Nchi nzima kugeuka sehemu za kuchungia mifugo, hili halifanani na karne hii

wafugaji ktk nchi hii hawana mtetezi. maeneo yao ya asili yote yamefanywa mbuga za wanyama na tumesahau wao ndiyo wamehifadhi wanyama pori kwa karne mpaka leo tumewakuta. wafugaji wamekuwa wakimbizi nchini kwao. tuko tayari kutenga maeneo kwa ajili ua wakimbizi lakini siyo wafugaji. siungi mkono uharibifu wa mazao lakini inawezekana ni kwa sababu hawana mtetezi. usishangae mfugaji toka shinyanga serengeti kumkuta mto ruvuma. it is time we recognised diversity of our activities. mkulima, mfugaji, mwindaji, mrina asali wote ni raia wema ndani ya mama Tanganyika
 
Mi natoka jamii ya wafugaji,ila watu wenye ng'ombe wengi wana kibri sana na wanatia hasira yaani huona wale ng'ombe ndo utajiri mkubwa na wa mwisho na wanaeza fanya chochote bila bugudha!! Ni shida sana kwa kweli!!
 
Umeandika pumber mkuu!
Asante mzee, nilitegemea mawazo yako yazigeuze hizo pumba kuwa na manufaa kwa jamii pana ya nchi hii.

Mkuu haiwezekani Tanzania ya leo yenye watu wanaofikia milioni 50 iendelee na maisha ya kuhamahama kwa wafugaji.

Mkuu viwanda vya nguo na viatu anavyoviongelea mkuu wa nchi hufanikishwa kwa uwepo logistics imara kati ya wafugaji wa mifugo na wenye teknolojia ya uanzishaji wa viwanda.

Mambo mengi inabidi yakae sawa kabla ya nchi kufaidika na uanzishwaji na ukuzwaji wa viwanda.
 
Mkuu aliyetoa tathmini ni mfanyakazi ambaye anashughulika na shamba la Mtibwa, punguza dharau za watoto wa vyuo vikuu mwaka wa kwanza. Punguza sarcasm, haikuongezei heshima kwa watu wanaosoma maandishi yako.
Hii migogoro imeachiwa wananchi kujichukulia maamuzi kwa mob psychology,
Kuchungisha mazao ni kosa kama yalivyo makosa mengine.
Wakosaji wangeshughulikiwa kama sheria inavyoelekeza, basi mpambano wa kudhibiti wenye makosa hayo ungefanikiwa.

Kinachoendelea ni kuwa wachunga ng'ombe wakifanya kosa hilo, wakulima hujimobilize na kwenda ku-retaliate kwa kukatakata mifugo ya wafugaji, badala ya ku report police na mfugaji aliyefanya kosa hilo akamatwe, atiwe korokoroni, anyimwe dhamana, kesi isikilizwe, akikutikana na hatia afungwe miaka ya kutosha ili iwe funzo kwa wafugaji waengine, ama polisi wanachukua mlungula!!! na kuwaacha wakosaji wakipita mitaani huku wakijoki.

WATANZANIA TUSIICHUKIE MIFUGO KWA SABABU YA MAKOSA YA BAADHI YA WAFUGAJI.
 
Back
Top Bottom