Nchi ya ajabu sana hii: Pamoja na janga la Corona bado Mamlaka zinakata maji

J C

JF-Expert Member
Dec 12, 2013
2,927
2,356
Hivi ninavyoandika mamlaka zanazohusika na maji zinakatia watu maji na hii corona. Jamani, tuweni na utu. Hii inaendelea hapa Mwanza mjini jamaa wanawahi asubuhi kabla hata watu hawajaamka wanakata wanasepa. MWAUWASA Mjitafakari, jambo jema Corona haichagui maskini au tajiri.

Mungu wa mbinguni endelea kutetea wanyonge maana hakuna mwanadamu awezaye kuwatetea kipindi hiki hasa katika nchi yetu Tanzania ambapo mnyonge ameachwa apambane na hali yake mwenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukatili si MWAUWASA bali ni wa mwenyekiti wa kijiji. Kwani Mwenyekiti akiamua jambo MWAUWASA au TRA watafanya nini? Jibu atakalokujibu " Kachote maji bure ziwani"
 
kwa nini usishangae Kenya wanaolazimisha watu kukaa ndani halafu wanawavunjia nyumba
Kwa hiyo kwa sababu Kenya watu wanavunjiwa nyumba, inawapa uhalali mamlaka za maji Tanzania kuwakatia watu maji wakati huu ambapo ilitakiwa hata kutoa discount ikizingatiwa kuwa maji yanafacilitate usafi yaani kujikinga dhidi ya corona? Wakati mwingine muwe mnatumia akili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nchi hii ni ya ajabu sana; wakati nchi nyingine zimawafutia wananchi wake bili za maji ili waweze kunawa kujikinga na corona, wao wanawakatia wananchi wao maji!!! Huu ni upuuzi wa serikali wa hali ya juu sana. Msiombe uongozi kama mnajua hamna uwezo wa kuwahudumia vizuri wenye nchi.

Nilitegemea wakati huu serikali ingekuwa imetoa moratorium ya angalau ya miezi mitatu wananchi wa hali ya chini wasilipe bili za maji. Hiyo ingeonesha kuwa serikali inawajali watu wake.
 
  • Thanks
Reactions: J C
Back
Top Bottom