Nchi masikini haiwezi kuendelea ikiongozwa kidemokrasia

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,658
20,887
Ili nchi iendelee inahitaji kiongozi mwenye maamuzi magumu na uthubutu. Maamuzi ambayo muda mwingine hayatapendwa na wananchi. Mambo kama haya hayawezekani chini ya demokrasia.

Hata wanaotuhubiria demokrasia kila siku wanajua kuwa haifai pale maamuzi magumu yanapohitajika. Ndiyo maana mataifa yenye nguvu yamejipa kura ya Veto umoja wa mataifa. Na pengine ndiyo maaana wanatuhubiria kila siku tuwe na demokrasia, wakijua kuwa tukiwa na demokrasia tutabaki maskini siku zote.

Demokrasia inabidi kuangaliwa upya
 
Mkuu samahani nini maana ya demokrasia? Upi msingi wa uwepo wa demokrasia? Na Ni kivipi nchi haiwezi endelea kwa kufuata demokrasia? Na nchi itapata vipi maendeleo isipo kuwa na demokrasia?

Kipindi Cha mfumo wa chama kimoja nchi ilipiga hatua kiasi gani ? Maana kulikuwa hakuna mfumo wa vyama vingi Mpaka 1992.
 
Ili nchi iendelee inahitaji kiongozi mwenye maamuzi magumu na uthubutu. Maamuzi ambayo muda mwingine hayatapendwa na wananchi. Mambo kama haya hayawezekani chini ya demokrasia...
Uwezo wako wa kufikiri ni mkubwa na wangi wanauwezo mdogo wa kufikiri kwa sababu ukitaja tu democrasia mtu anawaza kachama kake.

Nakushauri usichoke hata watu wawili au watatu wakielewe umelisaidia taifa
 
Wadada wa kazi mna maneno. Udikteta tangu lini ukawa mzuri? Enzi za nduli Idd ulikuwepo wewe, dikteta Mobutu aliiletea DRC maendeleo gani?

Dikteta wa nchi tajiri sana E. Guinea amefanya Nini E. G zaidi ya kuweka hela zote za nchi kwenye akaunti take huku mwanawe ambaye Ni waziri mkuu akizurula Marekani kwenye makasino.
 
Ili nchi iendelee inahitaji kiongozi mwenye maamuzi magumu na uthubutu. Maamuzi ambayo muda mwingine hayatapendwa na wananchi. Mambo kama haya hayawezekani chini ya demokrasia...
Umeongea ukweli demokrasia inaleta division kama mbinu ambazo mkoloni alitumia kumtawala mtu mweusi.

divide and rule.

Alikuja Meko hapa katawala miaka 5 tu.

mmeimba nyimbo zote nawashauri bakini na demokrasia yenu
 
Sasa mbona ktk Afrika, nchi nyingi ambazo kiuchumi ziko juu, ni zile zinazoongoza kwa demokrasia japo kwa kiwango fulani?na zile za makatiri sana hasa za west afrika ndiko umaskini umeshamiri?hii inakiwaje?

mfano mzuri hapa kwetu kwa awamu ya tano, licha ya ukatiri uliokuwepo ni hatua gani kubwa ya kimaendeleo tulifikia?

hali ya kiuchumi kwa wananchi ilikuwa mbaya , lakini waimba mapambio walikuwa wanasifia tu, leo hayupo ndio wanatuambia ukweli kuwa "jamani hali ilikuwa mbaya sana zile zilikuwa propaganda tu" tatizo la dikteta yeye ndiye anajiona kuwa anaakili kuliko wengine!!
 
Ili nchi iendelee inahitaji kiongozi mwenye maamuzi magumu na uthubutu. Maamuzi ambayo muda mwingine hayatapendwa na wananchi. Mambo kama haya hayawezekani chini ya demokrasia...
Hivi Nyie huwa mwaandika tumia akili ,au mnatumia nini?

Kama uelewi siasa bora ni moja ya kuleta maendeleo Basi pole Sana, mbona mnakua wanafiki Sana?

Mambo ya kijinga Sana mwawandikia watu
 
Mkuu samahani nini maana ya demokrasia? Upi msingi wa uwepo wa demokrasia? Na Ni kivipi nchi haiwezi endelea kwa kufuata demokrasia?...
Demokrasia haina uhusiano wa moja kwa moja na maendeleo ila ni chanzo kikubwa ya mambo kwenda pole pole sana! msururu mrefu usio na mantiki
 
Sasa mbona ktk Afrika, nchi nyingi ambazo kiuchumi ziko juu, ni zile zinazoongoza kwa demokrasia japo kwa kiwango fulani?na zile za makatiri sana hasa za west afrika ndiko umaskini umeshamiri?hii inakiwaje?mfano mzuri hapa kwetu kwa awamu ya tano...
nchi gan yenye demokrasia imepiga hatua?
 
Wadada wa kazi mna maneno.
Udikteta tangu lini ukawa mzuri?...
South Africa ambayo kidogo kwa Africa demokrasia yao imekomaa wakawa na Rais Zuma ambaye amefanya ufisadi wa hovyo.

Ufisadi unaweza fanyika kuwepo na demokrasia au kusiwepo. Demokrasia siyo dawa ya ufisadi na wala siyo kwamba nchi ikikosa demokrasia basi inakuwa ya kidikteta, kinyume cha demokrasia siyo udikteta.
 
Ili nchi iendelee inahitaji kiongozi mwenye maamuzi magumu na uthubutu. Maamuzi ambayo muda mwingine hayatapendwa na wananchi. Mambo kama haya hayawezekani chini ya demokrasia...
Unaweza kuwa sahihi. Maswali machache. Huyo kiongozi mwenye maamuzi magumu utamtambuaje na atapatikanaje.

Na kama maamuzi yake yatakuwa mabaya (kwa mfano maamuzi yake yakilenga zaidi katika kujilimbikizia mali na watu wake wachache.

Mifano ya viongozi kama hao ipo mingi barani Afrika). Pia atadhibitiwaje na nani au chombo gani
 
nchi gan yenye demokrasia imepiga hatua?
Badala yake nchi ambayo haina Demokrasia kama Misri ndiyo inaendelea. Ina sera bora za Uchumi nk. Morocco ya kifalme iko mbali kabisa.

Hadi tunawaomba watujengee uwanja. Libya ya Gaddafi ilikuwa mbali sana. Hapo hatujazungumzia jinsi South Korea na Singapore zilivyoendelea bila demokrasia.

Hatujazungumzia Malaysia ilivyopiga hatua kubwa kimaendeleo chini ya demokrasia fake.
 
Unaweza kuwa sahihi. Maswali machache. Huyo kiongozi mwenye maamuzi magumu utamtambuaje na atapatikanaje. Na kama maamuzi yake yatakuwa mabaya (kwa mfano maamuzi yake yakilenga zaidi katika kujilimbikizia mali na watu wake wachache. Mifano ya viongozi kama hao ipo mingi barani Afrika). Pia atadhibitiwaje na nani au chombo gani
Hii ni tatizo kubwa, lakini kuna nchi kama China wamefanikiwa kuwa na mifumo ya kuwajibishana huku serikali ikiwa na uwezo wa kufanya maamuzi magumu kwa maslahi ya nchi bila kulazimika kufanya maamuzi ya kuwapendeza watu ili wabaki madarakani.
 
Mkuu samahani nini maana ya demokrasia? Upi msingi wa uwepo wa demokrasia? Na Ni kivipi nchi haiwezi endelea kwa kufuata demokrasia?
Na nchi itapata vipi maendeleo isipo kuwa na demokrasia?

Kipindi Cha mfumo wa chama kimoja nchi ilipiga hatua kiasi gani ? Maana kulikuwa hakuna mfumo wa vyama vingi Mpaka 1992.
Kiufupi demokrasia ni serikali ya watu. Yaani watu ndiyo wamiliki wa serikali, na kinadharia ni kuwa maamuzi yote na sera zote za nchi zinatokana na watu. Yaani kama unakampuni, basi kila mfanyakazi ni mmiliki wa kampuni na ana-say ya jinsi gani kampuni iendeshwe.

Na kuhusu kutoendelea chini ya chama kimoja ni sababu ya sera mbovu za kijamaa na si sababu ya kukosa demokrasia. Kinachotakiwa ni sera nzuri tu.

China ya enzi za Mao na China ya leo zote zinaongozwa na chama kilekile. Lakini China ile Ilikuwa maskini na hii ya leo ni tajiri, kilichobadilika ni sera za kiuchumi: kusaidia makampuni yake kukua na kuingia kwenye soko huria kwa tahadhari.
 
Ili nchi iendelee inahitaji kiongozi mwenye maamuzi magumu na uthubutu. Maamuzi ambayo muda mwingine hayatapendwa na wananchi. Mambo kama haya hayawezekani chini ya demokrasia.

Hata wanaotuhubiria demokrasia kila siku wanajua kuwa haifai pale maamuzi magumu yanapohitajika. Ndiyo maana mataifa yenye nguvu yamejipa kura ya Veto umoja wa mataifa. Na pengine ndiyo maaana wanatuhubiria kila siku tuwe na demokrasia, wakijua kuwa tukiwa na demokrasia tutabaki maskini siku zote.

Demokrasia inabidi kuangaliwa upya

Kwani Kenya haiendelei? South Africa na botswana haziendelei.......
 
Back
Top Bottom