Nchi ya Saudi Arabia imeamua kuruhusu ujenzi wa makanisa

mtanganyika wa kweli

JF-Expert Member
Apr 12, 2015
2,420
1,717
Nchi ya Saudi Arabia imeamua kuruhusu ujenzi wa makanisa baada ya kusainiwa kwa makubaliano kati ya viongozi wa Wahhabi na Kadinali wa Vatican.
-
Makubaliano hayo kati ya Rais wa Baraza la Kipontifiki ya midahalo ya dini mbalimbali, Kadinali Jean-Louis Tauran na Sheikh Mohammed bin Abdel Karim Al-Issa, ambaye ni Katibu Mkuu wa NGO kubwa ya Wahhabi yanalenga kuruhusu ujenzi wa makanisa pamoja na mikutano ya Waislamu na Wakristo mara moja kila baada ya miaka miwili.
-
Saudi Arabia ni moja ya nchi zisizo na uvumilivu kwa dini nyingine zaidi ya Uislamu. Wasio waislamu wanaadhibiwa kwa kuonesha matendo ya dini yao nje ya nyumba zao huku Muislamu yeyote anayeamua kubadili dini akihukumiwa kifo. Sheria za kiislamu zinawahusu wote wanaoishi nchini humo bila kuzingatia imani zao huku Jeshi la Polisi likisimamia ufuatwaji wake.
-
Hadi sasa inakadiriwa kuwa kuna Wakristo zaidi ya Milioni 1.5 nchini humo ambao ni wahamiaji wanaofanya kazi hususani kutoka nchi ya Ufilipino.
-
Uwezekano wa kufanikiwa kwa harakati hizi za Vatican zilizoanza mwaka 2008 ulianza kuonekana baada ya Mwanamfalme Mohammed bin Salman kuingia madarakani ambapo amedhamiria kubadili muonekano wa nchi hiyo kimataifa kwa kubadili mambo kadhaa.
-
Katika kipindi chake tayari ameshabadili taratibu kadhaa zilizokuwepo kwa miaka mingi kama wanawake kutoruhusiwa kuendesha magari na kutakiwa kuwa na mwangalizi muda wote.
C&P#JF
jamiiforums-20180507-0001.jpg
 
Roho wa Mungu aendelee kuwaongoza..ila chakushangaza hawa wachungaji waliojazana huku kwenye Uhuru wa kuabudu hawaendi kutangaza injili huko.
 
"Katika zama za mwisho Dunia itajawa na maarifa ya utukufu wa Mungu kama maji yaifunikavyo bahari.."
 
Hii ni hatua nzuri hasa ikizingatiwa jinsi Saudi Arabia ilivyo na kimbelembele cha kujenga misikiti ktk maeneo mengi duniani.

Waache watu waabudu kwa hiari imani waipendayo kwani haya mambo ni "Wito" na hayahitaji mabavu kama walivyokuwa wakifikiri.

Na mwisho wa siku ni Mwenyezi Mungu mwenyewe ndiye atakayeamua na wala sio mwingine. Bwana asifiwe sana. Amen.
 
Roho wa Mungu aendelee kuwaongoza..ila chakushangaza hawa wachungaji waliojazana huku kwenye Uhuru wa kuabudu hawaendi kutangaza injili huko.
Watanyongwa mkuu

Kwan wao hawaogopi kufa..ahaha

Dah KUMBE ULIKUWQ UKIBADILI UNANYONGWA ,NCHI ILIKUWA YA KISENGE UNALAZIMISHWA KUAMINI
 
Sipati picha Kanisa la Kwanza litakavyo jaa Waarabu seat hazitatosha wallai
 
Ni ujinga uliopitiliza karne 21 unataka upangie watu cha kuabudu, uwaamulie mungu wao ambae unamtaka yeye.

Dini zinafanya watu wanakua wajinga sana.

Fafanua dini gani zinazomfanya ntu kuwa mjinga? Najua nchi moja huko Asia mgeni haingii nchini kama hana dini yoyote. Wanasema mtu ambaye hana dini si mtu huyo. Wewe unasema wenye dini ni wajinga.Eleza!
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom