Nchi masikini haiwezi kuendelea ikiongozwa kidemokrasia

Nimeisoma. Tunarejea kwenye swali langu la awali. Viongozi kama Jenerali Park tunawapataje Afrika. Usisahau mataifa mengi ya Afrika yameongozwa na Majenerali . Baadhi yao wakajivika hata majoho ya kiraia hadi leo.
Viongozi ni zao la jamii, siku ikifika Tanzania (Afrika kwa ujumla) ambayo tumenyukwa kiuchumi, kisiasa na kijamii wote [hata walio ndani ya Chama Tawala], ndio tutapata viongozi kama Kina Park.
 
Korea ipi unazungumzia hapa!? 😳😳😳 South Korea hujawahi kuwa na dikteta tangu 1948.
Mkuu South Korea imetawaliwa na wanajeshi kuanzia mwaka 1960 hadi mwaka 1987. Na hicho ndicho kipindi imepata maendeleo makubwa kabisa ya kiuchumi. Kabla ya hapo ilikuwa maskini kuliko Ghana. Kuinuka kwake kiuchumi hakujatokea kipindi inaongozwa kidemokrasia.
 
Nimeisoma. Tunarejea kwenye swali langu la awali. Viongozi kama Jenerali Park tunawapataje Afrika. Usisahau mataifa mengi ya Afrika yameongozwa na Majenerali . Baadhi yao wakajivika hata majoho ya kiraia hadi leo.
Africa tumewahi kuwa na strongmen wenye maono makubwa, lakini bahati mbaya wengi walipigwa vita na wakoloni wa zamani. Wengi waliishia kupinduliwa ma kuwekwa vibaraka na madikteta wa hovyo kama Mobutu, Bokassa, Nduli nk. Watu makini kama wakina Sankara hawakudumu.
 
Ili nchi iendelee inahitaji kiongozi mwenye maamuzi magumu na uthubutu. Maamuzi ambayo muda mwingine hayatapendwa na wananchi. Mambo kama haya hayawezekani chini ya demokrasia.

Hata wanaotuhubiria demokrasia kila siku wanajua kuwa haifai pale maamuzi magumu yanapohitajika. Ndiyo maana mataifa yenye nguvu yamejipa kura ya Veto umoja wa mataifa. Na pengine ndiyo maaana wanatuhubiria kila siku tuwe na demokrasia, wakijua kuwa tukiwa na demokrasia tutabaki maskini siku zote.

Demokrasia inabidi kuangaliwa upya
Demokrasia ni mbinu za mabeberu kuendelea kutawala nchi za Africa, ukiangalia kwa makini utagundua hiyo demokrasia wanayoihubiri hawaitekelezi ipasavyo kwenye nchi zao.

Mfano currently Marekani limetoka agizo kwa you tube kufuta video zote zinazopingana na chanjo ya covid, kwa maana hiyo ni kwamba wanakatili uhuru wa watu kutoa maoni yao kuhusu chanjo ya covid, wanataka kulazimisha watu wote waamini kuwa chanjo ni salama, hiyo siyo demokrasia wanayoihubiri kila siku.

Kila nchi ina demokrasia yake, demokrasia ya magharibi ambako asilimia kubwa ni literate haiwezi kuwa sawa na demokrasia ya Afrika ambako bado kuna asilimia kubwa ya watu ni illiterate. Kwenye nchi zetu za kiafrika kuna baadhi ya mambo kiongozi anatakiwa kuwa dictator ili mambo yaende kwa mfano kukomesha rushwa, ufisadi na ujujumu uchumi.

Sent from my itel W6004 using JamiiForums mobile app
 
Ili nchi iendelee inahitaji kiongozi mwenye maamuzi magumu na uthubutu. Maamuzi ambayo muda mwingine hayatapendwa na wananchi. Mambo kama haya hayawezekani chini ya demokrasia.

Hata wanaotuhubiria demokrasia kila siku wanajua kuwa haifai pale maamuzi magumu yanapohitajika. Ndiyo maana mataifa yenye nguvu yamejipa kura ya Veto umoja wa mataifa. Na pengine ndiyo maaana wanatuhubiria kila siku tuwe na demokrasia, wakijua kuwa tukiwa na demokrasia tutabaki maskini siku zote.

Demokrasia inabidi kuangaliwa upya
Watu wa msoga na genge lao hawatakuelewa katika hilo...wacha tuendelee kuogelea kwenye demonsgracias...
 
Kila mtetea uovu hujificha kwenye maendeleo ya China. Lakini hamko tayari kulinganisha nchi zilizoendelea kwa demokrasia v/s zisizo na demokrasia.
Hakuna nchi maskini imewahi endelea kwa kufuata demokrasia.
 
Kila mtetea uovu hujificha kwenye maendeleo ya China. Lakini hamko tayari kulinganisha nchi zilizoendelea kwa demokrasia v/s zisizo na demokrasia.
Tupe mfano wa nchi iliyoendelea kwa Demokrasia hii ya Kiliberali unayoisema.
 
CONCLUSION.

democrasia ililetwa na western countries ili waweze kututawala indirect ( tufauti na direct colonialism ).

Angalia, mambo mengi yakiafrika na baadhi ya third world countries yanavyoingiliwa kwa kigezo cha democracy.

Mfano ..ujengaji wa bwawa la Rufiji linalojengwa for now walileta pingamizi kwamba lina haribu environment !!! (qn. Walitaka tujenge wapi na wakati rufiji basin or plateu ndo sehemu yenye enough water to fit production of high mg ......

*kila nchi iliyo huru iwe na uhuru wa kufanya mambo yake bila kuingiliwa ............

* kwani wao walivyokuwa wanafurukuta kuendelea nani aliyekuwa akiwapangia cha kufanya ama kuingiliwa ????
 
Demokrasia inabidi kuangaliwa upya
Mama Samia Suluhu Hassan, rais wetu mpendwa wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, ameisha sema. Demokrasia siyo sawa na radha ya coca cola kuwa radha ya soda ya coca cola mjini Detroit, ni sawa na kule Kanyakumar, Pune, Tora bora, Otto strabbe, Bavaria, Chechnya, Kimasichana, Omurutunguru, Kilema, Siha, Oldonyo Sambu Kericho, Beijing, Lima, Maracana, zitaje tu sehemu unazozijua!

Kwa hiyo, mleta mada naomba umuelewe Mama yetu mpendwa.
 
Mpaka leo Tanzania hatuwezi hata kujenga barabara zetu wenyewe tunalipa billions makampuni ya nje yatujengee, bado tunaagiza Ngano,mchele, mafuta ya kula etc huku ardhi ya kulima tunayo , kwa hiyo tukiacha kupiga kura kuchagua viongozi wetu kwa haki, kuwa na mahakama za haki, uhuru wa vyombo vya habari etc ndio tutaweza? kwa hiyo ili tuendelee tunahitaji jitu moja la kutuburuza na kutuweka ndani na kufungia vyombo vya habari ili tuendelee? mleta mada una agenda mbaya sana au ndio akili ya CCM
 
Hizo unazoziita 3rd world , kwanza tujitahidi kuzifikia, sisi tuko 100th world country

Ni nchi za kawaida sana they arenot countries you can aim to reach! yaaani ni kama mwaka mmoja tu nchi ikiwa serious inaruka that stage
 
Katufute GDP per capita zake na hizo nchi za madikteta kama Misri na Morocco.

sasa egypt si nchi ya tatu afrika inaenda ya pili kwa GDP! hakuna nchi yenye demokrasia iko kwenye izo level, kenya yenyewe wanafululiza kuchukua mahindi tanzania, una kingine mkuu?
 
Back
Top Bottom