Nchi imetekwa na genge la Mafia?

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,004
Nchi imetekwa na genge la Mafia?

Joseph Mihangwa Mei 7, 2008
Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo

KWA lugha ya kigeni linaitwa "Mafia group," yaani "Genge la uhalifu."
Linaweza kuwa la ndani, la kimataifa au yote kwa kushirikiana katika nchi moja.

Katika nchi kama Italia, Columbia, Marekani na hata Urusi, genge hili lina nguvu sana, na serikali yoyote ikitaka kupambana nalo, inapaswa kujizatiti kikamilifu.

Huendesha serikali isiyo rasmi, lakini yenye nguvu kuliko hata serikali halali madarakani. Huendesha biashara kubwa kwa magendo ikiwamo pia ile inayoitwa biashara haramu ya fedha (money laundering) na biashara ya dawa za kulevya.

Lina vikosi vyake vya mauaji. Humuondoa yeyote anayeonekana kuwa kikwazo katika kutimiza malengo yake. Halijali cheo cha mtu, hata kama ni rais, waziri mkuu, jaji, mkuu wa jeshi la polisi au hata wakili "machachari" (mkali) anayepambana na mafisadi mbele ya sheria.

Mauji yanayofanywa na genge hili kwa walengwa wake yanaweza kuwa kwa njia ya kudhuru mwili au kudhuru kisiasa. Genge la Mafia linaweza kupenyeza watu wake katika taasisi nyeti za utawala wa nchi, ukiwamo utumishi wa umma, kuhakikisha kwamba serikali inatumikia uharamia zaidi kuliko kutumikia umma, na mipango ya nchi kulenga kunufaisha maharamia wa kimataifa na washirika wake nchini badala ya malengo ya kitaifa kwa ustawi wa wananchi.

Linaweza pia kupenyeza watu wake ndani ya jeshi la polisi ili kuhakikisha kwamba uhalifu haushughulikiwi ipasavyo ili kutoa nafasi kwa maharamia kuendesha shughuli zake bila kufuatiliwa au kudhibitiwa.

Genge hili laweza kupenyeza watu wake katika nyanja za kijamii kama vile siasa na dini kuhakikiaha kwamba taasisi hizo na nyinginezo zinapoteza dira juu ya maendeleo ya binadamu.

Bunge ni taasisi nyeti inayowakilisha matakwa ya wananchi. Bunge ndilo demokrasia yenyewe kazini. Bunge la nchi iliyotekwa na Mafia huwa na sura kama wabumbe kuingia kwa ushindi wa mizengwe na "takrima" na kutafuta maslahi binafsi badala ya uwakilishi wa wananchi.

Pili, ni bunge lisilowakilisha tabaka la walio wengi ndani ya jamii. Badala yake hujaza wafanyabiashara, wasomi na wanataaluma walioziasi taaluma zao na kusababisha upungufu mkubwa wa wataalamu kwa nchi.

Ili kuhakikisha kwamba wabunge hawapati nafasi ya kuhoji ufisadi hupenyeza watu wake bungeni na wenhine hupewa ukurugenzi katika kampuni za kifisadi, mbali na "takrima" kwa lengo la kuwanyamazisha na kulinda miradi ya mafisadi. Bunge hugeuzwa kuwa la mijadala ya mizaha na klabu ya wakubwa kukutana, na kwa mawakala wa genge hilo kujifunza siri na mbinu za serikali.

Yanayojiri nchini sasa hayana tofauti sana na sura tajwa juu. Unaweza kuamini kwamba Tanzania imetekwa na genge la Mafia. Hakuna sababu za msingi kwa Serikali kulea ufisadi wa wazalendo waliowekwa madarakani na umma kama si kwa ushawishi wa genge la Mafia.

Chanzo cha tatizo kinaweza kuwa ni udhaifu wetu wa kizalendo, hususani uchu wa madaraka na utawala kwa nguvu ya fedha. Tuliamini tangu mwanzo kwamba Tanzania itajengwa na wenye moyo. Ni viongozi wangapi leo wanachukua uongozi kwa nia ya kujenga nchi ?

Ni udhaifu wa chama tawala. Kiongozi mmoja mkubwa serikalini alipata kusema miaka ya karibuni : "Mfanya biashara yoyote akitaka mambo yamnyokee, aingie CCM." Tangu hapo chama tawala kimeingiza ndani wafanyabiashara (ambao si wanasiasa) kugombea nafasi za uongozi na kufadhili chama kwa malengo tofauti kabisa na matakwa, maadili na mwelekeo wa Taifa .

Haingii akilini kwa Mtanzania mfia nchi , kuelezwa na kuamini kwamba Gavana wa zamani wa Benki Kuu, Dk. Daudi Ballali hatafutwi na Serikali wakati kuna tuhuma dhidi yake.

Wala haingii akilini kuambiwa kwamba watu wanaorudisha fedha za EPA walizo pora Benki kuu hawastahili kukamatwa wala kuhojiwa mapaka Tume ya Serikali ikamilishe kazi yake.

Hivyo hivyo, haileti mantiki kwa kiongozi mtuhumiwa wa ufisadi kuachwa kuendelea na wadhifa wake katika kipindi cha kuchunguzwa. Mbona si hivyo kwa watumishi wengine wa umma? Je, tumefika mahali tumeanza kubeza misingi ya "utawala wa sheria" tunaodai kutetea chini ya Katiba. Giza halifukuzwi kwa mayowe ya "giza ondoka", bali kwa mwanga. Tunataka viongozi wenye mwanga badala ya viongozi "wachoji" na wafanyabiashara ofisini.

Tunajua tunao viongozi shupavu nchini ambao ni tumaini la wanachi kwa ukombozi wao. Lakini tumaini hilo linabaki njia panda tunapoona viongozi wanaelekea ama kukata tamaa au kukubali kushindwa.

Wananchi wangependa kufahamishwa hatua zinazochukuliwa na Serikali yao dhidi ya ufisadi na dhidi ya watuhumiwa wanaotajwa tangu awamu ya tatu hadi sasa, hususani juu ya sakata la IPTL, Biashara Ikulu, ufujaji katika mifuko ya wadundakazi ya " hifadhi ya jamii" uliofanywa na mtandao wa Mafia, na mengine.

Inavyoonekana Serikali inayapapasa tu (kwa kuzima taa) maovu haya kwa kumwangalia "nyani usoni." Ni hoja za umma (public opinion) zinazoisukuma Serikali bila kupenda, bila hivyo ingependa kuyaficha uvunguni maovu haya kwa kufunika kombe mwanaharamu apite. Iweje Serikali inywee kila watuhumiwa wanapotishia kuwataja vigogo washiriki iwapo watafikishwa mahakamani au kuwajibishwa?

Je, haikusemwa kwamba wale wanaoishi kwenye nyumba za vioo wasijaribu kuwatupia mawe wapita njia? Bila shaka vigogo wetu wanaogopa kufanya hivyo ili nyumba yao ya vioo isije kuangushwa na mvua ya mawe ya wapita njia.

Genge hili la Mafia linaundwa na kina nani? Na kwanini Serikali inapata kigugumizi mara kwa mara juu ya hatua za kuchukua? Ukitazama maudhui mazima ya ufisadi nchini, huwezi kujizuia kuamini kwamba mtandao huo unawahusisha wanasiasa waandamizi, vigogo katika dola na baadhi ya wafanyabiashara wakubwa na watendaji wakuu serikalini. Ndiyo maana mzunguko huu wa kiharamia unaweza kuhujumu nchi kwa raha bila hofu ya kuhojiwa ; unaweza kuhamisha fedha za maendeleo kuzipeleka kule unaotaka ziende - ( Meremeta, Tangold, Kagoda na kwingineko.)

Tunajua kila serikali madarakani hupenda ibakie hivyo, lakini inapofanya hivyo kwa maangamizi ya wananchi na mstakabali wa taifa, badala ya kupigania haki za raia wote, elimu, maji, afya na vita zidi ya umasikini, inakuwa ni kulinda maslahi ya vikundi hasidi kwa taifa na maisha ya watu, serikali hiyo lazima ihojiwe.

