Recta
JF-Expert Member
- Dec 8, 2006
- 855
- 38
Nchi imemshinda..kivipi? toa vigezo na measurement
Chama imemshinda..kivipi? toa vigezo na measurment?
otherwise hizo ni wishes zako ndugu...nchi inaende mbele tunachoona na malalamiko na uwazi katika kuendesha serikali..lol msitake kuturudisha huko kwa |Nyerere siri siri kila kitu lol
Mkuu kuna vigezo, mifano na vipimo vya kutosha kabisa kuelezea jinsi nchi inavyomshinda Mkuu wetu.
Nchi imemshinda:
1. Hakuna misingi ya utawala inayoeleweka
2. Hakuna mikakati ya maendeleo yanayoeleweka
3. Hakuna nidhamu ya kiutawala
4. Hakuna kauli yoyote anayoitoa kwa viongozi ndani ya serikali yake inayofanyiwa kazi
5. Hakuna hatua zozote zinazochukuliwa kwa viongozi wanaokwenda kinyume cha sheria za nchi
6. Kila kiongozi anafanya anavyojisikia mwenyewe. No controls
7. Wananchi wengi wanalalamika kuhusu hali ya uongozi wa nchi na hasa serikali yake
8. Viongozi kukashifiana hadharani
9. Kuwa mkimya katika mambo nyeti yanayohitaji uongozi thabiti kutoka kwake
10. Serikali yake imekosa ufanisi. projects nyingi zimekwama
11. Ufisadi ndio sifa kuu ya kiongozi bora
Chama kimemshinda:
1. Ndio maana ameunda Kamati ya Mwinyi, Kinana na Msekwa ili kumsaidia
2. Viongozi wa chama wamefaraganyika. Hakuna umoja wa kichama tena
3. Visasi vya kisiasa ndio mkakati wa uongozi wa chama
4. Chama kimehama kutoka chama cha wakulima na wafanyakazi hadi kuwa chama cha wafanya biashara, wala rushwa na wasanii
5. Hakuna imani ya CCM inayotumika kukijenga chama. Na wanaojaribu kutumia imani hizo wanakuwa maadui
6. Ahadi zote alizotoa katika kampeni baada ya kuteliwa 2005, hazijatekelezeka. Ikiwa ni pamoja na mpasuko wa Zanzibar. Ushirikiano/Uhisiano kati ya Bara na visiwani unadhoofika siku hadi siku