Nchi nzima kugeuka sehemu za kuchungia mifugo, hili halifanani na karne hii

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,489
13,608
Jana taarifa ya habari ya ITV imeonyesha hasara waliyopata wamiliki wa shamba la miwa huko Mtibwa. Kwa mujibu wa aliyehojiwa ambaye inaonekana ni msimamizi wa shamba hilo, hasara waliyopata ni ya shilingi milioni 800.

Wingi wa miwa ambayo ingevunwa na kuingizwa kwenye mchakato wa upatikanaji wa sukari, kwa namna moja au nyingine ungesababisha kushuka kwa bei ya bidhaa hiyo muhimu.

Hapa tunaongelea hasara waliyopata Mtibwa, hatujaongelea mateso wanayopata wakulima wengine wengi tu wenye kutumia nguvu nyingi katika kulima na kupanda mazao halafu ghafla tu ng'ombe wanaingia na kuharibu kila kitu.

Haipendezi hata kidogo kuona nchi nzima inageuzwa kuwa mali ya wafugaji na mifugo yao. Natambua ukame wa baadhi ya maeneo ya wafugaji. Kwa kukatiza tu na gari pale Monduli mtu anauona ukame halisi, hapo bado haujatembea katika maeneo mengine yenye shida kubwa sana ya maji na nyasi.

Waziri wa kilimo na wasaidizi wako, tunakoelekea kwenye nchi ya viwanda, tunakwenda kwenye maisha ambayo wawekezaji wa ndani ya wa nje hawatakubaliana na hasara zitakazotokana na uholela wa uchungaji ambao umekuwa na mateso makubwa kwa wakulima wasio na hatia.

Lifanyike jambo na lifanyike mapema iwezekanavyo. Leo Mtibwa wanadai kuingia hasara ya milioni 800, kesho atakuja muwekezaji na kudai kupata hasara ya mabilioni ya shilingi na hatakubaliana na majibu yoyote ya kutaka kumridhisha ili suala liweze kumalizika kwa amani.
 
Si kilimo tu!
Kuna mfugaji alikamatwa pori la hifadhi la Burigi,aliyemkamata badala ya kupongezwa,akasimamishwa kazi!!.

Wizara ya kilimo inajipangaje kupenyeza mawazo ya kilimo na ufugaji wa kisasa? Nilimsikia Tizeba anasema kwamba kuna wachina wana nyasi za kisasa huko kwao,zinazokua haraka,na kwamba nyasi hizo zikipandwa eneo la ekari moja,ngombe hata mia wanakula na kushiba na kusaza!! Lakini mbona hazileti?

Pili,viwanda vya nyama,vingesaidia sana kupunguza idadi ya mifugo inayozurura hovyo.

Mipango ya matumizi bora ya ardhi hakuna

Hawa wenye mifugo walazimishwe kuwa na namba za mifugo,watake wasitake,ili ukiiacha mifugo yako ilishe hovyo uwajibike.

Mabaraza ya wakulima na wafugaji yaanzishwe kuanzia ngazi ya kijiji,yafanye kazi ya kuwatambua wafugaji wote kijijini,na akija mpya,basi alete barua ya utambulisho na aonyeshe kajiandaa vipi kulilisha kundi la mifugo analozurura nalo

Kimsingi,ni kuwekeza kwenye maarifa zaidi.

Hata wakulima,nao wanaomba kugaiwa maeneo ya hifadhi,hata uwape maeneo yote ya hifadhi za nchi,bado wataendelea kulia,tatizo ni ninj? Twende kwenye intensive farming,kilimo cha kisasa ambacho hekari tano zitakufanya uvune kama mwenye ekari 20
 
Serikali ya Hapa Kazi Tu isipolichukulia hatua suala hili, watakuwa kichekesho.

Haiwezekani watu fulani tu toka sehemu zile zile wakaranda randa nchi nzima kutafuta malisho.

Huku nyuma wameiharibu kabisa ardhi yao.
Inabidi kule walikotoka wairejeshe ardhi waliyoiharibu tunaishi kama tuko middle ages!
 
mifugo yenye thamani ya mamia ya matrilioni inazurura tu,watanzania wanavaa yeboyebo za plastiki wakati raslimali ya ngozi ipo

watanzania wanatembea wamevaa ndala za bata ambazo ni plastiki,ngozi zipo.

makumi ya mamilioni ya ngombe,hakuna kiwanda cha maziwa.

wizara ya ardhi ilitakiwa iwe na kanda maalum ambazo ingeunda kwa kushirikiana na wizara nyingine,kama polisi walivyofanikiwa Tarime na Dar

yale maeneo korofi yaundie kanda maalum,yapelekee fedha na wataalam,yape deadline yaandae mipango bora ya matumizi ya ardhi,wakati huo huo maafisa kilimo wanaingia huko na kupeleka nyasi bora,elimu n.k,huko umasaini,morogoro,manyara,mbeya na kwingineko
 
mfano mzuri ni shinyanga,simiyu,na baadhi ya maeneo ya mwanza.

Huwa namshangaa ndugu yangu luhaga mpina anapotembela madampo na mifereji ya viwanda.

Kuna maeneo yanahitaji mkakati maalum kabla hayajawa jangwa,mojawapo ni kanda ya ziwa.

inahitaji programu maalum ya miaka hata kumi kila familia iwe na miti isiyopungua mitano,na ikibidi ziwepo by laws kulazimisha mipaka ya mashamba ipandwe miti,kama shamba lina pembe nne,huwezi kukosamiti nane

Hapa unaua ndege wawili,unaepusha migogoro ya ardhi kuhusu mipaka,mbili unaokoa mazingira
 
Viwanda vitapatikana kwa jasho sana kama ng'Ombe mbuzi na kondoo hazita fungwa kamba zisihujumu mashamba yetu na chanzo cha rasilimali viwanda.

Mfano wilaya ya kilosa yenye kila aina ya agricultural potentials pamegeuzwa makao makuu ya ng'Ombe tanzania. Ng'Ombe wanatamani wafakamie hadi katani
 
Serikali haina budi kupitia upya sera na sheria zinazoruhusu watu kuhama hama hovyo na mifugo yao!!Haiwezekani na haikubaliki kabisa watu hao hao wakawa kero kwa nchi nzima!!

Kama mifugo yao haiwezi kuchungika katika maeneo yao kwa sababu ya ukosefu wa malisho walazimishwe kuipunguza!!
 
Serikali ya Hapa Kazi Tu isipolichukulia hatua suala hili, watakuwa kichekesho.

Haiwezekani watu fulani tu toka sehemu zile zile wakaranda randa nchi nzima kutafuta malisho.

Huku nyuma wameiharibu kabisa ardhi yao.
Inabidi kule walikotoka wairejeshe ardhi waliyoiharibu tunaishi kama tuko middle ages!
Unapoongelea nchi ya viwanda lazima uje na scientific approach ya utatuzi wa matatizo. Ardhi kwenye mikoa ya wafugaji bado haijaguswa kiasi cha kuhalalisha kuhamahama kwao.
 
Jana taarifa ya habari ya ITV imeonyesha hasara waliyopata wamiliki wa shamba la miwa huko Mtibwa. Kwa mujibu wa aliyehojiwa ambaye inaonekana ni msimamizi wa shamba hilo, hasara waliyopata ni ya shilingi milioni 800.

Wingi wa miwa ambayo ingevunwa na kuingizwa kwenye mchakato wa upatikanaji wa sukari, kwa namna moja au nyingine ungesababisha kushuka kwa bei ya bidhaa hiyo muhimu.

Hapa tunaongelea hasara waliyopata Mtibwa, hatujaongelea mateso wanayopata wakulima wengine wengi tu wenye kutumia nguvu nyingi katika kulima na kupanda mazao halafu ghafla tu ng'ombe wanaingia na kuharibu kila kitu.

Haipendezi hata kidogo kuona nchi nzima inageuzwa kuwa mali ya wafugaji na mifugo yao. Natambua ukame wa baadhi ya maeneo ya wafugaji. Kwa kukatiza tu na gari pale Monduli mtu anauona ukame halisi, hapo bado haujatembea katika maeneo mengine yenye shida kubwa sana ya maji na nyasi.

Waziri wa kilimo na wasaidizi wako, tunakoelekea kwenye nchi ya viwanda, tunakwenda kwenye maisha ambayo wawekezaji wa ndani ya wa nje hawatakubaliana na hasara zitakazotokana na uholela wa uchungaji ambao umekuwa na mateso makubwa kwa wakulima wasio na hatia.

