Nchi inakoelekea si salama-Askofu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nchi inakoelekea si salama-Askofu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Jan 24, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 24, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  Nchi inakoelekea si salama-Askofu


  Na Benjamin Masese

  KIONGOZI wa kundi la waumini waliojitenga na Kanisa la Anglikana la Tanzania, Askofu Ainea Kusehna amesema kuwa nchi inapoelekea sasa si salama kutokana na
  baadhi ya viongozi kuchaguliwa kwa rushwa huku wakinyosheana vidole.

  Askofu Kusehna alisema hayo katika ibada maalumu iliyofanyika Mbezi Beach, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi wote wa kanisa hilo la Anglikana la Kiinjilisti Tanzania (KAKT) kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara.

  Katika ibada hiyo Askofu Kusehna alisema matatizo manne yanayoikabili nchi na watu wake ikiwa ni pamoja na rushwa, tamaa ya fedha na mali, madaraka na ukubwa pia tamaa ya starehe.

  Askofu Kusehna alisema makanisa yatasarambatika na taifa kuhangamia ikiwa watu wake hawatabadilika na kuacha uchu wa madaraka ya rushwa na kufuata haki inayoinua taifa lolote la demokrasia.

  Alisema kuwa asilimia kubwa ya maaskofu na viongozi wa serikali wanachaguliwa kwa rushwa na kuwa yupo tayari kuwataja viongozi wa dini pale inapohitajika katika vikao vyao vya majadiliano.

  "Mkisikia maaskofu wakitajwa, tambueni si wote ni maaskofu kutokana na matendo yao maovu ya rushwa, na ndio wa kwanza kuwanyoshea vidole wengine bila kujitambua kuwa wao wameoza.

  "Sisi tunatakiwa kuwa nuru kwa jamii pia kuwa mfano wa chumvi inayoleta ladha katika chakula, hebu niwaulize leo, sisi ni chumvi katika jamii?" alihoji. .

  Aliongeza kuwa kizazi hiki cha maaskofu ni cha usanii, na hakiwezi kutoa neno la Mungu linaloburudisha na kubadili mtazamo katika jamii, bali wanatoa somo linaloweza kuwalinda wao, huku wakiunga mkono kuwepo kwa ushoga na usagaji.

  Akizungumzia usajili wa kanisa hilo alisema kuwa kumekuwepo na mikakati kabambe kutoka kanisa la Anglikana Tanzania ya kuchafua kundi hilo ili likose usajili, na kuwa tayari wamepata nyaraka zao zilizopelekwa Wizara ya Mambo ya Ndani zikidai kwamba kikundi hicho kinatumia vichochezi vya kikabila, jambo ambalo ni hatari linaweza kudhoofisha mtengamano na umoja wa makanisa na nchi nzima.

  Askofu Kusehna alisema kuwa nyaraka hizo ziliandikwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana, Valentino Mokiwa kwenda kwa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Bw. Laurence Masha ambaye alimjibu kwa kumhakikishia kanisa hilo halitasajiliwa.

  Aliongeza kuwa tuhuma zingine ni pamoja na kudaiwa kutumia nembo ya Anglikana, vitabu vyake vya ibada, nyimbo na liturgia, kinyume cha sheria, wakati likiwa halijasajiliwa.

  Askofu Kusehna alihitimisha kwa kutoa tamko kwamba hakuna anayestahili kumnyoshea mwingine kidole iwe serikali, polisi, viongozi wa dini au wananchi kwa kuwa wote wana makosa, na pia wote wanatakiwa kujisafisha kuanzia kwenye chimbuko la matatizo hayo.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 24, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  Hali ya mustakabali wa taifa hili ipo njia panda kwa sababu serikali ya JK ni ya kifisadi na hatuwezi kuiamini kuandika katiba mpya itaichakachua tu kama ilivyochakachua uchaguzi mkuu na kujipa uhalali wa kuendelea kubaki madarakani...........................

  Jibu thabiti ni maandamano nchi nzima kulishinikiza Bunge kumfungulia JK mashitaka ya kulipora taifa hili utajiri wake kupitia DOWANS...kuanzia uteuzi wa Dr. Idrissa Rashid pale Tanesco.........mkataba wa kitapeli wa RICHMOND na ule uliofuata wa DOWANS........................................haya ni makosa ya uvunjaji wa katiba na Bunge inapaswa kuyachunguza haraka iwezekanavyo....................................

  Hakuna kuwaogopa wabunge wa CCM na uwingi wao Bungeni mbele ya nguvu ya umma..................................................
   
 3. Jaluo_Nyeupe

  Jaluo_Nyeupe JF-Expert Member

  #3
  Jan 24, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 2,269
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180

  Mhh! hili la kuwashirikisha wabunge wa CCM nina shaka nalo kama tutakuwa pamoja.
   
 4. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #4
  Jan 24, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Na tunapozidi kwenda mbele mambo na maisha ndivyo yatazidi kuwa magumu zaidi
   
 5. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #5
  Jan 24, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  CCM wanabakia kusingizia udini wakati hakuna udini badala ya kukimbilia kwenye hoja za msingi hiki chama hiki
   
 6. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #6
  Jan 24, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Naona hapo vita ya ufisadi imeingia kanisani! Minyukano kila kona
   
 7. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #7
  Jan 24, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  udini utoke wapi TZ? hii si Pakstani wala Iraq, ni watawala dhaifu, wanautaka kutumia muhimili wa udini kugawa watu ili watawale na kuibia watanzania ki ulaini (divide and rule)
   
Loading...