Nchi ya Tanzania imebakiwa na muhimili mmoja tu

Nedago

JF-Expert Member
Sep 26, 2018
908
1,348
Nakumbuka tulipokuwa shule ya msingi hapa hapa Tanzania,katika somo la maarifa ya jamii/saizi Uraia. Tulifundishwa na kuaminishwa kuwa Tanzania ina mihimili mitatu yaani Serikali,Bunge na Mahakama na kila muhimili uko huru na hauingiliwi na mwingine,lakini hawakuandika kuwa hii mihimili inaweza kubadirika na kubaki miwili au mmoja kulingana na itakavyoamua Serikali au Rais aliyepo madarakani wa wakati huo.

Inabidi sasa serikali kupitia wizara ya elimu irekebishe kwenye kipengere kile wanafunzi waelewe mapema ili wajue mapema kupunguza lawama baadae wakijitambua. Maana naona kwasasa ndivo hali ilivyo siri-kali imeiweka mihimili iliyo baki under arrest.

Mihimili hii miwili imewekwa kwapani wao ni ndio ndio ndio hakuna wanachofanya,kwakweli yachukiza hata haya hawaoni?

Sijasoma katiba lakini sidhani Kama inasapoti ushuzi unaofanyika sasa.
 
Nakumbuka tulipokuwa shule ya msingi apa apa tz,katika somo la maarifa ya jamii/saizi Uraia.tulifundishwa na kuaminishwa kuwa Tanzania ina mihimili mitatu yaani serikali,bunge na mahakama na kila muhimili uko huru na hauingiliwi na mwingine,lakini ###hawakuandika kuwa hii mihimili inaweza kubadirika na kubaki miwili au mmoja kulingana na itakavyo amua serikali au raisi aliepo madarakani wa wakati huo.inabidi sasa serikali kupitia wizara ya elimu irekebishe kwenye kipengere kile wanafunzi waelewe mapema ili wajue mapema kupunguza lawama baadae wakijitambua.maana naona kwasasa ndivo hali ilivyo siri-kali imeiweka mihimili iliyo baki under arrest.mihimili hii miwili imewekwa kwapani wao ni ndio ndio ndio hakuna wanachofanya,kwakweli yachukiza hata haya hawaoni????.sijasoma katiba lakini sidhani Kama inasapoti ushuzi unaofanyika sasa.
Ikulu ndo bunge na ikulu ndo mahakamana ikulu.
 
Ukiisoma katiba ukaielewa na kisha ukatafakari kinachoendelea nchini sasa unaweza kufikiri kuwa hii si Tanzania. Utakasirika zaidi na utajua kwa hakika kuwa umesalia mhimili mmoja tu kwenye hii nchi na mingine yote inayopaswa kuwa mihimili imekuwa vibaraka wa mhimili huo mmoja.
 
Kinadharia alikubali ipo mihimili 3 ila mmoja umejikita chini kabisa.


Kama hapa

45146052_1190164237815765_3037597310650417152_n.jpg
 
Aisee inakera Sana.
Ukiisoma katiba ukaielewa na kisha ukatafakari kinachoendelea nchini sasa unaweza kufikiri kuwa hii si Tanzania. Utakasirika zaidi na utajua kwa hakika kuwa umesalia mhimili mmoja tu kwenye hii nchi na mingine yote inayopaswa kuwa mihimili imekuwa vibaraka wa mhimili huo mmoja.
 
Mi naamini hata wadau wanashinda kesi au kupata dhamana pale muhimili mmoja ulijichimbia unapoamua na si vinginevyo na pia mijadala inaweza kutopitishwa pale bungeni kama mhimili ule hauna interest na mjadala huo

Nimeona mahakama imemuondolea makosa yote Diane Rwigala kule Rwanda nikacheka maana najua bwana yule wa kule kaamua kuachana na hiyo kesi na sio kwamba haki hiyo imetolewa na mahakama!
 
Ni kweli mihimili mingine imekufa kama sio kubaki kama kivuli tu.Hii ni shida kubwa sana imepelekea haki kutotendeka kabisa.
 
Panya yupi ataenda kumfunga paka kengele ilhali wote wanataka kuishi?
 
Ukichunguza hali hii haikuanza awamu hii. Kwanza sheria asilimia zaidi ya 99.9 hutungwa na serikali bunge ni kupitisha tu, hata pale wanapopinga baadhi ya vipengele bado mabadiliko yanakuwa ya kiujanjajanja. Halafu sheria inapata nguvu pale tu inaposainiwa na rais (ikisemwa yeye pia ni sehemu ya bunge lakini ni sentensi ya kijanja ukweli yeye ndiye muamuzi wa mwisho). Ina maana rais ni zaidi ya bunge.
Mahakama nayo inaweza kuamua kufuta sheria fulani lakini serikali ikaja na nyingine inayopinga uamuzi huo (rejea kesi ya mgombea binafsi), hali inayoonesha kuwa serikali ndiye mwamuzi.
Nafikiri wajuzi wanaweza kutueleza zaidi.
 
Bwana yule alisema kuna mhimili ambao umejichimbia zaidi kuliko miingine yote,nadhani mshaujua ni mhimili gani huo.
 
Back
Top Bottom