Lifanyike jambo na lifanyike mapema iwezekanavyo. Leo Mtibwa wanadai kuingia hasara ya milioni 800, kesho atakuja muwekezaji na kudai kupata hasara ya mabilioni ya shilingi na hatakubaliana na majibu yoyote ya kutaka kumridhisha ili suala liweze kumalizika kwa amani.
Unamuandiko mzuri, ila hapo kwenye kushuka bei ya sukari naomba upafanyie masahihisho. Tanzania hii hata ardhi yote ingelima miwa kamwe tusitegemee kushuka kwa bei ya Sukari. Mifano ipo wazi, mpaka naogopa kutonesha kidonda/jeraha wakati bado ni bichi kabisa. Labda tumuulize Waziri mkuu aliishia wapi na "singeli" yake ya sukari, maana naona sasa hivi kaamia kwenye korosho.
 
mifugo yenye thamani ya mamia ya matrilioni inazurura tu,watanzania wanavaa yeboyebo za plastiki wakati raslimali ya ngozi ipo

watanzania wanatembea wamevaa ndala za bata ambazo ni plastiki,ngozi zipo.

makumi ya mamilioni ya ngombe,hakuna kiwanda cha maziwa.

wizara ya ardhi ilitakiwa iwe na kanda maalum ambazo ingeunda kwa kushirikiana na wizara nyingine,kama polisi walivyofanikiwa Tarime na Dar

yale maeneo korofi yaundie kanda maalum,yapelekee fedha na wataalam,yape deadline yaandae mipango bora ya matumizi ya ardhi,wakati huo huo maafisa kilimo wanaingia huko na kupeleka nyasi bora,elimu n.k,huko umasaini,morogoro,manyara,mbeya na kwingineko
Mkuu huko kwenye kuvaa umeenda mbali sana, maana pasipo hata mlo bora, nguvu ya kufanya hizo kazi nayo hamna. We uliza bei ya Nyama kwa kilo ni shilingi ngapi?
Sasa hivyo Viwanda vikishajengwa ndio tujiande kusaga meno haswaa, mpaka tutaikumbuka mitumba.
Migodi ya dhahabu, si tunayo hapa hapa, uliza gram ya gold kwa sasa ni bei gani, alafu kaulizie na nchi jirani gram bei gani.?
 
huwa naisikia wizara ya ardhi inapima na kugawa viwanja vya makazi,biashara,viwanda.

sijawahi kuisikia inagawa mashamba hata kama ni eka tanotano tu.

Hili jukumu wamemuachia nani?
 
Mkuu tatizo kubwa la suala la malisho ya wanyama wa waafugaji ni the disguised population migration , katika form ya kutafuta malisho.
Hili suala ambalo ni implied serikali zote imekuwa ikilifumbia macho.

Mashamba ya wakulima yanatekwa mchana kweupe wakati ardhi ya huko sehemu za Tabora, Shinyanga, Kiteto, Manyara haziwi redistributed, kule wanakotoka wafugaji.
 
Jsamani Suluhisho ni kutaifisha mifugo yote itakakamatwa ikilishwa kwenye mashamba. hawatrudia, tumechokaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.
 
ukiitaifisha unatumia sheria gani?maana hata ardhi ya mtu ukichukua sharti ulipe fidia,ukishataifisha unapeleka wapi?
 
Unamuandiko mzuri, ila hapo kwenye kushuka bei ya sukari naomba upafanyie masahihisho. Tanzania hii hata ardhi yote ingelima miwa kamwe tusitegemee kushuka kwa bei ya Sukari. Mifano ipo wazi, mpaka naogopa kutonesha kidonda/jeraha wakati bado ni bichi kabisa. Labda tumuulize Waziri mkuu aliishia wapi na "singeli" yake ya sukari, maana naona sasa hivi kaamia kwenye korosho.
Mkuu turudi kwenye issue ya wafugaji hiyo "singeli" umeiongelea kwa dharau kuliko kutoka mchango wa kujenga kitu kipya.

Kumbuka Bakhresa anapelekewa umeme ajenge kiwanda cha sukari. Kitu muhimu ni kutokuendelea kuruhusu wafugaji wanachagua leo waingie kwenye shamba la nani na kesho la nani. Wizara husika inao wajibu wa kujua movement za wafugaji na namna za kuhakikisha wanakuwa na maeneo maalum. Sio mifugo yao ishibe kwa hasara za wakulima wanaolima kwenye mazingira magumu.
 
Hii kitu ishakuwa janga-nia yangu sio kulikuza hili tatizo lakini kama halita pata dawa litaifikisha Tanzania mahali pabaya sana. Tayari athari zake zinaonekana. Itabidi serikali ilivalie njuga na sidhani kama linaweza kutatuliwa kirahisi kwani linahusu jinsi maisha (livelihoods), uhai na uchumu wa wachungaji vinavyoingiliana na maisha, uhai na uchumi wa wakulima pamoja na sera zetu za wanyamapori na hifadhi.
 
Jana taarifa ya habari ya ITV imeonyesha hasara waliyopata wamiliki wa shamba la miwa huko Mtibwa. Kwa mujibu wa aliyehojiwa ambaye inaonekana ni msimamizi wa shamba hilo, hasara waliyopata ni ya shilingi milioni 800.

Wingi wa miwa ambayo ingevunwa na kuingizwa kwenye mchakato wa upatikanaji wa sukari, kwa namna moja au nyingine ungesababisha kushuka kwa bei ya bidhaa hiyo muhimu.

Hapa tunaongelea hasara waliyopata Mtibwa, hatujaongelea mateso wanayopata wakulima wengine wengi tu wenye kutumia nguvu nyingi katika kulima na kupanda mazao halafu ghafla tu ng'ombe wanaingia na kuharibu kila kitu.

Haipendezi hata kidogo kuona nchi nzima inageuzwa kuwa mali ya wafugaji na mifugo yao. Natambua ukame wa baadhi ya maeneo ya wafugaji. Kwa kukatiza tu na gari pale Monduli mtu anauona ukame halisi, hapo bado haujatembea katika maeneo mengine yenye shida kubwa sana ya maji na nyasi.

Waziri wa kilimo na wasaidizi wako, tunakoelekea kwenye nchi ya viwanda, tunakwenda kwenye maisha ambayo wawekezaji wa ndani ya wa nje hawatakubaliana na hasara zitakazotokana na uholela wa uchungaji ambao umekuwa na mateso makubwa kwa wakulima wasio na hatia.

Lifanyike jambo na lifanyike mapema iwezekanavyo. Leo Mtibwa wanadai kuingia hasara ya milioni 800, kesho atakuja muwekezaji na kudai kupata hasara ya mabilioni ya shilingi na hatakubaliana na majibu yoyote ya kutaka kumridhisha ili suala liweze kumalizika kwa amani.

Kimsingi hii ishu ya migogoro wa wakulima na wafugaji ni kama serikali imeshashindwa kuitatua kabisa days in, days out.

Most probably, serikali (kwa maana ya viongozi tuliowapa mamlaka ya kuamua) ni sehemu ya tatizo hili kwa maana ya SERA na MIPANGO yao kushindwa kufanya kazi kwa namna yoyote ile!!

Else, watoke na wakanushe hili kama wanaweza, then watueleze tatizo ni nini exactly kama siyo hivi nionavyo mimi!!

Binafsi hata mimi nilipoliona hili tukio kupitia taarifa ya habari ya ITV jana saa 2usiku, nlikuwa very shocked, hata kufikiri kama wafugaji wameweza kuteketeza shamba la kampuni kuuubwa ya sukari ya Mtibwa, itakuwaje kwa wakulima wadogo wadogo wa kilimo cha kujikimu cha ekari moja au nusu eka??

Kiukweli nilishangaa sana hata kujiuliza hawa wafugaji wana jeuri kiasi gani hata washambulie shamba la mazao ya kampuni kiasi cha ekari zaidi ya 300 na kuyateketeza kabisa?

Niliendelea kujiuliza labda hawa watu ni wajinga kiasi ambacho hawakuweza kutambua kuwa miwa ni zao kama yalivyo mazao mengine kama mahindi nk? Kwamba walidhani ni nyasi ndefu za kwenye swamps?

Sina hakika nini kitatokea maana polisi walisema wamewakamata tayari hao ng'ombe 500 walioshambulia hilo shamba pamoja na wamiliki wa hao ng'ombe.

Kwa vyovyote hata kama kila ng'ombe atauzwa kwa TZS 1,000,000 hawawezi kufidia hasara waliyosababisha ya zaidi ya TZS 800,000,000 kwa kampuni ya Sukari ya Mtibwa!!

Na baada ya hapo sijui wakiingia kwa wakulima wengine wadogowadogo wanaweza kuwaumiza kiasi gani tu!!

Kiukweli, serikali has to come up with a permanent solution to this problem before it's too late!
 
Hili jambo hata mimi huwa nalifikiriaga sana. Wenzetu wafugaji wametawanyika nchi nzima, tena mpaka mikoa iliyo mbali sana na asili yao kama Lindi, Mtwara, Ruvuma na Pwani. Kuna hatari nchi nzima kugeuka jangwa baada ya muda fulani. Na mbaya zaidi ni kwamba kule kwao walikotoka wanamiliki maeneo makubwa ya ardhi na wamekuwa wakali sana pale ndugu zao wa kutoka mikoa mingine wanapojaribu kwenda kule ili waweze kupewa ardhi wafanye shughuli zao hasa za kilimo. Tukiwaachia hawa wafugaji kutawanyika hovyo nchi nzima kuna hatari ya wao kumiliki au kuhodhi ardhi yote ya nchi, maana kule walikotoka kwao hawaachii ardhi na huku walipo wanachukua ardhi pia. Tutafakari.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom