#COVID19 Nchi tajiri zakosolewa vikali kwa kutoa chanjo za ziada wakati hali ikiwa mbaya Afrika

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Mkurugenzi wa shirika la afya Duniani kanda ya Afrika amezikosoa vikali nchi tajiri kwa kutoa chanjo ya tatu kwa watu ambao tayari wameshapatiwa chanjo hizo dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona.

Mkurugenzi huyo Matshidiso Moeti amewaambia waandishi habari kwamba uamuzi wa nchi hizo unatishia mustakabali wa nchi za Afrika. Amesema kutokana na nchi tajiri kuhodhi chanjo swala la usawa wa chanjo linakuwa ni mzaha.

Amesema hali bado ni tete barani Afrika wakati ambapo maambukizi ya virusi vya aina ya Delta yanakuja juu katika nchi 54 za bara hilo. Mpaka sasa ni chini ya asilimia 2 ya watu bilioni 1.3 wa Afrika waliopatiwa chanjo.

Watu zaidi ya milioni 7.3 wameambukizwa virusi vya corona barani Afrika kote na 186,000 wamekufa kutokana na ugonjwa wa COVID-19.
 
"Afrika hali ni nzuri na hawahitaji chanjo." Hiyo ni kauli ya hawa jamaa hapa:

IMG_20210820_061852_470.jpg

Kwenye kundi hilo yamo Niza doyi Lorenzo Samike Mathanzua na mienzao ya namna hiyo.

Beberu chanja watu wako, wacha huku waendelee kwanza kuruka ruka na kukanyagana.

IMG_20210718_063455_991.jpg

Tuko vizuri.
 
Lakini Waaafrika jamani, kha! Huu sasa ni ubabe.Inanikumbusha makala za wanyamapori hasa nikimuona fisi analazimisha kupora mzoga toka kwa chui au simba.
 
walisema mpaka sasa tungekuwa tunaokota mizoga barabarani. La msingi tumia chanjo aliyotumia waziri na mme wake kwenye blanketi kipindi cha Magu.
 
Wakati wenzetu wanafanya research kuhusu chanjo, CDC Africa naamini ilikua haijafungwa. Ilikua inaoperate
 
Mkurugenzi wa shirika la afya Duniani kanda ya Afrika amezikosoa vikali nchi tajiri kwa kutoa chanjo ya tatu kwa watu ambao tayari wameshapatiwa chanjo hizo dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona.

Mkurugenzi huyo Matshidiso Moeti amewaambia waandishi habari kwamba uamuzi wa nchi hizo unatishia mustakabali wa nchi za Afrika. Amesema kutokana na nchi tajiri kuhodhi chanjo swala la usawa wa chanjo linakuwa ni mzaha.

Amesema hali bado ni tete barani Afrika wakati ambapo maambukizi ya virusi vya aina ya Delta yanakuja juu katika nchi 54 za bara hilo. Mpaka sasa ni chini ya asilimia 2 ya watu bilioni 1.3 wa Afrika waliopatiwa chanjo.

Watu zaidi ya milioni 7.3 wameambukizwa virusi vya corona barani Afrika kote na 186,000 wamekufa kutokana na ugonjwa wa COVID-19.
Hacha wapeane hizo chanjo sisi hatuitaji wao wataishi milele hapa chini ya jua
 
Back
Top Bottom