Wala serikali yoyote haiwezi kutawaliwa na agenda pekee ya uchaguzi ujao au kubakia madarakani (kwa kubembeleza wafadhili waovu?) badala ya kufikiria maendeleo ya watu. Huo ni uchu wa madaraka usiojenga, wanasiasa na watawala ni watu wakupita, lakini taifa ni la kudumu milele.Nchi haiwezi kuendelea kwa kuongozwa na watawala "wachoji" – watafuta mali na biashara madarakani.

Lakini ukweli utabaki palepale kwamba ubinafsishaji bora ni ule wenye baraka kutoka kwa wananchi; kwani wao ndio wenye mali, na serikali huundwa na kupata nguvu kutoka kwao.

Mwisho ni kuhusu heshima na uadilifu wa viongozi. Inakuaje kiongozi wa juu serikalini,kama waziri, anapoboronga nafasi hiyo ajidai kurejea kujikosha kwa wananchi, kwamba alichoharibu ni uwaziri na sio ubunge? Hivi uwaziri si utumishi wa umma kama ulivyo ubunge?

Waziri anapokuwa bungeni huwakandia wabunge kuwa yeye ni sehemu ya mhimili wa Utawala, wenye kuweka ngome ya utetezi wa hoja za Serikali dhidi ya hoja za wabunge. Hivi ni sahihi kwa waziri huyo anapoporomoka kuwakumbuka wale aliokuwa akiwakandia bungeni ? Je, hiyo siyo aibu tupu?

Shabaan Robert anaiita hiyo ni Aibu ya Roho kwa kusema:

"Mtu asiye heshima, aibu ya roho yake,
Mfano wake tazama, kama popo mwendo wake;
Wanaposhindwa wanyama, hudai ndege wenzake,
Na ndege sio wenzake, wanaposhinda wanyama.

Na siku ya mapatano, ya ndege na wanyama,
Yeye huwa na miguno, halipati la kusema,
Hana masikilizano, kwa ndege wala wanyama,
Mtu kamaye daima, ni aibu kubwa mno.

0713-526972
 
Kwani hii ni siri au? Ni kitendo cha kuuliza abt 51% of wabunge wa CCM campaign funds zilipotoka...kinachoshangaza ni kwamba with CCM you can actually win without the money..watu vijijini still vote green...was all that money necessary...only time will tell....
 
Nchi imetekwa na genge la Mafia?

Joseph Mihangwa Mei 7, 2008
Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo

KWA lugha ya kigeni linaitwa “Mafia group,” yaani “Genge la uhalifu.”
Linaweza kuwa la ndani, la kimataifa au yote kwa kushirikiana katika nchi moja.

Katika nchi kama Italia, Columbia, Marekani na hata Urusi, genge hili lina nguvu sana, na serikali yoyote ikitaka kupambana nalo, inapaswa kujizatiti kikamilifu.

Huendesha serikali isiyo rasmi, lakini yenye nguvu kuliko hata serikali halali madarakani. Huendesha biashara kubwa kwa magendo ikiwamo pia ile inayoitwa biashara haramu ya fedha (money laundering) na biashara ya dawa za kulevya.

Lina vikosi vyake vya mauaji. Humuondoa yeyote anayeonekana kuwa kikwazo katika kutimiza malengo yake. Halijali cheo cha mtu, hata kama ni rais, waziri mkuu, jaji, mkuu wa jeshi la polisi au hata wakili “machachari” (mkali) anayepambana na mafisadi mbele ya sheria.

Mauji yanayofanywa na genge hili kwa walengwa wake yanaweza kuwa kwa njia ya kudhuru mwili au kudhuru kisiasa. Genge la Mafia linaweza kupenyeza watu wake katika taasisi nyeti za utawala wa nchi, ukiwamo utumishi wa umma, kuhakikisha kwamba serikali inatumikia uharamia zaidi kuliko kutumikia umma, na mipango ya nchi kulenga kunufaisha maharamia wa kimataifa na washirika wake nchini badala ya malengo ya kitaifa kwa ustawi wa wananchi.

Linaweza pia kupenyeza watu wake ndani ya jeshi la polisi ili kuhakikisha kwamba uhalifu haushughulikiwi ipasavyo ili kutoa nafasi kwa maharamia kuendesha shughuli zake bila kufuatiliwa au kudhibitiwa.

