Nchi inapokosa maono hulazimika kutekeleza maono ya mataifa mengine. Hii ni aibu kubwa, viongozi na watanzania tujitathmini

Hero

JF-Expert Member
Aug 20, 2010
3,172
2,000
Imekuwa ni kawaida kusikia wanasiasa kwa mfano wanatoa matamko yenye hamasa juu ya kuongeza mara soya, mara ufuta mara castor oil kwa kuwa wachina wanahitaji, nk.

Kwa hiyo kama nchi tumekuwa bendera kufuata upepo kwa muda mrefu.

Ndio maana hata baada ya kuanza kuendeleza bandari ya Dar, Kilwa, Mtwara, na Tanga, kabla hata hatujakamirisha wachina nao wakaja na maono yao kuwa kutaka kuitaifisha bandari ya bagamoyo kwa kidingizio cha kuijenga kwa fedha yao wenyewe, na kwa kuwa kama taifa hatuna maono tukajikuta kuanza kuwaza kujengewa bandari hiyo kwa masharti ambayo ni kichaa tu ndio anaweza kukubaliana nayo.

Inatia huruma sana na hasira kuwa nchi ya kuyumbishwa kwa kuwa mtekerezaji wa maono kutoka nje! Hata kama ni familia yako lazima itayumba sana na kwa kweli itakuwa ya kusikia maendeleo kwa majirani tu.

Nitoe wito kwa watz wote wenye mapenzi mema, tujikite na kuhakikisha yote tuliyoyaanzisha kwa fedha zetu kama nchi, iwe kwa mkopo au cash yetu, tuyathamini hayo na kuhakikisha yanatimia na kutoa huduma zilizotarajiwa! Tusiwe wepesi kudandia maono ya wengine kama mataahira.

Niseme tu, bandari ya Bagamoyo ni yetu na tutaijenga muda muafaka kwa utaratibu na masharti yetu bila kupelekeshwa wala kuharakishwa kwani Tz ni nchi huru yenye watu wanaojitambua.

Mungu ibariki Tanzania, amen🙏
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
8,434
2,000
Kama watu wenyewe wanaojitambua ni hawa kina bajaji na bwana wasukuma, basi safari hiyo bado ni ndefu mno. Hii ni kwa sababu wale maadui zetu ujinga na wale wenzake wamejikita mno ndani ya nguo zetu.

Hiiiiii bagosha!
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
7,259
2,000
Kwa hiyo na wewe ni sehemu ya hao Viongozi!! Kiasi mnataka eti kujitathmini!!! 🤔

Hii nchi ina utani sana aisee!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom