Nchi inavyoliwa: OUT na mabonanza, kila mtu na kasungura kake! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nchi inavyoliwa: OUT na mabonanza, kila mtu na kasungura kake!

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by siyabonga, Oct 12, 2012.

 1. s

  siyabonga Senior Member

  #1
  Oct 12, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 125
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mambo yanavyoenda kwa hivi sasa tuko katika auto- pilot. Kila mtu anajaribu kuvuna karibu anavyoweza katika eneo lake. Madini, Mali Asili, Viwanda, Afya basi alimradi kila mtu anakula anavyoweza. Ukikipata kitumie, na ukikosa kijutie!

  Hawa jamaa wa Chuo Kikuu Huria ni sherehe tu, party na mabonanza kila siku, sijui kazi wanafanya saa ngapi.

  Wakitoka huko ni kujishughulisha na mambo ya Mamiss, mivinyo, safari na ubadhirifu. Wana kesi nyingi za wizi na ubadhirifu mahakamani.

  Upo msururu wa watu ambao kwa miaka mingi hawajahitimu kwa kuwa papers zao bado hazijawa marked katika ngazi mbalimbali, idadi yao ya wanafunzi inazidi kushuka mwaka hadi mwaka. Hawana muda wa kufanya majukumu yao ya msingi.

  Kwa mtaji huu, sijui kama tutafika. Udhaifu kila mahali, hakuna mwenye muda wa kumsimamia mwingine. KWELI HILI NI SHAMBA LA BIBI!
   
 2. Brightman Jr

  Brightman Jr JF-Expert Member

  #2
  Oct 12, 2012
  Joined: Mar 22, 2009
  Messages: 1,233
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Wewe ni mmoja wa waathirika wa mambo ulioelezea hapa au umetumwa?
   
 3. N

  Nonda JF-Expert Member

  #3
  Oct 12, 2012
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
Loading...