Nchi inaelekea vitani; UPORAJI WA ARDHI WAWATISHA WABUNGE | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nchi inaelekea vitani; UPORAJI WA ARDHI WAWATISHA WABUNGE

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jul 13, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jul 13, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [TABLE="width: 879"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]• UPORAJI WA ARDHI WAWATISHA WABUNGE

  na Salehe Mohamed, Dodoma

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]
  WABUNGE wamesema serikali inaiandaa nchi kuingia vitani na umwagaji mkubwa wa damu kwa kuendekeza migogoro na uporaji wa ardhi unaofanyika sehemu mbalimbali hapa nchini.


  Onyo hilo limetolewa bungeni jana na wabunge mbalimbali walipokuwa wakichangia bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa mwaka 2012/2013 ambapo walisema serikali inawanyang’anya ardhi wananchi na kuwapa wawekezaji.

  Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu, alisema serikali imejigeuza wakala, dalali na kuwadi wa wawekezaji kwa kutumia nguvu kuwanyang’anya ardhi wananchi.


  Lissu alisema kitendo hicho ni hatari kwa taifa kwa kuwa kinaandaa mazingira ya vita na kutengeneza harakati za ukombozi na mapinduzi ya umwagaji damu siku zijazo.


  Alibainisha kuwa kesi za migogoro ya ardhi hapa ni nyingi ambapo mpaka sasa zipo 6,000 katika Mahakama Kuu, Kitengo cha Ardhi.


  “Kuna migogoro mingi kwenye ardhi ambapo mingine haipelekwi mahakamani kwa sababu chombo hicho kimekuwa mithili ya gulio la kununulia haki,” alisema Lissu.


  Lissu alisema wananchi hivi sasa wamekosa imani na mahakama inayoshughulikia masuala ya ardhi na matokeo yake wameamua kujichukulia sheria mkononi.


  “Migogoro ambayo imekuwa ikisababisha mapinduzi na vita vya kutafuta ukombozi katika baadhi ya nchi barani Afrika mingi ni ile inayosababishwa na ardhi,” alisema.


  Aliongeza kuwa serikali inafuata ubepari uchwara kwa kujigeuza kuwadi, dalali wa kuuza ardhi ya wananchi na kuwapa wawekezaji, ambao ni kampuni za Magharibi.


  “Tunatengeneza mapinduzi ya umwagaji damu siku zijazo, mimi sipendi niwe sehemu ya historia hiyo, nitawaambia wajukuu wangu kuwa tulikemea lakini tulizidiwa nguvu,” alisema Lissu.


  Lissu alitolea mfano kuwa serikali ilivyotumia nguvu kupora ardhi ya wananchi katika Jimbo la Singida Mashariki eneo la Shanta Mining, huku Mkuu wa Mkoa na viongozi wengine wa serikali wakipinga kimya kwa madai kwamba, wamekuwa makuwadi wa soko huria na wawekezaji.


  “Na namna zote zilifanyika ni wananchi kuchukua silaha. Waziri akifanya majumuisho aeleze vinginevyo wananchi wa Singida Mashariki wanasema ama zao ama za Shanta Mining,” alisema Lissu.


  Alisema kuna baadhi ya vitu vinatia aibu na kutolea mfano wa namna kampuni moja ya Kitanzania ya uwindaji wanyama kuingia mkataba na kampuni za uchimbaji wa madini ya uranium, kinyume cha sheria ya matumizi ya ardhi.


  “Kama si ukuwadi ni nini? Tunatengeneza mazingira ya vita vya wenyewe kwa wenyewe na hawatakuwa wamekosea,” alisema Lissu.


  Naye mbunge wa Kasulu Mjini, Moses Machali (NCCR-Mageuzi), alisema serikali inawalinda maofisa ardhi wanaopora ardhi za wananchi na kuvigawa kwa mtu zaidi ya mmoja.


  “Waziri wa Ardhi nilishakwambia kuwa Ofisa Ardhi wa Wilaya ya Kasulu, anauza maeneo ya wazi lakini hutaki kuchukua hatua, hivi kuna nini hapa, sasa nakwambia siungi mkono bajeti yako.


  “Siungi mkono na kama serikali itashindwa kuchukua hatua dhidi ya huyu Ofisa Ardhi, basi mimi nitawaambia wananchi wangu wachukue sheria mkononi maana nyie mmeshindwa kuchukua hatua.


  Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (CHADEMA), alisema atawahamasisha wananchi wake wachukue sheria mikononi ili wapate haki zao kwa sababu serikali imeshindwa kuitatua migogoro ya ardhi.


  “Polisi, serikali wameshindwa kuwasaidia wananchi wangu ambao kila wanapoipeleka migogoro ya ardhi kituo cha Polisi Kawe, askari hawachukui hatua kwa sababu wanapewa rushwa na wenye fedha.


  “Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri nakuomba uchukue hatua kumaliza migogoro hii, najua kuna mtu mmoja anamiliki Kituo cha Mafuta kiitwacho Tegeta Petrol Station, huyu amepora ardhi ya watu kwa kisingizio kuwa anafahamiana na watu wa Ikulu.


  “Mheshimiwa waziri hebu chukua hatua, kama umeweza kubomoa majengo fulani fulani pale Dar es Salaam, basi naomba ukavunje na yale majengo ambayo mimi na wewe tulifukuzwa na mlinzi siku tulipoyatembelea,” alisema Mdee.


  Mbunge wa Kisarawe, Selaman Jafo (CCM), pamoja na kutoridhishwa na migogoro ya ardhi jimboni kwake na Tanzania kwa ujumla, aliwatahadharisha watu waliopora ardhi kwenye mashamba pori jimboni kwake, kwamba ardhi hiyo itarudishwa serikalini kwa kuwa wameichukua bila kufuata utaratibu.


  Katika hatua nyingine, aliilalamikia serikali kwa kushindwa kuwachukulia hatua watendaji wasiokuwa waadilifu kwa kuwa ndiyo wanaosababisha migogoro hiyo katika maeneo mbalimbali nchini.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jul 13, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Serikali inachukua Ardhi toka kwa Wananchi bila kuwalipa na kuwapa Wawekezaji; Pesa Wawekezaji wanazolipa

  Watu serikalini wanagawana; Wananchi wa Tanzania ni Wapole, kwanini serikali ya CCM inataka kuwaamsha

  SIMBA waliolala? Wawekezaji watafurahi sana kwasababu wataaza kuchukua Madini yetu bure kama vile CONGO-

  KINSASHA
   
 3. Msalagambwe

  Msalagambwe JF-Expert Member

  #3
  Jul 13, 2012
  Joined: Jul 11, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Wabunge wa CCM wanabanwa na chama chao,
  Kutetea uoza wa serikali,
  kwa faida ya nani?

  Kule Kigamboni,
  ardhi inachuliwa na serikali,
  kutoa wanya,
  wa serikali ya Marekani,
  Kujenga,
  Kituokikubwa chajeshi Afrika.

  Serikali ya CCM,
  imehongwa mlungura,
  na serikali ya Marekaani,
  ili itumie,
  ardhi ya Tanzania,
  kueneza ubabe wake,
  Bahari ya Hindi,
  na Asia.

  China inakuja juu,
  kiuchumi na kijeshi,

  Sisi waTanzania,
  tusipochukua hatua sasa,
  tutaingia utumwani,
  sisi navizazi vyetu,

  khanga tshir na kofia,
  wali, nyama na pombe,
  mshahara wa masaa,
  usituponze,
  kuingia utumwa,
  sisi na vizazi vyetu.

  tunauz uhuru,
  tunauza utu,
  ili tuingie utumwani,
  kwa faida ya CCM
   
 4. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #4
  Jul 13, 2012
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Source Tathmini - John Mashaka on Economic Colonialism, Food Piracy, Land Grabbing & Future Conflicts hii hapa ya Ethiopia

  Tunaomba yeyote hasa waandishi wa habari watusaidie kutafsiri hii makala na kuirudisha hapa kwenye jukwaa na kulijadili. ina mahudhui mazito sana. Nimeona hadi waethiopia wanayatumia

  [​IMG]
  The African continent is facing its darkest moment yet, since the end of colonial era. There is enormous land grab, and food piracy trending in the continent, in which Africa's farmlands, and water sources, necessary for food production, are rapidly falling in the hands of –land grabbers- new wave of colonialists; Prevalence likely re-ignite another ugly chapter of confrontation.

  World largest commodity producers have sensed the dangers ahead, and since then have been imposing restrictions on their domestic staple food exports, in order to maintain economic, and food related security, leaving the global market with huge supply deficit. This new trend is posing a greater threat, particularly for Africa, whose farmland is becoming an alternative for wealthy countries with huge populations to bank on in terms of their future food sustainability

  History tells us that, major global conflicts and wars have been caused by the need for land, and imperialism; Quest for territorial expansionism and influence, need for natural resources, and food sufficiency. From the agrarian period, to the never ending Israeli-Palestinian conflict, land has been at the center stage. Similarly, the challenging internal and cross boarder future conflicts will be land related. The conflicts will be characterized by deadly internal uprising; hungry rural population looking for water and land for farming, turning against investors-land grabbers- or modern day settles if you will, while urban dwellers dying to have food revolting against their regimes.

  There is a new wave of scramble for the African continent and its resources. Rich nations with population explosion are buying huge tracts of the continents arable farmland, to meet their domestic food needs and security. Many wealthy nations, with no arable land, are exploiting the cracks of greed and corruption within the African regimes, to address the pressing food needs within their countries, leaving Africa in a potentially explosive situation. South Korea, China, Japan, India, Britain, UAE, and Saudi Arabia are leading the pack in land grabbing spree. Saudi Arabia has signed a deal for 500,000 hectares of land in Tanzania. South Korea has grabbed 960,000 hectares in Sudan, and 1.3 million hectares in Madagascar. These neo-colonialists are in Kenya, Uganda, Rwanda, Ethiopia, Congo, Mozambique, and Zambia just to name a few.

  In return for selling their countries, most of the African ill bent regimes have been receiving so called economic aid and personal goodies or incentives, as in the case of Madagascar's former president Ravalomanana, who was given a private jet for selling his country. The leader was eventually overthrown by angry urban poor, who could not afford to feed themselves. These foreign land grabbing, food pirates and colonialists are flocking in large numbers in the name of investors, taking African resources without firing a single bullet. They are coming with briefcases, and good to resist promises to the greedy African leaders, who are willingly signing contacts to hand over their countries to the settlers as modern day colonies.

  The most troubling secret behind these neo-colonialists, is that, all of the food produced in these farms, are not for domestic consumption; they are being shipped back to their home countries to feed their populations.
  According to London's Financial Times, Madagascar's regime leased the land to the South Korea's DAEWOO company for 99 years, and all the harvests during the period, had to be shipped back to feed South Koreans. The company paid nothing for the land, and the only promise to the government was the improvement of the country's infrastructure. This is the pattern across the continent. As long as the leaders can have posh homes, fat foreign bank accounts, and better education for their children abroad, they care less of their citizens. These African leaders have in the past inhumanely evicted, and burnt their citizens' houses at the expense of these neo- colonialists, food pirates, and land grabbing settlers

  In the case of Madagascar, The public was not informed of the land deal, and when the news leaked, the regime's life came to an abrupt ending. The country's leadership was toppled by the outraged population. The following leadership nullified the contract, declaring Madagascar's land neither for sale nor rent by foreigners. Natives many a times have had no significant gains in these deals, apart from providing slave labor. In a series of African leaders selling their countries, president Museveni In early 2000's, violently displaced his own people, and gave the land to a German coffee investor leaving his population in extreme poverty and despair.

  Millions of people around the continent have been violently driven out of their ancestral lands at the expense of land grabbers, and food pirates. It leaves us to wonder what's wrong with us Africans. Can w even think the basics? Can a Tanzanian national for instance go to Saudi Arabia, South Korea, India or even China and purchase 300 hectares of land? I took a big offence when a foreign politician told me that, an African is a big problem, especially when he has power, and a weapon. Indeed an African is a problem; he kills himself and blames it on foreign invaders. He rather trot the world looking for handouts, than take care of his diamonds and gold being stolen by foreigners. He is a pathetic creature that kills his own blood with a machete for money. An Africans is selling his land to foreigners to grow bio-fuel, yet he has no food. He is a slave in his own state of mind

  Tanzania has been, and is still facing hunger, and starvation caused by food shortages, even with her current smaller population. With projection of nearly 70million people by 2025, need for farmland, and water sources will be significant. Strain on these resources will be enormous and challenging, especially when the resources will be in the hands of foreigners. We have to realize that, there is no sanity, restraint, or tranquility where there is no food. We are likely to face internal lawlessness when people will have to deal with live or die situations due to lack of food. This tragedy will only be averted, if our future food security and sustainability planning takes into account the fact that our farmlands and water sources remains off limits for foreign lease, acquisition or purchase.

  Brazil moved to tighten her land ownership laws last year, in which no foreigner is allowed to purchase land. The same approach should be applied in Tanzania. We cannot allow foreign governments to ease their population congestion by taking advantage of our country to re-settle their land less. Tanzania is nobody's colony and is not going to be. We are a growing nation, leasing our land for 99 years to foreigners is a political suicide and betrayal to the people of Tanzania. Nationalists in the parliament of Tanzania must rise and confront this issue head on, be it in the East African Federation or Far East friends, Tanzania's land must be off limits.

  Our land and resources have no expiration date, and MUST remain out of bounds and completely out of the equation either through lease, or purchase by foreigners. Nyerere's administration regarded them so sacred, to an extent of leaving them intact for generations to come. Likewise, our present leadership must do the same as the current generation is in position to develop our land and its resources in very few years to come. We must adopt the Brazilians approach to maintain our future economic independence, and food security, averting the modern day economic colonization, food piracy, and land grabbing that is likely to ignite deadly survival conflicts of our times

  Mungu Ibariki Tanzania
  John Mashaka
  Mashaka.john@yahoo.com
   
 5. Msalagambwe

  Msalagambwe JF-Expert Member

  #5
  Jul 13, 2012
  Joined: Jul 11, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Watanzania,

  Twaipenda mno mno leo,
  nakuitolea kafara kesho,
  twatamani vya ghaibhu,
  twamtosa mama yetu.

  Uhuru wetu si kitu,
  si jambo muhimu kwetu,
  Fedha benki lukuki,
  ni bora kuliko uhuru.

  utitiri wa magari,
  majumba ya fahari,
  anasa na uzinzi,
  ni bora kuliko uhuru,

  Tunauza ardhi yetu,
  urithi wetu asilia,
  twaidharau mbachao,
  kwa msala upitao

  watu ni namba moja,
  upili ni ardhi,
  watu bila ardhi,
  ni kifo cha kibudu,

  Walipokuja mwanzo,
  kisa kilikuwa ardhi
  wanakuja tena upili,
  kisa kilekile Ardhi.

  Mara ngapi yatukute,
  ndipo tujifunze,
  mara ngapi waturubuni,
  ndipo tuzinduke?

  Zama zile shanga,
  Leo Dolali na magari,
  kutamani shanngingi
  ni kutamani shanga.

  Shangingi la mamilioni,
  ardhi bei gani?
  fedha ni makaratasi,
  ardhi bei gani?
  ufahari ukengeufu
  ardhi bei gani?

  Huu ni utumwa,
  tena utumwa wa kununua,
  twajitia utmwani
  kisa ufahari,
  twajitia utumwani,
  kisa fedha
  twajitia utumwani
  kisa uzinzi,
  twajitia utumwani
  twadhani utumwa mtamu

  Ardhi ni mama yetu,
  Ardhi ni asili yetu,
  twamuuza mama yetu
  kisa shanga,
  twamuuza mama yetu
  kisa shangingi.

  Nani anafaidi,
  Mauzo haya ya ardhi,
  Kamati kuu CCM!
  Ikulu magogoni!
  Ni UWT?
  Ni polisi au Mgambo?

  Ni ninyi JWTZ?
  Au wanachama wa CCM?

  Bunge la kulalama,
  Bunge lisilo na meno,
  Bunge la kupigwa nyuma,
  Bunge gani hilo?

  Hoja kuzifinyanga,
  Kapuni kuzitia,
  Ubabe kutawala,
  Spika na Ufisifisi.

  Hoja kuzipindua,
  sheria kuzipindisha,
  CCM kamati kibano,
  Wabunge kubanwa kende.

  Makaripio ya matusi,
  Bunge kugubikwa,
  Heshima mfyato,
  makalioni kuhifadhi.

  Wananchi wakati ni huu,
  Sheria mkoni kuchukua,
  Uhuru ni haki yetu,
  Ardhi ni haki yetu.

  Tupigane tufe tupone,
  heshima tuirudishe,
  adui yetu ni mweusi mwenzetu,
  nuksi mkoloni mweusi,
  Tusiogope mvi zao,
  wala sharubu zao nyeupe,
  kipigo koma tuwape,
  adabu kuwatia.

  sheria mkononi kuchukua,
  ndo dawa pekee sasa
  hogopwi afande kova,
  wala jack zoka,
  twashika kwa sharubu zenu,
  na kuwapa kipigo sawia,
  hawaogopwi wa ikulu,
  wala wapambe wake,
  wote njama zenu moja,
  utumwani tena kututia.

  shime wakati ni huu,
  sheria mkoni kuchukua.
   
 6. Msalagambwe

  Msalagambwe JF-Expert Member

  #6
  Jul 13, 2012
  Joined: Jul 11, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Mnyonge anapambanishwa na mnyonge ili mwenye nguvu avute kitu.

   
 7. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #7
  Jul 13, 2012
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Nimependa utabiri wa Mwl. J. K. Nyerere wa 1958 - "TANGANYIKA ITAMILIKIWA NA MATAJIRI WAGENI NA WENYEJI WATAKUWA WATWANA,"

  Kweli imetimia.
   
 8. Sn2139

  Sn2139 JF-Expert Member

  #8
  Jul 13, 2012
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 827
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Msalagambwe, shairi lako limetowa machozi na kunipa hamasa na chuki dhidi ya watawala. Hili lisambazwe nchi nzima
   
 9. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #9
  Jul 13, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,466
  Likes Received: 502
  Trophy Points: 280
  Kwa ubabe wa serikali Mbunge wa Kigamboni ametolewa nje kwa kutetea wananchi wake, hii haki kweli? kumbe kuna madiwani wamehongwa ili wakubali kuwa watu wa Kigamboni wanautaka mradi ilhali ni Uongo na Uzandiki mtupu! serikali hivi mnatafuta nini hasa kwa wananchi? mpaka lili uonevu huu? hebu kuweni na huruma na wananchi wenu kwanza !
   
 10. Msalagambwe

  Msalagambwe JF-Expert Member

  #10
  Jul 13, 2012
  Joined: Jul 11, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Asante Sn2139
  shime kunipa moyo pia,
  sifa kunimwagia,
  japo sistahili.

  Machozi yako si bure,
  Hamasa yamekutia,
  nguvu yamekujazia.

  Maono yamekuongeza,
  na kukutia mwingi ujasiri,
  Chozi la samaki majini,
  Binadamu halii BURE.

  Wenye nguvu ni wachache,
  Si tulio wanyonge ni wengi,
  uwngi wetu silaha tosha,
  uchache wao kaburi.

  Uwingi nguzo ya mnyonge,
  Umoja nguvu na fimbo.

  Mbiu hii tuisambaze,
  Kona zote waisikie,
  tuipige kama zeze,
  tuimbe na kucheza.

  Tumia mzao wa sayansi,
  Teknolojia ya mtandao,
  Magazeti wameyahodhi,
  Wahariri wadondoka nao.

  Intaneti mali yetu,
  Wanyonge tuitumie,
  Visemea mkononi pia,
  Ujumbe tupeane.  Ndugu zangu Watanzania,
  Mama yetu mali ya ghaibhu,
  amtumia apendavyo,
  Amfuja na kumchosha.

  Amtia unnajisi na dhihaka,
  ucchi kumwacha asilani.

  Maziwa ya mama wanywa,
  Sie twafa kwa dhiki,
  malimbuko yake wachuma,
  nakutuacha watupu.

  Wakati ndo huu ndugu zangu,
  ukombozi tuushike,
  Umoja fimbo yetu,
  Tumkomboe mama yetu.


   
 11. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #11
  Jul 13, 2012
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  kuna siku tutachoka, na hii nchi itakuwa syria
   
 12. Asa'rile

  Asa'rile JF-Expert Member

  #12
  Jul 13, 2012
  Joined: Jun 29, 2012
  Messages: 426
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu, alisema serikali imejigeuza wakala, dalali na kuwadi wa wawekezaji kwa kutumia nguvu kuwanyang'anya ardhi wananchi.Ninachojua ni kuwa Watanzania ni Simba waliolala..Sasa wakati wa kuamka Simba huyo ni sasa
   
Loading...