Nchi inayumba, tuanzishe mgogoro wa kitaifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nchi inayumba, tuanzishe mgogoro wa kitaifa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ntaramuka, Oct 22, 2008.

 1. Ntaramuka

  Ntaramuka Senior Member

  #1
  Oct 22, 2008
  Joined: May 2, 2008
  Messages: 169
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kufuatia hali ilivyo katika nchi yetu ni dhahiri kuwa kunahitajika juhudi za watanzania wenyewe kuinusuru nchi yetu. Viongozi wametusaliti,rasilimali za nchi nk wamefanya za kwao sisi wametuacha maskini na hali ngumu ya maisha, matokeo yake kila kona sasa ni maandamano kupinga dhuluma ya serikali yetu. Tazama migomo ya walimu, wastaafu, NMB nk.

  Lakini kikubwa zaidi na cha KUTISHA ni kwamba wastaafu wa JWTZ nao wanaandamana kudai chao! Jamani hii ni ishara mbaya.

  Ili kuinusuru hali hii ni lazima watanzania wote tuungane, tuandamane nchi nzima kuishinikiza serikali hii ya JK iliyopoteza uelekeo ili ikiwezekana watuachie nchi yetu ili kutuepusha na balaa linaloweza kutupata kwani hakuna ubishi tena kwamba JAKAYA nchi imemshinda

  MUNGU IBARIKI TANZANIA,
  WABARIKI NA WATU WAKE,
  AMIN,
   
Loading...