Uchaguzi 2020 Nchi ipo kwenye tope. Tumekwama kwa miaka mingine mitano, au zaidi...

Kalamu ya Mwananchi

Senior Member
Oct 27, 2020
100
550
Uchaguzi umemalizika. Kuhusu kama uchaguzi ulikuwa ni wa uhuru na haki, wote majibu tunayo moyoni. It was not.

Cha muhimu ni kwamba upinzani umegain enough momentum kiasi kwamba umekuwa tishio hadi kuitikisa CCM na kuwafanya wawe desperate, ambapo hawakuwa na namna nyingine zaidi ya kufanya hujuma za hali ya juu na za wazi wazi ili kubaki madarakani.

Kilichofanywa na Magufuli kingefanywa na mwenyekiti yoyote yule wa CCM ili kuokoa chama chake. Kwahiyo tusidhani mambo yangekuwa tofauti kama raisi asingekuwa Magufuli bali mtu mwingine kutoka chama hicho hicho. Tanzania, de jure ni multiparty democracy lakini de facto ni a one party state, ndo madhara yake hayo.

Uchaguzi pia umewaonyesha wananchi na upinzani picha halisi ya chama/ serikali wanayopambana nayo.

Kwa ambao wanajidanganya kuwa mambo yatakuwa afadhali baada ya hapa, basi hawajajifunza kitu chochote kuhusu miaka mitano iliyopita. Mambo yanaenda kuwa mabaya zaidi.

Sheria zitatungwa ili kupunguza momentum waliyogain wapinzani, uhuru wakujieleza unaenda kuzikwa rasmi na kila aina ya sheria kandamizi zitapitishwa ili kutarget wale ambao wanataka 'kukwamisha maendeleo'.

Uchumi utazidi kuporomoka na maisha ya wananchi yatazidi kuwa magumu zaidi.

Tutegemee more white elephant projects ili watawala kufurahisha nafsi zao kwa kisingizio kuwa wanaleta maendeleo. Miradi ambayo haina manufaa yoyote kwa mwananchi wa kawaida.

CCM isifurahi ikadhani kuwa upinzani sasa umekufa rasmi kisa bunge linaenda kuwa la kijani tupu, na wabunge karibia wote wa upinzani wameondolewa. Watu wengi sana wamechukizwa na huu uchaguzi, sasa serikali ijiandae kupambana na upinzani ambao utakuwa ni invisible.

Ni muda sasa strategy ikaja ya kuzindua wananchi waliolala usingizi wa pono wakihisi siasa haziwahusu, mkazo unahitajika ili kuongeza awareness na mwamko wa watu. Ndo maana serikali inatunga sheria kila kukicha kuondoa uhuru wakujieleza, wa vyombo vya habari na uhuru wa kupata taarifa. Na inaivest kwenye kutengeneza distractions na 'ubuyu' wa kila aina ili kupunguza mwamko mwananchi.

Muda wa wananchi kuzinduliwa umewadia.

Only when enough people are enlightened will this country be liberated.

Vive la resistance!
 
Majibu unayo wewe unamjibia kila mtu, lazima ujifunze hata kama Diamond Platnumz anaweza jaza uwanja wa Taifa haimaanishi ni presidential material. Jamaa yenu nyomi lilikua linamdanganya anasahau Majority watanzania wanataka maendeleo. Shika Jembe ukalime, wacha maneno maneno mengi.
 
Hili litakuwa ni tope la zege, maanake njia za kujikwamua hakuna; na wenye masululu wanatucheka wakiwa mbali; kama hao wamarekani na wengineo.
 
  • Thanks
Reactions: _ID
ukweli ni kwamba watu wengi hawajapiga kura hapa nilipo kuna watu 12 nimewauliza wnaniambia hawajapiga kura na kweli vidole vyao havina rangi alafu ukiangalia hata muitikio ulikua mdogo ile mistari milefu tuliyoizoea haikuwepo
 
Kilichofanywa na Magufuli kingefanywa na mwenyekiti yoyote yule wa CCM ili kuokoa chama chake. Kwahiyo tusidhani mambo yangekuwa tofauti kama raisi asingekuwa Magufuli bali mtu mwingine kutoka chama hicho hicho. Tanzania, de jure ni multiparty democracy lakini de facto ni a one party state, ndo madhara yake hayo.
Hata sielewi kwa nini umeiweka hii aya kwenye mada yako, kwani hii habari sio kweli.

Hakuna mwenyekiti wa CCM yeyote kati ya hao waliopita angeweza kufanya haya yaliyofanyika wakati huu.

