Nchi ya mafisadi; wakubwa,wadogo na watarajiwa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nchi ya mafisadi; wakubwa,wadogo na watarajiwa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Humble Servant, Oct 2, 2008.

 1. H

  Humble Servant Member

  #1
  Oct 2, 2008
  Joined: Aug 2, 2007
  Messages: 87
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ndg Wajumbe!
  kabla ya kunyooshea wengine vidole nataka tutafakari kama kweli sisi hatupo kwenye kundi mojawapo la mafisadi! maana kila mmoja sasa anaonekana kuchukizwa na rushwa na mabaya yote yanayo nyima haki na kunyanyasa wanyonge ila cha ajabu ni kuwa rushwa inaendelea kutoka kwa makatibu kata hadi IKULU, na kutoka mashirika binafsi hadi kwenye miradi ya kifamilia. yani kwa kifupi kila mtu ni mla rushwa na fisadi (in a broad sense) kwa nafasi yake.

  mfano kwenye kanchi ketu leo uki mtuma hata mdogo wako kukununulia kifaa cha gari au ujenzi utasikia akizungumzia(si kwako labda kwa wenzake) CHA JUU! akimaanisha kuwa anachukua gharama ya juu kuliko bei halisi ili na yeye apate ULAJI. au ana bargain na kupata kwa bei ya chini halafu haleti charge na ataandikiwa risiti ya bei zaidi ya pesa aliyotoa kuhalalisha ULAJI!je huu si ufisadi? katabia haka kanaanzia kwenye familia then ndo tunasikia hayo ya RADAR!

  hii ni tabia ya wanafunzi/vijana wetu viongozi wa kesho wakikua una tegemea nini......!!!!!!???????

  ukirudi kwa baba/mama/kaka (wakubwa) zao ambao wako kwenye maofisi mbalimbali yawe ya uma au ya binafsi! ndo balaa tupu put aside kina KARAMAGI,LOWASA etc, turudi kwa watendaji si wale walioleta richmond na IPTL etc, wengine wadogo zaidi ya hao.

  wakichukua pesa za kampuni sijui mnaita IMPREST...?hapa ndo vituko na uppety fisadi ulipo mtu atasema ametumia zote na anadai shirika zitaletwa risiti za uongo sikafanywa kuwa za kweli then pesa tumboni....watumishi waserikali semeni kama nawasingizia......!!!!!!!!je sikweli umelala hotel ya bei pungufu alafu unaleta risiti ya five star??? hii sio serikalini pekeyake hata mashirika binafsi....kama ni uongo semeni!!

  kwa wale watafiti wengine maprofesa na madaktari mchezo ni huu huu...je ni uongo??? hamletagi risiti za kununua na mnaandika bei za juu kuliko matumizi halisi???huu nao ni ufisadi...kama ni halali ndo napenda kusikia

  kwa wenye makampuni binafsi je unalipa kodi halali?? nimefanya uchunguzi(mdogo) nikagundua kuwa watu wana shusha kwa makusudi mapato yao ili kukwepa kodi je huu si ufisadi????toka umeanza kukwepa kodi unafikiri hujaiba sawa na kina RA,EL,NK,PATEL, etc???

  yani kwa kifupi THIS IS THE COUNTRY OF FISADZ; BIG(senior public servants,politicians and big business men),MEDIUM (those junior public servants and entreprenuers)SMALL (young boyz and girls wanaokula cha juu wakitumwa), and PROSPECTIVE FISADZ (those young kids in primary school waiting to be able to be sent to purchase a bit complicated item ili aweke cha juu)


  JITAFAKARI WEWE UPO WAPI KABLA YA KUNYOOSHEA WENGINE VIDOLE.........