Genge hili laweza kupenyeza watu wake katika nyanja za kijamii kama vile siasa na dini kuhakikiaha kwamba taasisi hizo na nyinginezo zinapoteza dira juu ya maendeleo ya binadamu.

Bunge ni taasisi nyeti inayowakilisha matakwa ya wananchi. Bunge ndilo demokrasia yenyewe kazini. Bunge la nchi iliyotekwa na Mafia huwa na sura kama wabumbe kuingia kwa ushindi wa mizengwe na “takrima” na kutafuta maslahi binafsi badala ya uwakilishi wa wananchi.

Pili, ni bunge lisilowakilisha tabaka la walio wengi ndani ya jamii. Badala yake hujaza wafanyabiashara, wasomi na wanataaluma walioziasi taaluma zao na kusababisha upungufu mkubwa wa wataalamu kwa nchi.

Ili kuhakikisha kwamba wabunge hawapati nafasi ya kuhoji ufisadi hupenyeza watu wake bungeni na wenhine hupewa ukurugenzi katika kampuni za kifisadi, mbali na “takrima” kwa lengo la kuwanyamazisha na kulinda miradi ya mafisadi. Bunge hugeuzwa kuwa la mijadala ya mizaha na klabu ya wakubwa kukutana, na kwa mawakala wa genge hilo kujifunza siri na mbinu za serikali.

Yanayojiri nchini sasa hayana tofauti sana na sura tajwa juu. Unaweza kuamini kwamba Tanzania imetekwa na genge la Mafia. Hakuna sababu za msingi kwa Serikali kulea ufisadi wa wazalendo waliowekwa madarakani na umma kama si kwa ushawishi wa genge la Mafia.

Chanzo cha tatizo kinaweza kuwa ni udhaifu wetu wa kizalendo, hususani uchu wa madaraka na utawala kwa nguvu ya fedha. Tuliamini tangu mwanzo kwamba Tanzania itajengwa na wenye moyo. Ni viongozi wangapi leo wanachukua uongozi kwa nia ya kujenga nchi ?

Ni udhaifu wa chama tawala. Kiongozi mmoja mkubwa serikalini alipata kusema miaka ya karibuni : “Mfanya biashara yoyote akitaka mambo yamnyokee, aingie CCM.” Tangu hapo chama tawala kimeingiza ndani wafanyabiashara (ambao si wanasiasa) kugombea nafasi za uongozi na kufadhili chama kwa malengo tofauti kabisa na matakwa, maadili na mwelekeo wa Taifa .

Haingii akilini kwa Mtanzania mfia nchi , kuelezwa na kuamini kwamba Gavana wa zamani wa Benki Kuu, Dk. Daudi Ballali hatafutwi na Serikali wakati kuna tuhuma dhidi yake.

Wala haingii akilini kuambiwa kwamba watu wanaorudisha fedha za EPA walizo pora Benki kuu hawastahili kukamatwa wala kuhojiwa mapaka Tume ya Serikali ikamilishe kazi yake.

Hivyo hivyo, haileti mantiki kwa kiongozi mtuhumiwa wa ufisadi kuachwa kuendelea na wadhifa wake katika kipindi cha kuchunguzwa. Mbona si hivyo kwa watumishi wengine wa umma? Je, tumefika mahali tumeanza kubeza misingi ya “utawala wa sheria” tunaodai kutetea chini ya Katiba. Giza halifukuzwi kwa mayowe ya “giza ondoka”, bali kwa mwanga. Tunataka viongozi wenye mwanga badala ya viongozi “wachoji” na wafanyabiashara ofisini.

Tunajua tunao viongozi shupavu nchini ambao ni tumaini la wanachi kwa ukombozi wao. Lakini tumaini hilo linabaki njia panda tunapoona viongozi wanaelekea ama kukata tamaa au kukubali kushindwa.

Wananchi wangependa kufahamishwa hatua zinazochukuliwa na Serikali yao dhidi ya ufisadi na dhidi ya watuhumiwa wanaotajwa tangu awamu ya tatu hadi sasa, hususani juu ya sakata la IPTL, Biashara Ikulu, ufujaji katika mifuko ya wadundakazi ya “ hifadhi ya jamii” uliofanywa na mtandao wa Mafia, na mengine.

Inavyoonekana Serikali inayapapasa tu (kwa kuzima taa) maovu haya kwa kumwangalia “nyani usoni.” Ni hoja za umma (public opinion) zinazoisukuma Serikali bila kupenda, bila hivyo ingependa kuyaficha uvunguni maovu haya kwa kufunika kombe mwanaharamu apite. Iweje Serikali inywee kila watuhumiwa wanapotishia kuwataja vigogo washiriki iwapo watafikishwa mahakamani au kuwajibishwa?

Je, haikusemwa kwamba wale wanaoishi kwenye nyumba za vioo wasijaribu kuwatupia mawe wapita njia? Bila shaka vigogo wetu wanaogopa kufanya hivyo ili nyumba yao ya vioo isije kuangushwa na mvua ya mawe ya wapita njia.

Genge hili la Mafia linaundwa na kina nani? Na kwanini Serikali inapata kigugumizi mara kwa mara juu ya hatua za kuchukua? Ukitazama maudhui mazima ya ufisadi nchini, huwezi kujizuia kuamini kwamba mtandao huo unawahusisha wanasiasa waandamizi, vigogo katika dola na baadhi ya wafanyabiashara wakubwa na watendaji wakuu serikalini. Ndiyo maana mzunguko huu wa kiharamia unaweza kuhujumu nchi kwa raha bila hofu ya kuhojiwa ; unaweza kuhamisha fedha za maendeleo kuzipeleka kule unaotaka ziende - ( Meremeta, Tangold, Kagoda na kwingineko.)

Tunajua kila serikali madarakani hupenda ibakie hivyo, lakini inapofanya hivyo kwa maangamizi ya wananchi na mstakabali wa taifa, badala ya kupigania haki za raia wote, elimu, maji, afya na vita zidi ya umasikini, inakuwa ni kulinda maslahi ya vikundi hasidi kwa taifa na maisha ya watu, serikali hiyo lazima ihojiwe.

Wala serikali yoyote haiwezi kutawaliwa na agenda pekee ya uchaguzi ujao au kubakia madarakani (kwa kubembeleza wafadhili waovu?) badala ya kufikiria maendeleo ya watu. Huo ni uchu wa madaraka usiojenga, wanasiasa na watawala ni watu wakupita, lakini taifa ni la kudumu milele.Nchi haiwezi kuendelea kwa kuongozwa na watawala “wachoji” – watafuta mali na biashara madarakani.

Lakini ukweli utabaki palepale kwamba ubinafsishaji bora ni ule wenye baraka kutoka kwa wananchi; kwani wao ndio wenye mali, na serikali huundwa na kupata nguvu kutoka kwao.

Mwisho ni kuhusu heshima na uadilifu wa viongozi. Inakuaje kiongozi wa juu serikalini,kama waziri, anapoboronga nafasi hiyo ajidai kurejea kujikosha kwa wananchi, kwamba alichoharibu ni uwaziri na sio ubunge? Hivi uwaziri si utumishi wa umma kama ulivyo ubunge?

Waziri anapokuwa bungeni huwakandia wabunge kuwa yeye ni sehemu ya mhimili wa Utawala, wenye kuweka ngome ya utetezi wa hoja za Serikali dhidi ya hoja za wabunge. Hivi ni sahihi kwa waziri huyo anapoporomoka kuwakumbuka wale aliokuwa akiwakandia bungeni ? Je, hiyo siyo aibu tupu?

Shabaan Robert anaiita hiyo ni Aibu ya Roho kwa kusema:

“Mtu asiye heshima, aibu ya roho yake,
Mfano wake tazama, kama popo mwendo wake;
Wanaposhindwa wanyama, hudai ndege wenzake,
Na ndege sio wenzake, wanaposhinda wanyama.

Na siku ya mapatano, ya ndege na wanyama,
Yeye huwa na miguno, halipati la kusema,
Hana masikilizano, kwa ndege wala wanyama,
Mtu kamaye daima, ni aibu kubwa mno.

