Nchi ya Rwanda na Rais wake Paul Kagame wamekuwa mfano bora na wa kuigwa katika kupambana na COVID-19

shakur kimboka

JF-Expert Member
May 11, 2013
203
500
Kuna nchi moja hapa hapa Afrika Mashariki ( nimeisahau Jina kwa sasa ) nasikia ina ' cases ' kama 1350 hivi za wenye COVID-19 na waliokufa hadi sasa ni zaidi ya 75 wanakimbilia 95 sasa. Na nasikia hiyo nchi ukitaka uwekwe ndani Wewe sema tu idadi Kubwa ya wenye COVID-19 utakiona cha Moto. Na hiyo nchi ilivyo ya Kishamba eti yenyewe inadhani kusema kuwa ina Maambukizi mengi ya COVID-19 ni aibu kwa Jumuiya ya Kimataifa ( Duniani )

Ni bahati mbaya sana hiyo nchi nimeisahau kwa Jina ila nikiikumbuka huko mbeleni katika huu huu Uzi wangu nitaitaja tu. Wenye Akili Kenya, Rwanda na Uganda wala hawafichi na wanaonyesha kweli kweli Juhudui zao katika Kupambana na COVID-19 na pia katika Kuwaokoa Watu ( Wananchi ) wao.

Sijui ni kwanini nimeisahau ghafla hiyo nchi. Naanza Kuzeeka ( Kukongweka ) sasa nadhani.
Bora ujisahaulishe hivyo hivyo,

Tumehifadhi babu zako, wajomba na dada zako hapa kwa kipindi chote wakati hampo stable kiuchumi wala kisiasa(60s-90s) na wengi tumeshawafukia hapahapa kwenye ardhi yetu na hivi ndivyo mnavyo tulipa kwa ukarimu na utu wetu?

Kweli shukrani ya punda ni mateke na sisi tunazidi kujifunza kutokana na makosa tuliofanya mwanzo

Sent using Jamii Forums mobile app
 

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
6,522
2,000
nimekumbuka Dada zake wanavyorefusha nyeti na akili zako zako kama zimerefushwa kabla ya muda wake


USSR
Kama Rwanda haina ' Rasilimali ' nyingi kama zilizoko nchini Kwako lakini Rais wake anaweza Kujibana na Kuzitumia hizo hizo ndogo na nchi yake inaenda na hata Kuiacha yako Kimaendeleo je, huoni kuwa Wewe ambaye una ' Rasilimali ' nyingi ( lukuki ) na idadi hiyo Kubwa ya Watu lakini hamna mbele wala nyuma mtakuwa na ' Upopoma ' mwingi? Nasubiri jibu lako juu ya hili tafadhali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Smart911

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
69,958
2,000
Dah! Hii kitu inauma na inaumiza sana kwenye hiki kipindi cha mlipuko wa Covid19...

Hakuna unafuu, taratibu wala mikakati yoyote ya kupunguza makali...


5. Wanajali sana Mapato ya Kodi kuliko kujua idadi ya Wagonjwa wanaoongezekaCc: mahondaw
 

Kim Jong Jr

JF-Expert Member
Mar 15, 2014
9,436
2,000
Acha ujuaji ww mtoa mada.
Unasema Rwanda mfano wa kuigwa mbona licha yalockdown yao Bado maambukizi yanazidi kuongezeka kuliko nchi zote za EA, mpaka kagame ameamua kuongeza mda wa lockdown mpaka 19 April?

Unasema nchi zinaficha data sahihi, twambie wewe unayejua zilizokamili.

Tatzo upinzani wako umekuharibu akili.

Nyie ndo mnapenda kila siku kusikia idadi ya wagonjwa wameongezeka TanzaniA.

Kwa taarifa yako hakuna lockdown Tanzania na Mungu mkuu yupo juu ya ardhi hii sasa.

