Nchi inakwenda wapi? Mwenyezi Mungu tusaidie

MANILABHONA

JF-Expert Member
Apr 1, 2015
462
348
Wiki iliyopita katika kipindi cha Frola show kwenye stesheni moja ya TV mgeni mwalikwa alitamka maneno yaliyonitisha kidogo, alisema chagueni viongozi wanaofanana na Mwl.Nyerere. Chama cha Mapinduzi (CCM) alichokiongoza Mwalimu kilikuwa chama cha wakulima na wafanyakazi kilichojali misingi ya utu, usawa na haki .kilikuwa chama chenye itikadi iliyoonesha wazi ujamaa na kujitegemea kilihimiza watu kufanya kazi kwa bidii mavuno yanayopatikana tugawane sote kwa usawa . Tulihubiri amani na umoja KILIKUWA CHAMA KINACHOONGOZA NA SI KUTAWALA Nikajiuliza maswali wapo kweli watu wa namna hiyo? Pengine wapo lakini hawajui wala hawapendi kujiingiza katika siasa. Hebu tuangalie wanaovuma sasa hivi na vyama vyao:
1.CCM: ya sasa siyo ile ya Mwalimu Nyerere!!!! ya sasa inatafsiriwa CCM= CHUKUA CHAKO MAPEMA na ndicho kinachoendelea sasa hivi kila anayepata nafasi basi anajirundikia mali majumba na kadhalika na kuweka ndugu zake katika nafasi fulani fulani ili waweze kufaidi vizuri, rushwa imekuwa ndio msingi wa maisha, katika chama tumekuwa tukibaguana kwa misingi ya dini na kabila. Kila mtu sasa hivi atajijua mwenyewe ndo maana yanaibuka makundi ya ajabuajabu. NI WAZI CCM HII YA SASA YA CHUKUA CHAKO MAPEMA HAIFAI KABISA KUENDELEA KUTAWALA NCHI. Sasa ni chama (kiongozi) gani mbadala?
2.CUF: Kinaweza kuwa na nguvu Zanzibar lakini si Tanzania bara, wakati fulani kauli zake zinatia hofu mfano jino kwa jino. ngunguri au ngangari sera zake hazifahamiki vizuri kwa wananchi Katika nyakati fulani Mwenyekiti wake anaonekana kuwa na Busara
3.CHADEMA: Kinaonekana kupendwa na watu wengi hasa wenye asili ya kaskazini mwa Tanzania Inaonekana hata uongozi katika chama hiki unatolewa kwa kufuata misingi ya ukabila.Hii inawatia hofu wananchi wengine wasiokuwa Wachaga.Lakini pia fuatilia mihadhara yao wanachokihubiri ni vitisho.ugomvi chuki na uchochezi. Wanachokihubiri si amani tena bali wanaandaa jeshi kwa ajili ya mapambano wanaliita RED BRIGADE!!!!!. Kuna taarifa pia kuwa kina udini ndani yake.Waogopeni watu hawa wanaotaka kuingia ikulu hata kwa kumwaga damu. NI WAZI CHAMA HIKI PIA KAMA ILIVYO CCM YA SASA NACHO HAKIFAI KUINGIA MADARAKANI NA KUONGOZA NCHI
4.NCCR: Kidogo kinaonekana kuwa na uongozi makini, imara na kiongozi anayejua siasa. Tatizo kinaathiriwa na Anakotokea Mwenyekiti wake kaskazini kusikoaminika kule ambako kila kitu kwao ni dili hata kuongoza nchi ni dili la kuingiza pesa (Nyerere aliuliza kuna biashara gani huko Ikulu) lakini pia hakina wanachama wengi
5.ACT-Ni chama kinachohubiri falsafa ya Mwalimu Nyerere, kama ilivyokuwa CCM ya Mwalimu. kinahubiri amani, rasilimali kwa wote. Lakini ni chama kichanga hakina muda mrefu na kina wanachama wachache.Sina uhakika kama viongozi wa chama hicho wakipewa nafasi watasimamia yale wanayohubiri kwenye mikutano. Wanaowajua vizuri pengine watusaidie je wana msimamo thabiti wa kutuletea Tanzania ya wakati wa Mwl Nyerere? Pengine ndio chama pekee chenye nafuu.
Eeee Mwenyezi Mungu tuwekee Nuru nchi hii iko gizani ,hatujui tuendako
 
Kumbe umetumwa na ccm ndomana kila nikichungulia nakukuta pekeyako kweli watz wameamua mwaka huu
 
We umetumwa, mwanzo umeanza vizuri, baadae umeharibu, huna maana. Mods delete hii kitu ndo inavunja amani.
 
Back
Top Bottom