0713-526972

mzee haya mambo ya copyrightutaua shekhe

Jana tulishayazungumza

weka first paragraph na kisha weka link ndani ya quote
 
mzee haya mambo ya copyrightutaua shekhe

Jana tulishayazungumza

weka first paragraph na kisha weka link ndani ya quote

Ulizungumza na nani? Wewe ukiwa kama nani hapa JF? Kama wewe unakosa usingizi na hizi article basi hujalazimshwa kuzisoma. Sijaona katika gazeti lolote la Tanzania linalotaka kufungua mashtaka dhidi ya JF kwa kutumia article zao hapa ukumbini. Mimi sinufaiki kwa kuweka hizo habari hapa hali kadhalika JF hainufaiki kifedha. Hebu acha kutaka kuvuruga mtitiriko wa habari hapa JF.
 
Bubu, that was a brass knuckled, mean ass assault to the jugular!

Ha haa ahaaaaa! Sorry, couldn't help it. Talk about freedom of information! Let's defend it to the death, hanh?
 
Ha ha ha sometimes you have to put uungwana aside, of course I know about copyrights issues, but so far I have not read anything about any media in Tanzania who are planning to sue JF in regards to usage of their articles. GT was one of my favorites posters on JF, but lately I don't know what is going with him.
 
Bubu,
Itakuwa vema kama utatumia link badala ya long story kweli inaboa,huu ni ushauri tu mzee.
 
Weken story BUBU bila kujali.

Najibu swali kama tumetekwa na MAFIA ama laa, kwani huu ndeio mjadala ila GTamefanikiwa kuwafany7a watu wasijadili hoja za msingi ila badala yake anataka kuibua kitu kipya ili tuache kusema na kuwataja hao mafia hapa.

Nchi imetekwa na MAFISADI kwani mpaka sasa hawana sifa yeyote ya kuitwa MAFIA ,na hivyo kutokana na ufisadi wao wanajikuta sasa nchi inaelekea kuwaelemea kila kukicha.

Kama taifa kuna watu ambao naamini kuwa wanatakiwa kufikishwa mbele ya vyuombo vya kisheria na hata ikibidi mahakama za kimataifa kwani wamekuwa wakuwatesa na kuwanyanyasa wanyonge wa taifa hili, angalia kule Pemba hakuna haki hata kidogo, ni manyanyaso tuu kila kukicha.

Mafisadi haya yanalindana sana sana na kuna siku haki itatendeka na kila fisadi atalia na kusaga meno.
 
Haya...Gigo ndio alikua anatumia neno Genge!!akimaanisha CCM lakini Hakuna Genge La ajabu!! Tanzania...Ni Ujinga...acheni kuumiza vichwa!!
 
Bubu,
Itakuwa vema kama utatumia link badala ya long story kweli inaboa,huu ni ushauri tu mzee.

Tatizo ni kuboa? Kuboa maana yake nini? Ukienda kuisoma kwenye link huko ndio hutakuwa bored? Na ukianza kuwa bored katikati ya story si unaitosa. Sielewi unawezaje kuwa bored na stori ambayo si lazima uisome. Umesema ni ushauri tu, lakini wewe ndio hupendi mabandiko, wengine tunaona ni poa. Labda ungesema ni ombi la kukusaidia wewe, sio kutushauri sisi. Sisi tunaona ni poa!

Uzuri wa kubandika taarifa nzima hapa ni kurahisisha marejeo ya nini tunakiongelea. Ukieenda kwenye link unatoka JF halafu kurudi tena inakuwa hatua isiyokuwa ya lazima. Ni rahisi pia ku dissect vipengele kwa vipengele kwa urahisi kwa sababu unaweza ku cut and paste kipande cha stori unachotaka kukilenga. Ukianza ku cut and paste btn websites kanakuwa ka shughuli ambako sio lazima. Halafu kule kwenye ma link kuna wakati yanatolewa. Tunataka rekodi zibakie hapa.

Ishu ya msingi ilikuwa ni haki miliki. Lakini kama Bubu alivyosema, hatujasikia mtu kulalamika. Hicho kitu hatukijui na kingekuwepo tungekijua!
 
Back
Top Bottom