Chromium
JF-Expert Member
- Apr 17, 2008
- 589
- 186
Nazungumza kwa masikitiko makubwa. Ninasononeka. Ninaandika nikilia. Navuta machozi nikitafakari pepo mchafu anawasumbua watawala wetu.
Hakuna asiyetambua kuwa nchi yetu inayumba. Nchi imekosa mwongozaji. Nchi imepoteza dira. Nchi inakwenda pasipofahamika. Nchi haieleweki inakopelekwa.
tuliowachagua, wanaiba kwa kasi mpya, wakikingiana kifua. Nchi inaliwa. Nchi inalika. Nchi inamalizwa. Nchi inafilisiwa na genge la walafi wachache wanaojidai kuwa hatuelewi wanavyoinajisi nchi yetu. Ninaumia. Ninasikitika. Ninaogopa. Mpka lini mambo haya? Mpaka lini? Kwa nini haya majitu yanajiamini hivi?
Hayo ndiyo ninayokusudia kushirikishana nani wana Jambo. Ninalo jambo la kusema. Nimeamua kutoka kichakani niseme niliyonayo. Kusema kutaniweka huru. Naomba msinielewe vibaya.
Nashindwa kuandika kwa machozi niliyonayo. Nitaendelea nikinyamaza.