  Nawasilisha.
  HS

  MUNGU IBARIKI TANZANIA
   
 2. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #2
  Oct 2, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Mzee naona umepiga "ikulu" ndio maana watu haawachangia kwenye topic yako. Hayo uliyosema ni ya kweli kabisa. Nchi hii imezidiwa sana na mmomonyoko wa maadili kiasi kwamba, hata mambo yayolikuwa ya ajabu siku hizi yanaonekana ni ya kawaida tu. Hata traffic police akikamata basi lililozidisha abiria, utawasikia abiria wakiongea kwamba dereva na kondakta wafanye haraka kumpa rushwa ili safari iendelee.

  Mara tunasikia maofisa wa NECTA wanauliza vyeti original kwa watu ambao hawakuliona darasa, ama walisoma ila wakafeli vibaya! Tunaona jinsi jamii inavyoo ona kwamba ni jambo la kawaida kwa mwanafunzi aliyefeli kidato cha nne au cha sita kwenda kwenye chuo cha ualimu. Yaani kazi ya ualimu kwa sasa ni ya wale waliofeli. Sasa watawafundisha nini wanafunzi wakati masomo hayo hayo wao walifeli?

  Badala ya kuboresha masilahi ya walimu ili kuvutia wanafunzi waliofaulu kuwa walimu, tunashuhudia walimu ambao wana miezi 7 hawajalipwa mishahara. Nakumbuka niliwahi kukaa sakafuni miaka ya themanini wakati naanza darasa la kwanza, na mpaka leo wanafunzi bado wanakaa chini! Hivi tunahitaji mbao na pesa toka nje ya nchi ili kutengeneza madawati??? Mkapa alikuwa sahihi aliposema Watanzania ni wavivu wa kifikiri! Kutoweza kutatua matatizo yanayoweza kutatulika kirahisi ndani ya jamii zetu nao pia ni ufisadi.

  Nchi hii inakatisha tamaa sana!
   
 3. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #3
  Oct 2, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Umepigilia msumari wa ukweli, nakubaliana na maandishi yako kwa asilimia 100. Kwa Watanzania ninaowajua mimi, ambao sio wala rushwa au wababaishaji, haizidi asilimia tano. Wengine wote labda tunapiga kelele kwasababu tu hatujapewa nafasi ya kubugia huo ULAJI.

  Hii vita inatakiwa ianzie nyumbani kwetu, hapo tutakuwa na nafasi ya kushinda, vinginevyo utakuwa wimbo tu wa kisiasa.
   
 4. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #4
  Oct 2, 2008
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Hii maada haitaenda mbali

  Wewe ungesema CCM wamefisadi hata madawati pale temeke ungeona moto wake hapa.Tatizo mkuu wanaopiga kelele kwa mafisadi wengi wao wanazitaka hizo nafasi ili wafisadi zaidi maana nafasi walizonazo haziwapi mwanya mzuri wa kufisadi.
   
 5. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #5
  Oct 2, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Usione vyaelea vimeundwa. Watanzania wa leo wamejengwa kuwa hivyo walivyo, hawakudondoka kutoka juu
   
 6. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #6
  Oct 2, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Wa-Tanzania kama nchi zingine, tupo waadilifu na pia tupo mafisadi hilo ni kwa kila taifa, ufisadi ni tabia ya kuzaliwa zaidi kuliko kujifunza, maana ona Lowassa, Mwalimu alisema jamaa ni fisadi sasa ungetegemea angejirekebisha lakini wapi hata sasa yuko nje lakini bado tu!
   
 7. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #7
  Oct 2, 2008
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Na
  Tatizo letu mimi nionavyo ni kwamba hatupigii kelele mafisadi ili tukomeshe ufisadi ILA tunachofanya ni kupigia kelele mafisadi walioshiba na tuiingize mafisadi wengine wenye njaa.
   
 8. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #8
  Oct 2, 2008
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Naona mtizamo wenu na mtoa mada kidogo siafikiani nao. Suala la msingi sio kuwa kila mtu anadai cha juu, iwe kigezo cha watu kuziba masikio yao juu ya ufisadi. Tatizo la ufisadi Tanzania ni suala la mfumo, na hii iko kama mtiririko wa joto au nishati ndani ya wiya au chuma. Kuwa ukiweka umeme sehemu moja, basi sehemu ya pili hata kama urefu ni km 20, mara moja charge inakuwepo.

