! Mbunge anayetibiwa Apollo bila haya anasimama na kudai jimboni kwake hakuna huduma ya afya! Na anashangiliwa! Zitakuwepo wakati wabunge wanatumia 30% au zaidi kwa matibabu nje? Hivi wao afya zao bora kuliko zetu?
6. Wafanyabiashara bungeni: Mwalimu alituonya mno kuhusu hili. Mfanyabiashara wa usafiri akijadili mpango au bajeti husika unadhani atatetea maslahi ya nani? Tena siku hizi mtu anaingia hana hata genge la bamia anatajirikia bungeni anaanza biashara bungeni.

Ili tuepuke janga linalotunyemelea ni vyema haya yakatazamwa upya. Na hakika ni CCM na Serikali yake ndio inaweza kutuepusha na hili janga.

CCM tuondoleeni SIASA TAJIRISHI mlizotuletea! Hivi hamuoni Kwa nyie kupenda utajiri kinyume na waasisi wa ninyi ndio mnawawezesha watu ili wakatukane BBC, VOA, DW? Mnadhani nani wanawalipa wanaofyeka mashamba na kuchoma nyumba za wenzao? Ni mliowatajirisha!

Na mkiendelea kuwajaza mahela basi tutarajie janga kubwa mno baadae. Hizo hela Bora mpeleke vijijini watu waboreshewe huduma.

Viongozi wetu wa CCM ninyi ndio mna Serikali. Wabunge wenu wakikataa au mkiwanyima SIASA TAJIRISHI hata hao wahuni watasinyaa. Sasa hivi mnatajirika wote ndio maana wana kiburi.

Futeni mapato haya haramu bila kujali maslahi yenu. Ondoeni wafanyabiashara bungeni. Mwalimu alisema waende wakafanye biashara hukoo!

Wasalaam
 
Nikikosoa hata ulipoweka nukta na koma nitakuwa mbinafsi. Umemaliza kila kitu mkuu. Tumeyaongea sana haya, na tukitaka nchi yetu ianze kwenda bila fitina tuifanye Siasa kuwa kazi ya wito.
 
Back
Top Bottom