Nchi inaitwa Bongo land nchi ya dili

Speed of light

JF-Expert Member
Nov 8, 2014
313
284
Ni jambo la msingi kuelewa historia ya jambo lolote kwa lengo la kutatua tatizo na pengine kuliendeleza kwa ufanisi jambo hilo

Kwa misingi hiyo Ingelikuwa ni vizuri zaidi kwa Magufuli kukubaliana na mkondo wa maji unakoelekea huku akijitahidi kutayarisha miundo mbinu ya kuubadilisha mkondo wa maji katika muulekeo mpya. akitumia nguvu kubwa kuulazimisha mkondo wa maji upande mlima bila shaka anaandaa mafuriko na mwisho wa siku maji yatajielekeza muelekeo wenye mteremko

Siku Mheshimiwa alipowaapisha makatibu wakuu kiapo cha uadilifu hadharani kidogo nilipigwa na bubumbuwazi. nilijiuliza maswali mengi bila kupata majibu ya kuridhisha.

Azimio la Arusha lilikuwa jibu tosha kwa viongozi wa serikali kuhusiana na swala la uadilifu. viongozi wenye dhamana hawapaswi wawe na hisa popote au wamiliki shughuli za kibiashara bali wawe ni wasimamizi wa sera za serikali tu ili kuondoa ufisadi na hujuma katika shughuli za kiserikali na za kiungozi

viongozi na watumishi wa serikali hawapaswi wawe na kazi mbili aidha wachaguwe uongozi ama shughuli binafsi waswahili wanasema mshika mbili mmoja humponyoka

Ingawa sera ya ujamaa imepigwa kumbo kimya kimya na kuukumbatiwa ubepari bado wananchi wana tamaduni na fikra za kijamaa ndani ya damu ni vigumu kuwabadilisha kwa ghafla imechukua miongo kadhaa kujenga imani za kijamaa

kinadharia na kiasili sisi ni wa mfumo wa kijamaa. kivitendo serikali inafuata sera za kibeberu,huu ni usanii wa hali ya juu kabisa, ndio maana likazuka neno BONGO LAND Nchi ya wenye kutumia bongo tumia akili yako ya ziada ili kuendesha maisha na sio sheria, kanuni na taratibu.

Sheria zipo vitabuni kivitendo tunatumia bongo zaidi kuzivunja. kwa mfano neno
DILI. linamaanisha kupata chochote kinyume na sheria na tararibu hakuna mwananxhi asiyefahamu maana ya neno DILI na hata kujihusisha na DILI Yenyewe ni sehemu ya maisha ya wanachi wa bongo land kama huamini nenda popote nchini kwa mwananchi yoyote haijalishi mnafahamiana ama la mwambie nina mifuko ya sukari ama mabati ama chochote kile cha DILI Uone kama atakushangaa ama ataanza mchakato wa majadiliano na kuichangamkia Hiyo DILI asilimia 90% watakubali kutoa ushirikiano

Magufuli you have long way to go kubadilisha mifumo iliyojengeka miaka mingi
angalia usiwape wapinzani njia rahisi ya kukiangusha chama chako kwa kukivua nguo hadharani. wapinzani wanakushangilia sana pale unapokiacha uchi chama kilichokuweka madarakani. kwa kuzikejeli serikali zilizopita ambazo zilikuwa ni za hicho hicho chama chako cha mapinduzi mwisho wa siku wapinzani watawashawishi kirahisi wananchi kukikataa chama cha mapinduzi si tayari umekiadhiri hadharani...?

historia ni mwalimu mzuri maishani.
 
Back
Top Bottom