  Watu wanatakiwa wapige kelele na kukemea hili ili huko charge zilikoanzia zikatike.
  Haiwezekani watawala wawe wala rushwa halafu utegemee wafanyakazi na wahudumu wa kawaida wasidai "cha juu". Kama makamanda wa polisi wangekuwa hawadai mgao wao, basi na mapolisi wa barabarani nao wangepunguza. Kadhalika Mawaziri, makatibu wakuu n.k. Kwa maana hiyo suala la msingi hapa ni nani mwanzisha mwendo. Ukitaka kumuua nyoka tafuta kichwa kiliko na wala sio mkia.

  Chukua mfano mwingine rahisi, kupambana na biashara ya madawa ya kulevya haihitaji kupambana na vijana wanaotembeza tembe mitaani au watumiaji, hapa tunatakiwa kupambana na wanoyaingiza nchini. Naomba tubadili mwelekeo
   
 9. H

  Humble Servant Member

  #9
  Oct 2, 2008
  Joined: Aug 2, 2007
  Messages: 87
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mkuu naomba kutofautiana na wewe, mimi siamini kabisa kuwa kuna watu wanazaliwa mafisadi!ufisadi ni swala analojengewa mtu na jamii yake (environmental/social determinism) ukizaliwa kwenye jamii ambayo watu wanaona rushwa na wizi ni halali, uwezekanao wa kupata wezi wengi ni mkubwa vivyo hivyo ukizaliwa kwenye jamii ya watu wasiopenda rushwa na dhuluma uwezekano ni kuwa wadhulumaji watakuwa wachache maana it will be socially unacceptable!

  ndo maana kwa kesi yetu sisi watanzania tunawachukia kina EL,RA etc sio kwasababu ni wala rushwa/fisadz bali kwa sababu hatujapata nafasi hizo!!!!!!matendo yetu katika imprest na cha juu yana shuhudia hilo!!!!!!

  tukipata tutaziendeleza kuleta RICHMOND kubwa na Ma IPTL watu hawapati ujasiri wa kufanya dhambi hizi kwa siku moja ni tabia inajijenga kuanzaia kwenye kuforge risiti na vocha ndo baadae ujasiri una kuwa na kufika huko!!
   
 10. H

  Humble Servant Member

  #10
  Oct 2, 2008
  Joined: Aug 2, 2007
  Messages: 87
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  hilo sio lengo letu hata kidogo ufisadi lazoma ulaaniwe kwa nguvu zote na ndio maana leo na elekeza MKUKI kwetu.........isije ikawa MKUKI KWA NGURUWE.......kwa BINADAMU MCHUNGU.........

  wakati tukiwaonyesha vidole wengine kuwa ni wachafu na sisi tunajitakasa vipi...????

  [/QUOTE]Tatizo la ufisadi Tanzania ni suala la mfumo, na hii iko kama mtiririko wa joto au nishati ndani ya wiya au chuma. Kuwa ukiweka umeme sehemu moja, basi sehemu ya pili hata kama urefu ni km 20, mara moja charge inakuwepo.Watu wanatakiwa wapige kelele na kukemea hili ili huko charge zilikoanzia zikatike[/QUOTE]

  hili ni kweli ndo maana nataka tuanzie kukata charge tunazo peleka sisi then ndo tuweze kuinsulate zile za wengine....


  [/QUOTE]Haiwezekani watawala wawe wala rushwa halafu utegemee wafanyakazi na wahudumu wa kawaida wasidai "cha juu". [/QUOTE]


  ..........je ni halali na busara kila mtu kuwa mla rushwa just because viongozi wana kula???? this is very wrong na halihitaji maelezo kulikataa.


  [/QUOTE]Kama makamanda wa polisi wangekuwa hawadai mgao wao, basi na mapolisi wa barabarani nao wangepunguza. Kadhalika Mawaziri, makatibu wakuu n.k. [/QUOTE]hawa wana sababu.......je wewe unae forge risiti unadaiwa mgao na nani!!!!je unampelekea bosi wako mgao akisha idhinisha malipo???hili halitokei sana
  [/QUOTE] Kwa maana hiyo suala la msingi hapa ni nani mwanzisha mwendo. Ukitaka kumuua nyoka tafuta kichwa kiliko na wala sio mkia.[/QUOTE]

  hili ni kweli ndo tunataka kujua mzizi ulopo tuukate maana tukiwapigia kelele waliopo tukaacha mfumo ujilee toka ndani ya familia zetu hakika itakuwa ni kazi bure na hatutafanikiwa kupunguza rushwa na ufisadi kamwe....itakuwa kudai kutoa fisadi mwingine na kumweka mwingine pengine mwenye njaa zaidi

  [/QUOTE]Chukua mfano mwingine rahisi, kupambana na biashara ya madawa ya kulevya haihitaji kupambana na vijana wanaotembeza tembe mitaani au watumiaji, hapa tunatakiwa kupambana na wanoyaingiza nchini. Naomba tubadili mwelekeo[/QUOTE]


  we are many times wrong ndo maana mada kama hii ipo mezani kutafuta mzizi walio tokea kina EL,RA, NK, etc

  si dhambi kutofautiana mawazo hayo ni yangu, tusikie ya kwenu!!!!!!!!
   
 11. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #11
  Oct 2, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Mkuu maneno yako ni kweli, lakini tumefikia mahali sasa Tanzania inasikitisha, lakini ni kwa sababu tunaongozwa na mafisadi waliokubuhu, katika maisha yangu machache niliyoishi Tanzania nime shuhudia tabia za viongozi wengi ambao ni wasafi na pia viongozi ambao ni wezi tu hata ufanye nini,

  Ninamjuua kiongozi mmoja ambaye wizi ulikuwa kwenye damu yake, kwamba siku moja alikuwa anahama kutoka nyumba moja ya serikali kwenda nyingine mkulu alichukua mpaka balbu, sasa hata huyu mkulu alipoewa nafasi kubwa zaidi wale waliokuwa wakifanya naye kazi walishangaa sana maana wote walikuwa wanamjua kwua ni mwizi, haikuchukua hata mwaka kule alipohamishiwa kwenye uwaziri, akabambwa na kulazimishwa kujiuzulu,

  Hawa wa namna hii wako wengi sana kwenye serikali yetu, kuna waziri mmoja yeye tabia yake ni kuiba kwenye ma-super market hasa akiwa nje, siku moja serikali ikaletwa film ya mkulu akikawapua huko majuu, na mpaka leo mkulu ni fisadi haijawahi kutokea, ninakumbuka wakati flani hata waziri Diria ilibidi asachiwe Airport na wazungu kwa sababu ya ufisadi, sawa ninakubali maneno yako lakini mkuu please Tanzania tuna badhi ya viongozi wasio mafisadi, ingawa ni wachache sana,

  Ni kweli kuna ambao ni mafisadi kutokana na mazingara, hao ni wengi sana sio siri infact hata wananchi pia ni wengi sana kwenye huu mkumbo, lakini hata mazingara ya America, ambako huna sababu ya kuwa fisadi si bado wapo mafisadi, kuna watu huzaliwa na ufisadi kwenye damu na miongoni mwao ni viongozi wetu!
   
 12. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #12
  Oct 3, 2008
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280

  Mkuu
  Huyo waziri ni mgonjwa kuna magonjwa ya aina nyingi sana hapa duniani.
  Mtu kama huyo akikosa cha kuiba anaweza kuweka sharti lake mahala akalinyatia harafu akalikwapua akaridhika kua siku imekamilika,Ni mgonjwa huyo.

