Nchi ya Rwanda na Rais wake Paul Kagame wamekuwa mfano bora na wa kuigwa katika kupambana na COVID-19

Kuna nchi moja hapa hapa Afrika Mashariki ( nimeisahau Jina kwa sasa ) nasikia ina ' cases ' kama 1350 hivi za wenye COVID-19 na waliokufa hadi sasa ni zaidi ya 75 wanakimbilia 95 sasa. Na nasikia hiyo nchi ukitaka uwekwe ndani Wewe sema tu idadi Kubwa ya wenye COVID-19 utakiona cha Moto. Na hiyo nchi ilivyo ya Kishamba eti yenyewe inadhani kusema kuwa ina Maambukizi mengi ya COVID-19 ni aibu kwa Jumuiya ya Kimataifa ( Duniani )

Ni bahati mbaya sana hiyo nchi nimeisahau kwa Jina ila nikiikumbuka huko mbeleni katika huu huu Uzi wangu nitaitaja tu. Wenye Akili Kenya, Rwanda na Uganda wala hawafichi na wanaonyesha kweli kweli Juhudui zao katika Kupambana na COVID-19 na pia katika Kuwaokoa Watu ( Wananchi ) wao.

Sijui ni kwanini nimeisahau ghafla hiyo nchi. Naanza Kuzeeka ( Kukongweka ) sasa nadhani.
sasa kama ugojwa wenyewe unaweza kufichika manayake hauna uhalisia ni wakawaida sema tuna tiana hofu tuu bora waendelee kuficha hivyohivyo m bona magojwa yapo mengi tu nayanauwa kila siku bila matangazo ni ulimbukeni kutangazatangaza inasaidia nini kutangaza wambie watu wachukue tahadhari inatosha china wenyewe waliacha kutangaza ndio mana wapo salama sasa

Sent from my CPH1903 using JamiiForums mobile app
 
Mpk leo 02/04 Rwanda maambukizi ni watu 82,Kenya maambukizi ni 110.

Hebu tusaidie ku-justify statement yako ya 'Rwanda maambukizi yanazidi kuongezeka kuliko nchi yoyote ile EA'
Kama Rwanda wako 10m plus na Kenya wako 50m plus then wagonjwa ni 82 kwa 110 mtawalia , waliothirika hapo zaidi ni nani? Bila watu kufikiri vzr wanasiasa watafanya ugonjwa wa korona neema ya kuteka wananchi wao, kilo moja ya unga na moja ya mchele kwa familia za kiafrika ni msaada ama kejeli?! Fikirieni vzr mtajua mchezo wote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu muda wa kupiga majungu ulitakiwa uelimishe watu jinsi gani ya kujikinga na corona!
Serikali ya Rwanda kupitia Rais wake imefanya yafuatayo..

1. Inawajali Wananchi wake mara kwa mara juu ya Ugonjwa
2. Inatoa Msaada wa Vyakula bure kabisa kwa Wananchi wake
3. Inatoa bure kabisa Vifaa vya Kujiinga na Ugonjwa kwa Wananchi wake
4. Waziri wake wa Afya hana Unafiki katika Kutoa Taarifa sahihi kwa Wananchi
5. Kwa Rwanda huu Ugonjwa siyo wa Aibu au wa Kuficha kwa Jumuiya ya Kimataifa
6. Viwanja vya Ndege na Mipaka yote Umakini umeongezeka na Kudhibitiwa
7. Imeunganisha nguvu na Jumuiya ya Kimataifa katika Kutafuta Suluhu ya Ugonjwa duniani

Serikali zingine duniani na Marais wao wamefanya yafuatayo

1. Wanaficha Taarifa za Wagonjwa kwa Wananchi wao
2. Marais wao wanajificha Kuuongelea wakidhani ni Ugonjwa la laana
3. Mawaziri wao wa Afya wakizungumza ni Kuchekacheka tu kama Ngiri na Mizaha mingi
4. Wananchi wao wanajazana hovyo hadi Kujambiana sana katika DalaDala
5. Wanajali sana Mapato ya Kodi kuliko kujua idadi ya Wagonjwa wanaoongezeka
6. Wanaficha Taarifa za Ugonjwa ila chini chini wanaomba Misaada ya Pesa WB
7. Viongozi wao wanakataza Mikusanyiko ila wao wakiongea wanakusanya Watu wengi

Nchi zingine za Afrika bado hajizachelewa Kuiiga Rwanda na hasa Kumuiga Rais wake Mahiri na bora kabisa Paul Kagame.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom