Nchi imepoteza zaidi ya dola milioni 500 kutokana na uamuzi wa Serikali kununua korosho

Munjombe

JF-Expert Member
Dec 10, 2018
1,937
2,632
Nchi imepoteza zaidi ya dola milioni 500 kutokana na uamuzi wa serikali kununua korosho za wakulima na kutaka zibanguliwe na viwanda vya ndani.
--------------
Katazo la Serikali la kuuza korosho nje ya nchi limesababisha pengo kwa Tanzania katika salio la malipo na kuwepo upungufu wa takribani Dola500 milioni kwa mwaka ulioishia Novemba 2018.

Ripoti ya mwezi ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ya Desemba 2018 imeonyesha mlinganyo wa jumla wa malipo wa (BoPs) ukiwa na upungufu wa Dola 753.0 milioni kwa mwaka ulioishia Novemba 2018 ikilinganishwa na upungufu wa Dola 171.6 milioni iliyorekodiwa Oktoba ya mwaka huo.

Ripoti hiyo inasema mapato ya mauzo ya korosho ambalo ni zao linaloongoza kwa mauzo ya nje ya nchi yameshuka kutokana na uamuzi wa Serikali kununua korosho za wakulima na kuzibangulia katika viwanda vya ndani.

Mauzo ya korosho nje ya nchi yamekuwa yakifikia Dola 575 milioni, mauzo hayo ambayo ni sawa na mauzo ya mazao mengine matano ya biashara kama tumbaku, chai, kahawa na katani.

Hivi karibuni Serikali ilitangaza kununua zaidi ya tani 200,000 za korosho kutoka kwa wakulima katika mikoa inayozalisha kwa wingi zao hilo tayari kwa kuuza nje ya nchi baada ya kuzibangua kwa viwanda vya ndani.

Chanzo: Mwanachi
 
Ripoti ya mwezi ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ya Desemba 2018 imeonyesha jinsi zuio la Serikali ya Tanzania la kutokuuza korosho nje ya nchi ambayo haijabanguliwa ilivyoshusha mapato ya zao hilo

koroshopic.jpg
 
Nchi imepoteza zaidi ya dola milioni 500 kutokana na uamuzi wa serikali kununua korosho za wakulima na kutaka zibanguliwe na viwanda vya ndani.

Chanzo: Mwanchi online/BOT
Ayani husu kabisa, nataka malipo ya korosho zangu, kulipa kilo 200, 300. Hazina tija kwangu, mkulima mwenye malengo amevuka huko. Lipa korosho. Na uje kuhakiki mashamba ukipenda, mambo ya subiri subiri hatutaki.
 
Wale tuliokuwa hatuaamini alichoandika Ben saanane kuhusu PhD ya bwana Huyu ndo tumeanza kuelewa. Tukifanya vetting sawasawa huenda hata masters degree na bachelor degree ni magumashi pia
 
Back
Top Bottom