  Magonjwa yapo mengi ambayo ni ukichaa ukiwa na digrii tofauti tofauti ,Mfano ukichaa wa wizi, ukichaa wa ulalamishi,ukichaa wa ubishi,ukichaa wa kupenda mapenzi,ukichaa wa kujisaidia pembeni kwa choo yani mwingi tu.

  mimi nafikiri FISADI ni yule si kichaa wa wizi lakini anafanya wizi makusudi.Mtu anayeiba hadi kwenye supemarketi sio FISADI ni Mgonjwa
  Unless kama ni daywaka.
   
 13. H

  Humble Servant Member

  #13
  Oct 3, 2008
  Joined: Aug 2, 2007
  Messages: 87
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
   
 14. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #14
  Oct 3, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Tuko pamoja hapo mkuu.
   
 15. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #15
  Oct 3, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  1.
  Unajua nijuavyo ni kwamba kuna viongozi ambao ninaamini walikuwa ni wasafi kwa standard zetu za kibongo, nilishwahi kutoa list huko nyuma wametoka uongozi wakiwa ni watu wa kawaida, na hawakukutwa na kashfa za wizi, hata mara moja I mean ni kufuata tu standard zetu za kibongo ninaamini unanielewa hapo.

  Na unajua siku hizi ninapokuatana na viongozi wa sasa na wa zamani, huwa ninawahimiza sana kuhusu wao kuandika vitabu kuhusu experience zao za uongozi, maana wengine huenda wanasingiziwa kashfa walizonazo wanaweza kujisaidia sana na kumbu kumbu vitabuni, kwa mfano siku moja nilikuwa ninaongea na Mzee Rupia, akaniambia kuwa amewahi ksuoma Masters NYU, NY-US, tena in the 60s, that was a shock to me, sisi tumezoea kusikia akihusishwa na ufisadi tu and I told him that kwamba why don't you set the record straight through a memoir, akasema atafikiria sana.

  2.
  Lakini hatuwezi kukwepa ukweli na facts of life, nimeiskia sana pint yako ikiwa raised hapa JF kwenye mijadala mingi, lakini ukweli unabaki pale pale kwamba Tanzania kama nchi zingine masikini za dunia tunajaribu sana kuwaiga hao wakuu wa dunia, lakini you have a point hapo, ingawa nia yangu haikua kuhalalisha ufisadi mdogo kwa kuitumia US, isipokua kusisitiza hoja kuwa kuna baadhi ya mafisadi huwa ni wagonjwa na uko kwenye damu, yaani ufisadi!

  3.
  Hapa umepiga msumari unapotakiwa, unajua hii tabia siku hzizi bongo imehalalishwa imekua ni kama sheria, inasikitisha sana.
   
 16. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #16
  Oct 3, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Bila shaka watetea mfumo watakurupuka na kukuunga mkono lakini mimi mmh!
  Kilichojificha hapa ni kuwa ama unatetea uongozi wa nchi kwa kushindwa kuongoza vita dhidi ya UFISADI au umeathirika na virusi vyake kiasi kwamba huwezi tena kufurukuta. Vyovyote vile hii ni tabia ya kubwaga manyanga na ni hatari kwa nchi kama hii yetu maanake unataka kutuaminisha kwamba sasa it is our way of life and so is acceptable.

  Al Haj Idi Amin Dada wa Uganda pamoja na mapungufu yake yote anakumbukwa kwa kufanikisha kitu kimoja humo nchini. Aliweza kutokomeza mfumo wa hatari ulioanza kushika kasi na ambao ulikuwa hatari kwa taifa hilo. Huo mfumo uliitwa "kondoism" na kwa tafsiri ya juu juu ni unyang'anyi wa kutumia silaha za moto ukiambatana mauaji. Walioendesha jambo hili ilikuwa kama vile wako juu ya sheria na pole pole walianza kuheshimika kwenye jamii pamoja na mambo yao ya kikatili.

  Field Marshall aliagiza jeshi lake na polisi kutokupoteza muda kwa kuwapeleka mahakamani hawa washenzi na wakipatikana dawa yao ilikuwa iwe moja tu kuwatwanga risasi palepale wakikamatwa - hakuwa na ubia nao, period. Mwanzoni ilionekana kama ni kwenda kinyume cha sheria lakini baada ya muda mfupi tu matunda ya operation hiyo yalionekana hata kwa kipofu na watu waliweza kuishi bila hiyo hofu.

