dubu
JF-Expert Member
- Oct 18, 2011
- 3,500
- 3,481
Jumuiya ya Afrika Mashariki imezitaka nchi wanachama kuiga mfumo wa utatuzi wa migogoro unaotumiwa na Serikali ya Tanzania wa kutumia nguvu kubwa ya ushawishi,na mazungumzo kuondoa chochoko zinazoweza kusababisha umwagaji wa damu usio wa lazima badala ya kusubiri kutumia nguvu hizo madhara yakishatokea.
Changamoto hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Dr. Richard Sezbera alipokuwa akizungumza na makundi mbalimbali ya wananchi na watendaji waliojitoka kuwakumbuka mamilioni ya wananchi waliopoteza maisha katika mauaji ya Kimbari ya Rwanda mwaka 1994 .
Wakizungumza baada ya kumalizika kwa hafla hiyo washiriki kutoka nchi mbalimbali wakiwemo walionusurika kwenye mauaji hayo ya Kimbari na mengine yanayosababishwa na masuala ya kisiasa katika nchi zao ambao walifanya maandamano na kuweka mashada ya maua katika mnara ulioko kwenye makao makuu ya jumuiya hiyo wameishukuru Tanzania kwa kuwa kuwa jirani mwema na kimbilio la wote wenye shida.
Kwa upande wake mwakilishi wa Serikali ya Tanzania katika hafla hiyo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Bw.wilson Nkambaku amesema lengo la Tanzania ni kuona wananchi wa nchi zote wanaishi kwa amani kwamba kazi kubwa inayofanyika sasa ni kuwaelimisha wananchi kutokubalikutumiwa na baadhi ya watu wanaotafuta maslahi yao kuuana wenyewe kwa wenyewe.
Chanzo: ITV