Wote hao walikuwa ni watu wenye ubinaadam, mbali ya kuwa na ushindani na wapinzani wao. Hiki unachokiona wakati huu ni tofauti kabisa. Inahitaji mtu mwenye sifa ya kipekee kabisa kuyafanya haya yaliyofanyika wakati huu.

Huuhaukuwa ushindani wa kifikra, bali nikufanya na kuwaambia washindani wako "utanifanya nini"? Unatumia vyombo vyote ulivyokabidhiwa na wananchi kulinda maslahi yao na ya nchi kwa manufaa yako binafsi!

Watu wa namna hii wapo wachache sana ndani ya nchi hii.
 
Uchaguzi umemalizika. Kuhusu kama uchaguzi ulikuwa ni wa uhuru na haki, wote majibu tunayo moyoni. It was not...
Kubali mmpigwa !
Siasa ni sayansi "by Dr Slaa"
Wagombea ubunge chama kimewanyima pesa!
Matangazo ya mgombea urais hakuna!
Siasa za mgombea wenu ni vurugu na kudai haki, bila kuongeza lugha ya wapiga kura utafaulu?, Mkulima wa ndizi na Uhuru na haki wapi na wapi!
Mawakala amjawapa posho!
Viongozi wakuu wa chama wamemsusa mgombea!
Mgombea kutetea ushoga waziwazi!
Mgombea kushirikiana na wezi wa Mali zetu na kutafuta wakili wa nje!
Mgombea kutoa vitisho kwa nchi yake, utafikiri yeye raia wa nje!

Siasa zenu za kupinga kola kitu siyo poa!
Uchaguzi huu ulikuwa huru, jifunzeni uzalendo
 
Mada kama hizi enzi hizo zilikua zinaletwa na watu kama Pascal Mayalla! Ila kwa sasa ndiyo hivyo tena! Imebakia tu stori.
Mkuu Tate Mkuu , kama ulivyosema enzi hizo, kila zama na zama zake, human beings are not static, they are dynamic and they change with time and place, zile ni enzi nyingine na hizi sasa ni enzi nyingine.

Enzi zile kulikuwa na katiba yake, sheria zake, taratibu na kanuni, kulikuwa na laws and order, sasa we are using the laws of the jungle, struggle for existence, survival is for the fittest, to be fit to survive, one has to be adaptive to the changing environments, usipoweza kubadilika kwenda na wakati uliopo, you just perish. I'm a survivor

P
 
Uchaguzi umemalizika. Kuhusu kama uchaguzi ulikuwa ni wa uhuru na haki, wote majibu tunayo moyoni. It was not...
Ukisema nchi imeingia topeni laaaahaulaaa. Sisi wengine unatifariji kiasi. Maana tope sheikh asikuambie mtu. Salaaaaaleeeeeeeeee.
Tuache tu tuchezee tope. Wengine twalipenda. Japo tumelazimishwa
 
Mkuu Tate Mkuu , kama ulivyosema enzi hizo, kila zama na zama zake, human beings are not static, they are dynamic and they change with time and place, zile ni enzi nyingine na hizi sasa ni enzi nyingine. Enzi zile kulikuwa na katiba yake, sheria zake, taratibu na kanuni, kulikuwa na laws and order, sasa we are using the laws of the jungle, struggle for existence, survival is for the fittest, to be fit to survive, one has to be adaptive to the changing environments, usipoweza kubadilika kwenda na wakati uliopo, you just perish. I'm a survivor
P
Wewe bado ni Great Thinker mkuu! Umefafanua vizuri sana. Na umechagua njia sahihi bila shaka.

Hata mimi baada tu ya Mzee Baba kuapishwa, huenda nikahamia moja kwa moja kwenye Majukwaa mengine. Mfano lile Jukwaa la MMU, Michezo, nk.

Hakuna namna. Watoto wangu bado wananihitaji sana. Nina uhakia Wasiojulikana wameshaanza tayari jalamba kwa ajili ya kazi yao maalum kama ilivyokua enzi zile za awali.
 
Mkuu Tate Mkuu , kama ulivyosema enzi hizo, kila zama na zama zake, human beings are not static, they are dynamic and they change with time and place, zile ni enzi nyingine na hizi sasa ni enzi nyingine.

Enzi zile kulikuwa na katiba yake, sheria zake, taratibu na kanuni, kulikuwa na laws and order, sasa we are using the laws of the jungle, struggle for existence, survival is for the fittest, to be fit to survive, one has to be adaptive to the changing environments, usipoweza kubadilika kwenda na wakati uliopo, you just perish. I'm a survivor

P
Kweli ulipitia jeshini flexibility ni muhimu ukiwa rigid utaumia..

Hongera CCM

Congratulations in advance President Magufuli
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 
Back
Top Bottom