  Kwa waliosoma historia hakuna nchi iliyotawaliwa na UFISADI (rushwa) kama China. Vita ilipotangazwa dhidi ya mafisadi, adhabu ya watuhumiwa ilikuwa ni kuwatwanga risasi hadharani huku ndugu, jamaa na marafiki wakishuhudia na haikuchukua muda hali ilibadilika na fikra kwa ujumla nao ukabadilika. Sisemi ufisadi uliweza kutokomezwa kabisa lakini kwa kiwango kikubwa na ole wako ukamatwe.

  UFISADI Tanzania unapandwa, unamwagiliwa, unapaliliwa, unastawi na unapokomaa unavunwa kwa kasi, ari na nguvu za ajabu. Serikali yetu ina ubia na mafisadi - sasa nani anayetaka kuheshimika katika hiyo jamii hatataka kuwa FISADI tena wa nguvu. Tumejijengea mfumo unaopakata ufisadi sasa nini cha ajabu kama wengi wanajikuta kwenye huo msafara na wanaupa kipaumbele ?

  Mtu yeyote anayediriki kumtetea Mkapa, mtu yeyote ambaye haoni mapungufu ya huu uongozi na mtu yeyote anayethubutu kubeza sauti za hao wachache wanaojituma kukemea huu uchafu, atakurupuka na kuunga mkono hoja hii maana keshaathirika. Ndiyo nakubali Tanzania waathirika ni wengi tena kwa kiwango cha kutisha lakini si wote.

  Swali ni nani huyo amesababisha yote haya mpaka tukafikia tulipo. Jibu ni rahisi lakini kwa ulafi wetu wa kutaka vya bure, si wengi wetu tutaliona hilo. Sana sana tutazidi kudumaza mawazo yoyote ya kujikomboa kwa kutoa mada kama hii hapa inayowatuhumu wananchi kwa ujumla wao. Kuna siku watasema NO WAY na hiyo siku haiko mbali.
   
 17. H

  Humble Servant Member

  #17
  Oct 3, 2008
  Joined: Aug 2, 2007
  Messages: 87
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  mkuu nashukuru kwa`mchango wako,
  ila naomba kukuhakikshia kuwa sikuanzisha mjadala huu kwa lengo la kutetea mtu yeyote yule......kama unavyosikia sijui EL anasafishwa etc. hilo si lengo langu kabisa....... lengo langu ni kuanzisha mjadala wa kujitafakari sisi kama whistle blowers je tu wasafi kiasi gani???

  usije kukuta tunapigia kelele dhambi ambazo na sisi tunazitenda. kwa sababu tu hatuna nafasi hizo, maana kelele hizi zitakuwa za bure na kamwe lengo letu la kushinda vita hii halitafikiwa!!!maana nani atawarithi hao mafisadi kama wengi wet tukiwa tunaufanya ufisadi kulingana na nafasi zetu???

  hivyo mjadala huu utatufanya tutafakari usafi wa jamii yetu kwa ujumla wake wote na ikibidi tuanze kubadilika tabia kama watu binafsi na hatimae kama taifa! tuache wote dhambi!!

  kwenye la pili nakubaliana na wewe ulafi ndio tatizo, lakini sasa kama tukiwa na wapiga kelele kama MTIKILA ambaye nae kumbe yupo kwenye payroll ya mafisad kama RA unategenea tutafanikiwa kweli????ndo maana mada ipo mezani
   
 18. M

  Malila JF-Expert Member

  #18
  Oct 3, 2008
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Wengine ufisadi wetu upo ktk small scale kiasi kwamba madhara/dhuruma yake havionekani moja kwa moja,basi tunadhani sisi si mafisadi.Ukweli ni kwamba wengi tu mafisadi.
   
Loading...