Memento

JF-Expert Member
Jun 13, 2021
4,423
9,962
Nimeona wengi wakimshutumu Mwambe, lakini inawezekana Mwambe akawa yupo sawa Ila kikwete ndio aliongopa. Tarehe 17/10/2015 ilifanyika hafla ambapo raisi mstaafu J Kikwete alizindua jiwe la Msingi kwa ajili ya ujenzi wa bandari ya Bagamoyo.

Hadi kufikia hatua ya kuweka jiwe la Msingi tafsiri rahisi ni kuwa mmeshakubaliana (mkataba) kuanza ujenzi. Sasa hivi Mwambe anasema hakuna mkataba uliosainiwa bali ilikua muhtasari tu wa vikao, sasa Cha kujiuliza lile jiwe walilozindua raisi kikwete pamoja na wale wachina ilikua geresha?

Au inawezekana pia raisi kikwete alituongopea, lile jiwe la Msingi halikua kwa ajili ya bandari ya bagamoyo.

Ni nani mkweli Kati ya kikwete na Mwambe?

Chini nimeweka clip ya you tube kikwete alizindua hilo jiwe la msingi



Screenshot_20211119-181127_1.jpg
 
Mtoa Mada ungeweka na Mifano pamoja na tafsiri kuwa kuweka jiwe la msingi ni sehemu ya mkataba. Mbio za mwenge au waziri fulani huwa wanaweka mawe ya msingi kwa ujenzi fulani na inakuwa kwenye michoro tu, badaye ndiyo hutafuta pesa au mwekezaji, wakikubaliana na mwekezaji ndiyo mkataba husainiwa.

Je, unafahamu kuwa michiro ya bandari ya bagamoyo imechorwa na serikali ya Tanzania au China,ukilifahamu Hilo ndiyo utajua nini maana ya jiwe la msingi.
 
dah nilitaka kuuziwa kiwanja hapo ukuni kikubwa kweli kwa bei yakutupa nikadharau... dah leo bei zitakuwa balaa......

Tuache siasa, hatuwawezi hawa wanasiasa wetu washatushinda na sisi ni majibwa koko tu....sisi tutafute fursa zilizopo na sisi tufanye yetu..
 
Kikwete akiwa rais wa Tanzania aliweka jiwe la msingi kuashiria kuanza rasmi ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo.

Hiyo ina maana kuwa majadiliano yalishafanyika, mkataba ulishasainiwa, bajeti ya pesa ilishatengwa, utekelezaji wake ulishaanza!

Alipoingia Magufuli akasema amesitisha ujenzi (utelekezaji) wa bandari ya Bagamoyo kwa sababu mkataba ule ulikuwa haina maslahi kwa Tanzania.

Sasa tulitegemea serikali ya Samia Suluhu ije na kauli kuwa, imeamua kufufua ujenzi wa bandari ya Bagamoyo ambao mkataba wake ulizuiwa kutekelezwa na Magufuli.
 
dah nilitaka kuuziwa kiwanja hapo ukuni kikubwa kweli kwa bei yakutupa nikadharau... dah leo bei zitakuwa balaa......

Tuache siasa, hatuwawezi hawa wanasiasa wetu washatushinda na sisi ni majibwa koko tu....sisi tutafute fursa zilizopo na sisi tufanye yetu..
Bandari inaanzia mlingotini mpaka zinga. Haya maeneo ndiyo ya kuwahi kuwekeza nyumba za kupanga na lodge kwa ajili ya wageni na wafanya kazi wa bandari. Changamkieni fursa mapema
 
Hakuwahi (aliwai = aliwahi). Ila wanavyocheza shere na kupishana kauli sasa hivi; unaweza kutumia akili na kugundua kuwa kuna kiti wanakwepa.

Hata kama mwanzo kulikua na mkataba, basi hauwezi tena kua una prevail baada ya marehemu kua ameukataa. Inawezekana wawekezaji husika (China na Oman na North Korea) walishaamua kuachana na mradi huo wa US$ 10bn.

Kwavyovyote vile kuwarudisja tena mezani lazima mazungumzo yaanze upya ikiwa kila nchi mdau bado ana nia ya kuendelea nao. Inawezekana mtazamo wa kila nchi husika kuhusiana na mradi huo umebadilika. Kwa maana hiyo hata makubaliano ya vipengele vya mkataba haviwezi kua kama vya mwanzo

Ila nchi za Kiafrika hatuko consistent kwenye mambo muhimu ya nchi zetu. Ndio maana tuna struggle sana kupata wawekezaji na kuvutia mitaji kutoka nje. Regime change kwetu inakua na uncertainty nyingi sana. Watu serious duniani hawatuelewi!!!
 
Mkataba wa kipumbavu alipaswa auweke wazi ili kila mmoja auone huo upumbavu.
Kwakuwa amefanya siri ni ngumu kuamani maneno yake, maana hata yeye amefanya upumbavu mwingi tu.

Tokea upate ufahamu ulishawahi kuonyeshwa mikataba hadharani ama unajisemea tu…Jiwe aliamua kuwa muwazi period… maana hili swala la Tanzania kufanywa kichwa cha mwendawazimu kilimkera sana, mara kwa mara alikuwa anasema tumechezewa sana…imetosha

sasa km wewe ni tomaso subiria nchi iuzwe hii uchakae…ukafikiria ni watu wote wako kwa ajili ya maslahi yako…
 
Tunakwenda na kauli ya SPIKA mh.Ndugai kuwa "VIONGOZI WALIPOTOSHWA...."

Maisha inabidi yaendelee na huo mradi inabidi uendelee kwa faida ya taifa.........


Siempre JMT
 
Kikwete akiwa rais wa Tanzania aliweka jiwe la msingi kuashiria kuanza rasmi ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo.

Hiyo ina maana kuwa majadiliano yalishafanyika, mkataba ulishasainiwa, bajeti ya pesa ilishatengwa, utekelezaji wake ulishaanza!

Alipoingia Magufuli akasema amesitisha ujenzi (utelekezaji) wa bandari ya Bagamoyo kwa sababu mkataba ule ulikuwa haina maslahi kwa Tanzania.

Sasa tulitegemea serikali ya Samia Suluhu ije na kauli kuwa, imeamua kufufua ujenzi wa bandari ya Bagamoyo ambao mkataba wake ulizuiwa kutekelezwa na Magufuli.
Unaitafuta kauli ya mh.Rais SSH?!!!

Hivi bado hujaelewa tu kauli ya mh.Spika Ndugai kuwa "VIONGOZI WALIPOTOSHWA"?!!!

Mh.Samia naye alikuwa ni kiongozi awamu ya 5.........

Mambo ya kinchi inabidi yaendelee tu kwa faida pana.......

#Siempre JMT
 
1.MOU PROPOSAL,(Tentative)
2.MOU AGREEMENT.
Jiwe la msingi linaweza wekwa hatua yoyote bila kuiua pesa utapata wapi.

Nilichoona katika maelezo tangu awamu ya 4,5,6 wanaelezea kimhemko ndio maana maswali ni mengi na wachangiaji wanachambua matamko badala ya kuhoji mkataba wenyewe use
Umesainiwa au
Haujasainiwa.
Wote tumekuwa MAZUZU wakuchambua hewa.
 
Back
Top Bottom