Mnatumwa na mabeberu
Watanzania Ni misukule Nani kakwambia lockdown Ni lazima case zipungue

Sent using Jamii Forums mobile app
 

broken ages

JF-Expert Member
Mar 23, 2012
225
225
M

broken ages
Mbona umeniquote Mimi na kunivisha tuhuma zisizokuwepo hayo maswali muulize mtoa mada sio Mimi.
GIRITA samahani sana naomba niwie radhi maana nilikuwa namaanisha kumjibu mtoa mada ambaue ni GENTAMYCINE
na kwa bahati mbaya nikawa nimeku-quote wewe naomba GENTAMYCINE anielewe na wala sina sababu ya kumtuhumu ila nilikuwa tu na maana ya kumwelewesha ili aelewe kwamba TANZANIA hatujifunzi kuishi kama Rwanda ama nchi nyingine yeyote bali tunaishi kama TANZANIA na tunapaswa kuwapenda,kuwathamini na kuwamini viongozi wetu na hasa mkuu wa nchi yetu.
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
16,451
2,000
Mkuu tutumie muda mwingi kuelimisha jamii namna ya kujikinga na ugonjwa huu, tuache lawama

Wataacha vipi kulaumiwa kama wamejikita kwenye kufanya ndivyo sivyo?

Nini kisichojulikana kuhusiana na ugonjwa huu?
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
16,451
2,000
Serikali ya Rwanda kupitia Rais wake imefanya yafuatayo..

1. Inawajali Wananchi wake mara kwa mara juu ya Ugonjwa
2. Inatoa Msaada wa Vyakula bure kabisa kwa Wananchi wake
3. Inatoa bure kabisa Vifaa vya Kujiinga na Ugonjwa kwa Wananchi wake
4. Waziri wake wa Afya hana Unafiki katika Kutoa Taarifa sahihi kwa Wananchi
5. Kwa Rwanda huu Ugonjwa siyo wa Aibu au wa Kuficha kwa Jumuiya ya Kimataifa
6. Viwanja vya Ndege na Mipaka yote Umakini umeongezeka na Kudhibitiwa
7. Imeunganisha nguvu na Jumuiya ya Kimataifa katika Kutafuta Suluhu ya Ugonjwa duniani

Serikali zingine duniani na Marais wao wamefanya yafuatayo

1. Wanaficha Taarifa za Wagonjwa kwa Wananchi wao
2. Marais wao wanajificha Kuuongelea wakidhani ni Ugonjwa la laana
3. Mawaziri wao wa Afya wakizungumza ni Kuchekacheka tu kama Ngiri na Mizaha mingi
4. Wananchi wao wanajazana hovyo hadi Kujambiana sana katika DalaDala
5. Wanajali sana Mapato ya Kodi kuliko kujua idadi ya Wagonjwa wanaoongezeka
6. Wanaficha Taarifa za Ugonjwa ila chini chini wanaomba Misaada ya Pesa WB
7. Viongozi wao wanakataza Mikusanyiko ila wao wakiongea wanakusanya Watu wengi

Nchi zingine za Afrika bado hajizachelewa Kuiiga Rwanda na hasa Kumuiga Rais wake Mahiri na bora kabisa Paul Kagame.

Ni aibu kuwa bunge linaendelea.

Bajeti gani wakuu wakati Corona inaweza kuja kutusambaratisha?

Kwanini posho mnazolipana zisije huku kuunga mkono juhudi za kumaliza ugonjwa huu hapa nchini?
 

Kitanga

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
366
250
Mkuu tutumie muda mwingi kuelimisha jamii namna ya kujikinga na ugonjwa huu, tuache lawama
Nimetoka Musoma juzi lakini nilichokiona huko njiani ni kuwa mabasi mengin ehayafuati maelekezo yaliyotolewa na serikali hasa matumizi ya vitakasa mikono kwa abiria. Watu wanapanda bila kutumia vitakasa mikono. Kwa kweli eleimu lazima itolewa na ikibidi kuwepo na ukaguzi standi za mabasi na hata ndani ya basi lenyewe kama kuna vitakasa mikono
 

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
43,836
2,000
Nimetoka Musoma juzi lakini nilichokiona huko njiani ni kuwa mabasi mengin ehayafuati maelekezo yaliyotolewa na serikali hasa matumizi ya vitakasa mikono kwa abiria. Watu wanapanda bila kutumia vitakasa mikono. Kwa kweli eleimu lazima itolewa na ikibidi kuwepo na ukaguzi standi za mabasi na hata ndani ya basi lenyewe kama kuna vitakasa mikono

Kwani ungewasilisha Hoja yako tu bila Kuitaja Musoma isingeeleweka?
 

yahoo

JF-Expert Member
Sep 9, 2011
3,448
2,000
Mkuu kwa kuwa unauwakika wa kupokea salary ya magufuli kila mwezi ndo unataka na sisi tufungiwe ndani kama hako kakijiji ka Rwanda ili upate sababu ya kushinda kwenye tv ukiangalia mchezo na mkeo?, maisha sio copy and past acha wao wafanye yao kivyao
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom